Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Sitosahau UKIMWI ulichofanya mtaani kwetu. Nyie watu wa mapenzi kuweni makini

Wanawake wengi usalama ni mdogo hasa kwenye hizi meetings za upcountry! Wengi wanaachia sana hata awe vipi!
Mara nyingi, ingawa siyo wote, wanawake wengi wanapenda kupendwa, kuthaminiwa, kupandishwa hadhi mbele ya wanawake wenzao, kupewa majawabu ya changamoto zinazomzunguka, kupata matokeo chanya kwa muda mfupi (kufanikiwa), na hawataki na hawahimili stress. Kadhalika, wanawake wengi wanapenda mwanaume anayependwa na wengi hata kama malaya. Kingine mwanamke akiwa tu karibu na mtu akazoeana naye ufungua code za udhaifu wake wa kuachia mzigo kwa mtu huyo, hata kama mtu huyo mtu anamwonekano special.

Akitokea mdau akawa ana sifa tajwa hapo juu au anamudu kutekeleza hayo ni vigumu sana mwanamke kuchomoa hata awe ameolewa, au mgumu vipi, labda awe na changamoto ya kimsingi inayomzuia kugawa dodo.

Wafanyakazi, class mate, Jogging mate, watoa huduma kama madaktari, mahakimu, wakufunzi, walimu, bodaboda n.k wana nafasi kubwa sana ya kupafikia panapofichwa.

Kuna msela pale sinza alikuwa na mkee chombo kweli kweli, yaani hatari na nusu, ngozi nyororo nyeupe, yupo kama nusu mwarabu nusu ethiopian, na shape kama masogange ila tall kama sepenga. jamaa alimtoa mkoani huko. Sasa siku jamaa akaswekwa rumanda pale sinza. kesi ilikuwa ndogo na ilipaswa aachiwe. Si mke akaenda kumwona mmewe post. Yaani jamaa alisota kituoni karibu mwezi, Askailiii wakawa wanajiria tu mzigo. mwishoe askaliii wakawapasia mzigo mabosi zao makao. Jamaa akawa anashangaa analetewa misosi ya maana na anapewa hadhi pale selo. Hatari sana.

Hatari zaidi ni mabosi. Bosi akiwa smart anamaliza ofisi nzima. Na kama bosi ana upenyo wa kugawa fursa au kupinya huyo ndio hatari zaidi. Kuna Halamashauri moja mjini ilikuwa na afisa elimu ambaye aliwala sana walimu. Ukifika ofisini kwake asubuhi unakuta list ya walimu waliojaaliwa zaidi ya 6 kila siku wanamsubiri. Jamaa aliwala walimu wengi kwa kiwango cha kutisha. Cha kushangaza baadhi yao ni wake wa watu wenye uwezo. Ukichunguza sababu ni kuwa alikuwa na uwezo wa kuwapa fursa ya kwenda projects za mitihani,sensa, na kusimamia uchaguzi. pia alikuwa ana uwezo wa kuwapeleka shule nzuri wazitakazo. kadhalika alikuwa anamfanya mwalimu asisumbuliwe na mkuu wa shule hata kama ana dosari.

Kuna Taasisi ina nafasi nyingi za kusafiri mikoani na nje ya nchi. Kupata kazi tu hapo ni shughuli pevu. Wanawake pale uanza kupata majaribu kuanzia interview na baada ya kuajiriwa. Wakipata kazi wale wenye TBS wote upewa safari za nje ya nchi mfululizo bila kuombwa mzigo. Mabinti hunogewa na hizo safari na kuanza kuwasifia Mabosi vibaya sana. Baada ya miezi mitatu safari zinakatishwa ghafla wanaanza kwenda wamama. Kinachofuata hapo ni kila binti kupambana kujipendekeza kwa mabosi. Baada ya miazi 6 unakuta Bosi kala mabinti wapya wote ishirini then anawapasia kwa mabosi wengine. Mabosi wakimalizana na mabinti huwapa uhamisho kwenda kwenye matawi. Katika mazingira hayo ni vigumu kwa mabinti wakiwemo wake na wachumba kuchomoa hata waambiwe kuwa wazee wana TANESCO.

Tusiwasimange sana wanawake majaribio wanayopitia ni magumu kuchomoa. wanawake wakiwemo lecturers wana mapito ya hatari na wanahifadhi siri. Njia ya kupunguza majaribu ni kumfanya mwanamke awe independent, kufanya matendo ya kumpunguzia stress, kumwezesha ipasavyo kimapenzi na kirasilimali na kumjali. Kuwa na mwanamke unayemmudu ambaye wewe ndio kichwa na anajiona salama zaidi kuongozwa nawe. Anza kuwekeza kwa mtoto wako wa kike ili kumwepusha na hilo gharika mbeleni.
 
Back
Top Bottom