Sitta Azima Maswali BUNGENI: Richmond & BoT Zimsubiri Yeye Atoke Marekani!!

Sitta Azima Maswali BUNGENI: Richmond & BoT Zimsubiri Yeye Atoke Marekani!!

Kwa kweli Wadanganyika tumekwisha, ina maana Waheshimiwa Watukufu wabunge wetu wamekaa kimya kwa kauli hiyo ya Mzee Six? Nakumbuka zamani Babu yangu aliwahi kuniambia Umri sio Akili wala Busara, pia aliniambia sio lazima watu ambao wamesoma wewe na Busara. Ndio naamini kwa sasa kuwa Bwana Six amesoma lakini Busara hakuna. Huwezi kumwambia naibu wako mbele ya kadamnasi kama Bunge kuwa anatoa maamuzi ya kukurupuka. Kwa kweli this is terrible. Anatakiwa aombe Radhi kwa Makinda, Kwa Bunge na Kwa Watanzania wote. Anatakiwa kuniomba radhi kwani kwa kusema kuwa Naibu Spika hana uwezo maana yake wabunge waliomchagua hawafai, pia watanzania tuliowachagua hao wabunge na sisi hatuna maana
 
Tunapoteza lengo kumlaumu spika Sita. Ni mtindo wa CCM na serikali yake ndio adui mkubwa wa nchi hii sasa.
Sita yupo pale kulinda maslahi ya CCM na serikali yake. Ndio maana humsikii hata mbunge mmoja wa CCM akimlalamikia Sita kwa upuuzi kama huu. Anna Makinda, yaani hata huoni aibu kudharauliwa namna hiyo? Kwani u-naibu spika ni nini, si utaendelea kuwa mbunge? Hii ni dharau usiyoistahili.
 
Ni kweli Spika pamoja na wabunge wote wa CCM (Mama Makinda akiwa ni mmoja wao), wako pale kulinda maslahi ya CCM (mafisadi wakiwamo). Lengo kubwa kwa sasa ni kuondoa uozo (uvundo) uliojaa ndani ya serikali ya CCM hivyo vilio na kelele zielekezwe moja kwa moja kwa wale wanaokubali kwa njia moja ama nyingine kukumbatia ama kubeba uozo huo kwa faida yao binafsi na kwa faida ya wengine. Hata wakitia pamba masikioni tusikate tamaa tuendelee kuwapigia kelele mpaka ifikie mahali waone aibu kwa mambo machafu wanayolifanyia Taifa letu. Haiwezekani Spika wa Bunge alione bunge kama Taasisi yake binafsi amabayo anaweza kuindesha kwa jinsi atakavyo mwenyewe. Naomba waungwana tusichoke tuendelee kupiga kelele na kuzomea popote pale awapo ama aonekanapo, Wabunge pia lioneni hilo na mlihoji kwa nguvu zote. Mama Makinda ukikaa kimya tutaomba TUSI ulilotukanwa na Mh. mwenzio SITTA lifikishwe kwa wale waliokupigia kura ili waone kama ni halali kwao kuendelea kuwa na mwakilishi anayekurupuka katika utendaji wake.
 
Nchi hii vituko haviishi ...samuel sitta akijua kuwa hoja ya richmond ipo moto ..kapewa safari ya geresha kwenda marekani..ili kukwepa kujadili hoja ya richmond na BOT..

nasema uzalendo upo wapi..,kama anajua taifa linamuhitaji kwa hoja hizi nyeti kwa nini akiaamua kchagua kusafiri kwenda marekani...huu nauita ni usanii...na usaliti.

nchi itaendelea kuendeshwa kisanii hadi lini???
 
kwani bila yeye hoja haiwezi kujadiliwa?. Ina maana akiumwa ndiyo hakuna kikao cha bunge?. speaker wa bunge ana msaidizi na katibu, kama hayupo bado mambo yanaendelea kama kawaida hapo bungeni.
 
Nafikiri katumwa kumuona Balali akubali kubeba mizigo ya BOT, asilipue mabomu.Ya EPA, ALex Stewart etc
 
Its simple, kama akaona hoja zinazo kuja ni nyeti mno na hawezi Anna Makinda hawezi kuzi-handle afanye uamuzi rahisi, badala ya yeye kwenda Marekani amtume Makinda na yeye "superman" a deal na hizo hoja nyeti.

Naona mzee anajikuta ktk njia panda, trip anaitaka at the same time kufukia mashomi kwa mtindo wa "busara zangu" pia anakutaka!

U cant have ur cake and eat it
 
Mzee Samuel Sita, you must be kidding us......

