Wakuu, kama spika tuliye naye ndio huyu, basi hakuna bunge......!
Sitta amkataza Makinda kujadili BoT, Richmond
* Asema hayo ni mambo nyeti
* Asema yasubiri mpaka atakaporudi
* Anakwenda Marekani Jumatatu
* Lowassa awaomba radhi wabunge
Na Tausi Mbowe, Dodoma
SPIKA wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samwel Sitta amemtaka Naibu Spika, Anna Makinda kutokurupuka kuyazungumzia au kuyatolea maamuzi katika Bunge mambo yote �nyeti� wakati yeye hayupo.
Spika Sitta alitoa tahadahri hiyo wakati anamkabidhi kiti cha Spika kwa Naibu wake kwa muda wote akapo kuwa nchini Marekani kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi wiki ijayo.
�Mambo yote �nyeti� yatasubiri mpaka mimi mwenyewe nipo, Naibu Spika asije akakurupuka akaanza kuyavaa mambo makubwa wakati mimi sipo,� alisisitiza Sitta.
Sitta alitoa mfano wa mambo hayo nyeti kuwa ni pamoja na sakata la ufisadi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Richmond Spika amabyo alisema ili kujadili masuala hayo ni lazima mwenyewe awepo.
�
Haya ni masuala mazito yanayoigusa nchi, si masuala rahisi rahisi ni vizuri mimi mwenyewe nikawepo katika mjadala huo na si vyenginevyo, �alisema Spika Sitta.
Hatua hiyo ya Spika inakuja kufutia kupata safari ya nchini Marekani kwa shughuli za kikazo aliyosema ni muhimu kwa kuwa lengo lake ni kuliongezea uwezo Bunge.
�Napenda kuwatangazia na kuwaaga waheshimiwa wabunge kuwa naenda Marekani,
ingekuwa ni safari ya kitalii nisingeenda hasa katika kipindi hiki kizito ambapo wananchi wanataka kujua ukweli wa mambo katika masuala mazito yanayoihusu nchi
yetu, Alisema Sitta na kuongeza:
"Lakini safari hii ni ya kulijengea uwezo Bunge hivyo sina budi kwenda,
lakini namtahadharisha mheshimiwa Naibu Spika kuwa asije akakurupuka na kuvamia mambo nyeti, mambo yote �nyeti� yatasubiri mpaka nitakaporudi�.
Alifahamish kuwa atakuwa nchini Marekani hadi Alhmisi wiki ijayo na kwamba shughuli zote za Bunge anamwachia Naibu Spika, Anna Makinda mpaka atakaporudi.
Awali Spika huyo aliliambia Bunge kuwa bado mashauriano baina ya ofisi yake na serikali yanaendelea kuhusu ripoti ya ukaguzi wa mahesabu ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ili kupelekwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na wabunge.
�Mashauriano baina ya ofisi yangu na serikali bado yanendelea na suala hili nitalitolea majibu kwa kuzingatia haki, hivyo naomba wabunge muwe na subira,� alisisitiza Sitta.
Sitta alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Hamadi (CUF) kumbusha ahadi yake na kwa kuuuliza kama serikali ipo tayari kupeleka ripoti hiyo bungeni kwa ajili ya kujadiliwa.
Mapema wiki hii, Spika Sitta aliwaambia Wabunge kuwa ofisi yake iko kwenye mazungumzo na serikali kuhusu ripoti hiyo kupelekwa Bungeni kwajili ya kujadiliwa na kwamba jibu wangelipata katikati ya wiki hii baada ya wabunge hao kutaka ripoti yote iwasilishwe bungeni.
Mapema asubuhi Waziri Mkuu, Edward Lowassa aliwaomba radhi wabunge kwa kushindwa kutoa nyaraka muhimu kwa wabunge, ikiwemo ripoti za Richmond na ya EPA ili waweze kuzipitia kabla ya kujadiliwa kwa maelezo kwa hali hiyo ilisababishwa na sakata la BoT linaloendelea.
Waziri Mkuu alikuwa akitoa ufafanuzi baada ya kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamadi Rashidi kuomba muongozo wa Spika kutaka Wabunge wawe wanapatiwa nyaraka muhimu na kuzisoma kabla ya kuingia bungeni.
Akitoa ufafanuzi juu ya sula hilo Waziri Mkuu alisema kuwa kwa muda mrefu Gavana Mkuu wa BoT, alikuwa mgonjwa na kwamba kutokana na sakata linaloendelea katika benki hiyo mambo hayakaa vizuri,� alisema Waziri
Mkuu.
http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=4274