Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi

Sitosahau yaliyonipata kijijini Kwamsisi

SEHEMU YA 5

Ilikuwa ni siku ya Ijumaa kama ilivyo ada niliamka asubuhi sana kwa msaada wa kengele ya simu yangu. Nilijiandaa tayari kwa ajili ya kuingia kazini, sikutaka kuchelewa kama ilivyokuwa siku iliyopita. Nilifika shuleni majira ya saa kuminambili na ushee nilikuwa mtu wa kwanza kufika pale shuleni, sikuwakuta watoto bado kulikuwa na kigiza cha asubuhi. Nilishangazwa na nilicho kikuta, mwalimu mkuu wa shule akiwa pamoja na walimu wengine wawili (jumla walikuwa walimu watatu) walikuwa wamelala katika kiwanja cha mstarini huku wakiwa wapo uchi wa mnyama mimi niliwashuhudia, isingekuwa mimi kuwahi basi huwenda wangeaibika sana mbele ya wanafunzi wote. Ni mimi na Sitti pekee ndio tuliosalimika, ijapo tulikuwa wageni lakini tulishakuwa makonkodi haswa wagumu kuingilika!

Niliwashtua walimu wenzangu waliokuwa wamelala huku wakiwa wamenyolewa kidogo kichwani. Wachawi walichukua kiasi kidogo cha nywele zao, walikurupuka na kushtuka sana walipoona kumbe wamelazwa kwenye mazingira yale ya shule wakaanza kutimua mbio kila mtu na njia yake, inaonekana ule msamaha tulioutoa jana haukutosha kumfanya mzee Samasimba kutusamehe kabisa. Maana kwa picha hii niliyoiona bila shaka yule mzee atakuwa anahusika kwa zaidi ya asilimia mia moja.

Baada ya muda wanafunzi wachache walikuwa wakiingia shuleni, baadhi ya wanafunzi ni watoto wa wachawi pia kwahiyo michezo yote waliyokuwa wakituchezea walikuwa wakiijua. Walikuwa wakishirikiana na wazazi wao kutuchezea michezo hiyo, japo nikiri kwamba tangu nilivyo ripoti katika shule hii sikuwahi kushuhudia sana watoto wakichapwa kwasababu ilikuwa ukimchapa mtoto wa mtu basi utaingia kwenye matatizo makubwa na jamii ya wazazi wao.

Kuna hadithi kwamba yupo mwalimu mmoja alikuwa akiwachapa sana wanafunzi hapo kwanza naye alikiona cha mtema kuni (alizinyonyoa nywele zake kisha akazila!) Baada ya tukio hilo fimbo kwa watoto imekuwa historia hapo shuleni, ijapo mimi hushika kwa lengo la kuwatishia tu. Wengi wetu tunakomaa na ule usemi wa ukinisikiliza usipo nisikiliza haunipunguzii mshahara wangu! Tulifanya kazi tu kutimiza wajibu.

Kwahiyo watoto wengine walijua kinacho endelea na walifika mapema ili kuhakikisha kama wale walimu bado wamelala pale ili wawaaibishe kwa kupiga kelele kuwaita wanafunzi wenzao, lakini haikuwa hivyo, walivyofika walinikuta mimi nikiwa nimefura kwa hasira. niliwahesabia namba na haraka haraka kila mwanafunzi alipewa eneo lake la kufanya usafi, ninauhakika kuwa leo lazima wapeleke ripoti kwa wazazi wao na hii inaweza kuongeza chuki dhidi yangu.

Wale walimu wenzangu walianza kuingia kazini mmoja mmoja na mpaka walipofika wote walikuwa wamechoka sana, ilionekana kama walifanyishwa shughuli kubwa jana yake, nyingi huwa ni za mashambani ama za kubebeshwa vitu vizito, na unafanya bila kujitambua unakuwa kama ndondocha kwa muda mfupi, wachawi wana mambo sana!! Tulianza kufundisha nakufikia saanne muda wa mapumziko tulisika ngoma ikipigwa kwa sauti dum dum dum...! Hii ni sauti ya hatari ni lazima ikitokea hivi kuna tukio kubwa limetokea, ngoma iliendelea kupigwa na mara kijana aliyetumwa kuja shuleni kutoka ofisi za kijiji alifika akiwa anahema sana.