Nimesoma ktk vyombo vya habari kwamba Spika wa bunge, Mzee wa Speed and Standard ameamrisha hoja zile 'sensitive' zisijadiliwe mpaka pale yeye atakaporudi toka US. Is this a joke or what???

Toka lini taasisi ya bunge ikawa ni mali ya mtu mmoja i.e Speaker, na vipi yeye ana mamlaka ya kusimamisha kwa hoja hizo kujadiliwa kwani hana msaidizi/wasaidizi?..., this can only happen in Tz, nilidhani alipotoka Msekwa ambaye tayari alishaona bunge ni kama mali yake mambo yangebadilika, kumbe mambo yamekuwa mabaya zaidi.....

Je, Mh. Sita anao uhakika asilimia 100 kwamba atarudi 'salama' buheri wa afya, je ameandikiana mkataba na Mungu, vipi mathalani akitokea kupatwa na mauti, au ugonjwa mkubwa(japo simuombei hayo)ina maana hoja hizo hazitajadiliwa milele..mpaka afufuke toka kuzimu au apone.

It is time for our leaders to think before they say, and not otherwise.

I am tempted to say that, most of our leaders; say or act on things and then they think afterwards.

Viongozi kumbukeni mmebeba dhima kubwa ya kuwaongoza watu, ahadi ambayo mmeichukua kwa kuapa wengine kwa mishafu na biblia. Tangulizeni maslahi ya Taifa mbele na si vinginevyo.

Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania.
 
Wakuu, kama spika tuliye naye ndio huyu, basi hakuna bunge......!



Sitta amkataza Makinda kujadili BoT, Richmond

* Asema hayo ni mambo nyeti

* Asema yasubiri mpaka atakaporudi

* Anakwenda Marekani Jumatatu

* Lowassa awaomba radhi wabunge



Na Tausi Mbowe, Dodoma


SPIKA wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samwel Sitta amemtaka Naibu Spika, Anna Makinda kutokurupuka kuyazungumzia au kuyatolea maamuzi katika Bunge mambo yote �nyeti� wakati yeye hayupo.


Spika Sitta alitoa tahadahri hiyo wakati anamkabidhi kiti cha Spika kwa Naibu wake kwa muda wote akapo kuwa nchini Marekani kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi wiki ijayo.


�Mambo yote �nyeti� yatasubiri mpaka mimi mwenyewe nipo, Naibu Spika asije akakurupuka akaanza kuyavaa mambo makubwa wakati mimi sipo,� alisisitiza Sitta.


Sitta alitoa mfano wa mambo hayo nyeti kuwa ni pamoja na sakata la ufisadi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Richmond Spika amabyo alisema ili kujadili masuala hayo ni lazima mwenyewe awepo.


�Haya ni masuala mazito yanayoigusa nchi, si masuala rahisi rahisi ni vizuri mimi mwenyewe nikawepo katika mjadala huo na si vyenginevyo, �alisema Spika Sitta.


Hatua hiyo ya Spika inakuja kufutia kupata safari ya nchini Marekani kwa shughuli za kikazo aliyosema ni muhimu kwa kuwa lengo lake ni kuliongezea uwezo Bunge.


�Napenda kuwatangazia na kuwaaga waheshimiwa wabunge kuwa naenda Marekani, ingekuwa ni safari ya kitalii nisingeenda hasa katika kipindi hiki kizito ambapo wananchi wanataka kujua ukweli wa mambo katika masuala mazito yanayoihusu nchi
yetu, Alisema Sitta na kuongeza:


"Lakini safari hii ni ya kulijengea uwezo Bunge hivyo sina budi kwenda, lakini namtahadharisha mheshimiwa Naibu Spika kuwa asije akakurupuka na kuvamia mambo nyeti, mambo yote �nyeti� yatasubiri mpaka nitakaporudi�.

Alifahamish kuwa atakuwa nchini Marekani hadi Alhmisi wiki ijayo na kwamba shughuli zote za Bunge anamwachia Naibu Spika, Anna Makinda mpaka atakaporudi.


Awali Spika huyo aliliambia Bunge kuwa bado mashauriano baina ya ofisi yake na serikali yanaendelea kuhusu ripoti ya ukaguzi wa mahesabu ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ili kupelekwa bungeni kwa ajili ya kujadiliwa na wabunge.


�Mashauriano baina ya ofisi yangu na serikali bado yanendelea na suala hili nitalitolea majibu kwa kuzingatia haki, hivyo naomba wabunge muwe na subira,� alisisitiza Sitta.


Sitta alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Hamadi (CUF) kumbusha ahadi yake na kwa kuuuliza kama serikali ipo tayari kupeleka ripoti hiyo bungeni kwa ajili ya kujadiliwa.


