Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Nilipoteza dada zangu wawili in raw mmoja 2008 mwingine 2009 kipindi hicho ukikutwa na ukimwi unaambiwa usubiri cd4 sijui zipande mara zishuke hii hali ya kusubiri ndio ulikuwa mtihani sana dada zangu walikufa huyo mmoja alisepa na mwanae mdogo,kiukweli Ukimwi sikia kwa jirani ila sio kwako
 
Hiyo ndo iringa mzee,sio kabisa yaani...kuna sehemu inaitwa ndiuka,ipo pembezoni mwa barabara ya morogoro au barabara ya zambia,hiyo sehemu 80%ya wakazi wana ngwengwe...ukienda iringa enda kwa brake usijifanye gangwe utasahaulika mapema.
 
Ninachoshangaa...kwenye mazishi yote niliyohudhurua,sijawai sikia historian ya marehemu Kwamba Amekufa kwa gonjwa la UKIMWI,,,, hapo ndo naamini UKIMWI unatisha
Nilihudhuria semina moja hiv walinisaidia kunielekeza jambo kama la kwako!
Iko hiv kamwe katika maisha yako hautakuja kusikia mtu amekufa kwa UKIMWI maana ukimwi ni upungufu wa kinga mwili kwanza inqbidi utambue kwanza.
Hivyo hii inasababisha Mgonjwa anapoumwa gonjwa fulan lqbda tuseme maralia au kifua au amonia ni kwamba kinga zake zimeshindwa au kushuka kupambana na ugonjwa huo. Hivyo unaweza kuwa na hilo shida ila kinachokuua ugonjwa fulani ambao kinga zako zimeshindwa kupambana nazo.
Ndo mtu anaweza kuwa hana maambukizi hya ukimwi lakin akafa kwa ugonjwa wa fulan hivyo wanasema kinga zako zimeshindwa kupambana na tatizo hilo.
Ndo maana wataalamu wanakuambia kila mtu ni mgonjwa wa Ukimwi. Hivyo kqmwe hautakuja kusikia mtu amekufa kwa UKIMWI.
 
Da UKIMWI hatari,nmempoteza Maza mdogo 1998 iyo mbeya,Iringa (mfindi) kiwanda cha chai kipindi maza nurse iyo Hospital ya blukubond nmekaa kama ten years,nikamzika uncle alikuwa mwalimu.

Back days 2016 nmemzika sister,so sad aliletewa ugonjwa na mumewe(R.I.P) blood.

Tatizo lipo vijana tujilinde ,tuzipende afya zetu ,hususani tunaokula viombo uko ndo hatari kubwa sana
 
Nimekaa mufindi 15 yrs niliondoka kule 2012! Napajua vizuri sana..sema basi haturuhusiwi kuweka majina huyo mamdogo wako huenda ningemfahamu.! I love the Nature kule, baridi balaaa, Napamisi Mufindi Club e.t.c..kule nilikataa kurudi tena maana HIV ipo kwa kiwango kikubwa sana
 
NB. Msiache kutumia kondomu kuna UTI sugu, kisonono, kaswende, homa ya ini na mimba zisizotarajiwa ila UKIMWI hakuna
Acha kudanganya watu. UKIMWI upo na unafyeka sana. Tena hiki kizazi cha vijana wa 1990s na 2000s wako less sana na vitobo in 20 years wataanza kuanguka, tusipojicheki tutakuwa na taifa la wazee ambao ni generation ya 70s na 80s. Awareness iko chini sana hao TACAIDS tu siku hizi husikii matangazo yao tena kama enzi za "Pande na UKIMWI" ARV zina ukomo. Chukua tahadhari.
 
VERY TRUE,KWELI KABISA,mimi ni shuhuda wa hili jambo,miaka hiyo, baadhi ya watu nawafahamu,kwenye eneo husika,...NGOMA,ilifyeka maeneo yote uelekeo wa Iringa,Pale Rungema ilikuwa mtihani,njoo mpaka Ulete na Ifunda washkaji kibao tumewapoteza hasa msimu wa ulanzi ukisogea mbele kidogo Tanangozi ilikuwa ndio parking kubwa ya malori mademu kibao mitungi n.k...pale ndio palifutika kabisa na magari yakawa haya simami tena ilikuwa ni mahame,ashukuruwe MUngu pameanza kufufuka tena miaka hii,miaka hiyo palikuwa pamechangamka kuliko Ilula.
 
Ukimwi ni mastory ya kizamani siku hizi hakuna mtu anaogopa. Watu wanaogopa kansa na kisukari siku hizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…