Nimetumwa na mwenyekiti kwamba kunamsiba umetokea huko Mahameni! Mahameni ulikuwa ni mji wa zamani ambapo wanakijiji walihama enzi za vijiji vya ujamaa na kutengeneza kijiji cha Kwamsisi lakini walikuwepo baadhi ya watu waliokuwa wakiendelea kuishi huko. Mzee Kingalu amefariki kwa kuangukiwa na ukuta wa nyumba yake. "Unasema?!" niling'aka kwa mshtuko. "Ndio hivyo, kwahiyo mwalimu mkuu atume wawakilishi." Niliangua kilio cha kwikwi. "Haiwezekani nasema haiwezekani wamemuuwa mzee wetu." Nilikuwa na uchungu mkubwa, kati ya wazee wengi wa pale kijijini ni huyu tu ndiye niliyeelewana naye alikuwa mzee mpenda maendeleo alijitoa kunisaidia kwa hali na mali.

"Pole sana Soka, tunauelewa ukaribu wako na mzee Kingalu huna budi kuukaza moyo," walimu wenzangu walizidi kunipa moyo akiwemo Sitti aliyekuwa habanduki pembeni yangu. "Ninawapa ruhusa nyinyi wawili ili muende kutuwakilisha kwenye msiba huu," tulitoka tukiwa tunatembea haraka haraka kuelekea kitongoji cha Mahameni hapakuwa mbali kutoka eneo la shule, ni mwendo kama wa nusu saa kwa kutembea kwa miguu. Kijiji chote kilizizima, mzee Kingalu alikuwa ni moja ya wazee walioheshimika sana pale kijijini, ingawa alikuwa pia na uchawi wa kurithi, kwani uchawi ni kama mila kwenye jamii ya wazigua, alirithi mkoba huu kutoka kwa mababu zake.

Tulifika na hapo Sitti akaanza kuangusha kilio si unajua wanawake tena mimi nilijikaza kisabuni. Watu walikuwa ni wengi wakiimba nyimbo za maombolezo hata wale wachawi nilio waona jana usiku wakipanga mikakati dhidi yangu na mzee Kingalu nao niliwaona wakibubujikwa na machozi. Tuliingia moja kwa moja kwenye ile nyumba ya Msonge iliyokuwa na msiba. Niliingia ndani na kumkuta Wana-Kingalu (Mkewe) akiwa na huzuni nyingi nilimpa pole naye akanikumbatia kwa huzuni, alikuwa ni bibi mtu mzima. Niliingia chumbani kuutazama mwili wa mzee, "nyumba aliyoangukiwa na ukuta ndio ile pale alikuwa amejipumzisha kitandani." nilionyeshwa nyumba nyingine kwenye boma ya ukoo wake.

niliingia kwenda kuutazama mwili wa marehemu, walikuwa wamemlaza kwenye kitanda cha supatu (kamba za kusukwa na minyaa), mwili haukuwa na majeraha kabisa ingawa ulikuwa ukivuja damu puani na mdomoni na ulikuwa umevimba kiasi. Hapo nilishindwa kujizuia nikaangua kilio. "Mtetezi wangu sasa hayupo nitawezaje kuishi kwenye hichi kijiji kilichojaa vitimbi na mauzauza ya kila aina?!"

Walinichukua na kunisogeza pembeni nilimuona Sitti akiwa amekaa sehemu tofauti akijumuika na wanawake wenzake. Kinacho fuata ni mwili kuoshwa na kisha kuzikwa kwa taratibu zote za dini ya kiislamu. Usishangae mchawi kuzikwa kidini kwani hawa wachawi huwa wanajivika sura ya udini uliokubuhu na lengo kuu ni ili wasiweze kushtukiwa ama kuhisiwa kama ni watu wabaya. Mfano Mzee Masimba alikuwa ni mtu wa swala tano akiwa pia ni mmoja wa viongozi wa msikiti mkuu wa Kwamsisi.