Mapema wiki hii, Spika Sitta aliwaambia Wabunge kuwa ofisi yake iko kwenye mazungumzo na serikali kuhusu ripoti hiyo kupelekwa Bungeni kwajili ya kujadiliwa na kwamba jibu wangelipata katikati ya wiki hii baada ya wabunge hao kutaka ripoti yote iwasilishwe bungeni.


Mapema asubuhi Waziri Mkuu, Edward Lowassa aliwaomba radhi wabunge kwa kushindwa kutoa nyaraka muhimu kwa wabunge, ikiwemo ripoti za Richmond na ya EPA ili waweze kuzipitia kabla ya kujadiliwa kwa maelezo kwa hali hiyo ilisababishwa na sakata la BoT linaloendelea.


Waziri Mkuu alikuwa akitoa ufafanuzi baada ya kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamadi Rashidi kuomba muongozo wa Spika kutaka Wabunge wawe wanapatiwa nyaraka muhimu na kuzisoma kabla ya kuingia bungeni.


Akitoa ufafanuzi juu ya sula hilo Waziri Mkuu alisema kuwa kwa muda mrefu Gavana Mkuu wa BoT, alikuwa mgonjwa na kwamba kutokana na sakata linaloendelea katika benki hiyo mambo hayakaa vizuri,� alisema Waziri

Mkuu.http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=4274
 
Mafisadi wana namna yao ya kufanya mambo . Nilibaki na bado nimeshangaa kwa tangazo lile . Sitta hawezi kumuona Ballali kwa uhakika na siamini kwamba Ballali anaweza kumuona Sitta .Ni wale wale .Kwanza anakaa US siku 4 hazitoshi kumuona Ballali maana sasa Ballali ni zaidi ya JK kumuona lazima upitie vituo kadhaa labla hujamuona na uwe na shida yako maalumu ielekwe nje kabla hujatinga ndani . Nadhani kuna kitu so serious maana jinsi Bunge linavyo endeshwa kunaonyesha usiri sana.
 
Quote:
Mapema asubuhi Waziri Mkuu, Edward Lowassa aliwaomba radhi wabunge kwa kushindwa kutoa nyaraka muhimu kwa wabunge, ikiwemo ripoti za Richmond na ya EPA ili waweze kuzipitia kabla ya kujadiliwa kwa maelezo kwa hali hiyo ilisababishwa na sakata la BoT linaloendelea.


Waziri Mkuu alikuwa akitoa ufafanuzi baada ya kiongozi wa Upinzani Bungeni, Hamadi Rashidi kuomba muongozo wa Spika kutaka Wabunge wawe wanapatiwa nyaraka muhimu na kuzisoma kabla ya kuingia bungeni.


Akitoa ufafanuzi juu ya sula hilo Waziri Mkuu alisema kuwa kwa muda mrefu Gavana Mkuu wa BoT, alikuwa mgonjwa na kwamba kutokana na sakata linaloendelea katika benki hiyo mambo hayakaa vizuri,� alisema Waziri

Mkuu.http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=4274

Wakuu, kwa aliyeelewa manvi alimaanisha nini kwa maelezo haya atufafanulie kwani wengine tumetoka patupu
 
What the *&%$!!!!

Only in TZ would people accept this.
 
Sasa huko bungeni wafanye nini kama siyo kujadili masuala yanayoigusa nchi, wacheze karata au ngoma za kienyeji mpaka arudi au? Hapo kawatukana Naibu Spika na wabunge wote.

Halafu kumbe Naibu Spika Mheshimiwa Anna Makinda ana sifa ya kukurupuka mpaka imebidi Spika amtahadharishe? Makubwa!

Tuendelee kujivunia "amani na utulivu".
 
Na bado watu wengi tu wanaendelea kuiaminin serikali ya kisanii namna hii!!!!! Hv hii ni laana nini???????
 
Hivi huyu Sitta mbona anawafanya watz wajinga sana jamani?

Hivi mambo haya yataendelea hivi mpaka lini?

Jamani naombeni kuuliza sasa kazi ya naibu spika ni ya nini, kwa maeleza ya huyu myeyushaji Sitta, nadhani ni dhairi anatueleza kuwa hiki cheo hakina kazi ile ni njia nzuri yake yeye na ya wa aina hii kuendelea kula hela zetu

RUDISHENI HELA ZETU
 
Huu ni ushenzi usio na kifani... kweli nataka kuamini watz wote ni wafu
 
Tuandamane Mkuu wangu ee naona unataka kutuvurugia "amani na utulivu" tulionao, chonde chonde
 

KIKWETE...

BORA WANACHAMA WACHAFU NA WACHACHE WACHACHE WACHAFUKE KULIKO CHAMA KIZIMA KICHAFUKE

CHUKUA HIYOOO.....
 
Back
Top Bottom