ITAENDELEA...
(Usiache kutoa maoni.)
MUENDELEZO SEHEMU YA 6

cariha
 
Naona criticsm zimekuwa nyingi kwahiyo nitaishia hapa kwenye episode 6 ahsanteni wote kwa kufuatilia, niko naendelea kupambana na chaki.

Ndio maana tulikwambia usisome critics hakuna alieleta story yake jf akasifiwa na wote
Ukileta kitu we tiririka tu usisome maoni ya watu hadi umalize
 
Kumbe Upo.Kuna jamaa alianzisha Thread Kueleza Maisha Yake Ya Ujambazi,Tukashangaa Kimya Sijui Baada ya Kufika Episode ya 8 Nafkiri Sasa cjui Alienda kuiba wakampiga chuma

[emoji28][emoji28][emoji28]yule tuliishia alipata kazi ya tajiri kkoo sasa sijui ndio alienda mazima hajawahi kurudi tena
 
Nikisoma hivi hlf Mimi mwaka wa nne huu natafuta mchawi wa kunilogea watu sipati, nabakia kusema hiiiiiiiii
Halafu nahitimisha kuwa uchawi haupo.

[emoji1787][emoji1787][emoji1787]kwanini unataka uwaloge?unaanzisha vita utaiweza kweli?
 
Walimpiga kipaipai[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]Yaani mtu anakunuiza nenda Mwana kwenda kama upepo unavoenda afu anakupuliza huku ananuia "km maiti inarudi na yeye arudi kama hairudi basi asirudi tenaa"weeee...usiombe

Dah wewe una experience unajua kunuia[emoji28][emoji28][emoji28]
 
haya mambo kwa tanga ni ya kweli kabisa mm mwenyewe nilikuwa handeni kijiji cha ndelema ukikuta nyumba hawajui uchawi basi wana mganga wao anaowatibu
Me nikiandika mambo ya tanga kuhusu ushirikina naonekana mbaya wanatanga wanakuja juu nakujinasibu kuwa wenyewe ni wastaarabu, toka lini mshirikina au mchawi akawa mstaarabu
Nipo tanga kutwa nzima wapangaji wenzangu kwenda kwa waganga, kitu kidogo tu wameenda kwa mganga au kupiga simu kwa mganga. Principal yangu sitaki kushirikiana au kushare kitu nao ni mimi na familia yangu tu.

Mambo haya watu wengi wa bara yanatushinda
Dini ya mudi na ushirika vinaenda sambamba
ushirikina=uchawi=roho mbaya
 
"uttoh2002,
Yani kweli umekalisha kengele chini ukiamini hii ni story ya kweli?

Another chiiz in town.
 
Me nikiandika mambo ya tanga kuhusu ushirikina naonekana mbaya wanatanga wanakuja juu nakujinasibu kuwa wenyewe ni wastaarabu, toka lini mshirikina au mchawi akawa mstaarabu
Nipo tanga kutwa nzima wapangaji wenzangu kwenda kwa waganga, kitu kidogo tu wameenda kwa mganga au kupiga simu kwa mganga. Principal yangu sitaki kushirikiana au kushare kitu nao ni mimi na familia yangu tu.

Mambo haya watu wengi wa bara yanatushinda
Dini ya mudi na ushirika vinaenda sambamba
ushirikina=uchawi=roho mbaya
Umeanza vizuri, ila aya ya mwisho umepuyanga.
 
Umeanza vizuri, ila aya ya mwisho umepuyanga.
Hapana mkuu utakuta mtu swala 5 afu ni anaswalisha au anamiliki msikini ila ni mganga wakinyeji au watu wana mtuhumu kuwa ni mchawi
Kwa wakristo haiwezeka ila washirika washirikina wapo ila wanajificha sana
 
Back
Top Bottom