Sitta: Nitagombea Uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba kwa sababu naamini kuwa nina sifa za kutosha

Sitta: Nitagombea Uenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba kwa sababu naamini kuwa nina sifa za kutosha

Sasa si bora kukawa na bunge kivuli la katiba manake kukawa na spika kivuli ili watu waridhike, wabongo bana mtu anasimamia misimamo yake wakati hata sio mpiga kura wa kuchagua spika.

Kwani sie ambao sio wajumbe wa bunge la katiba tukiwaachia waliokuwa bungeni tutakufa, mbona tunajihusisha hata na visivyotuhusu. Sita kama sifa anazo akajiuze kwa wapiga kura wake ili wamchague kuuza sura katika media ndio kampeni zenyewe sasa wakati hata kanuni bado.
 
Bunge la katiba halifuati matakwa ya vyama, kama anakidhi sifa za kugombania uenyekiti atagombania tuu mtake msitake..!! Msitake kuhodhi mchakato huu wa kutengeneza katiba mpya! Patachimbika bila jembe wala sururu mnatuchosha
 
mods tuwekee hapa kisanduku cha maoni kati ya sita,chenge na chikawe tuone nani mwenye kukubalika kwa watanzania asimamie mchakato wa kupata katiba mpya
 
Namuunga mkono Sitta kugombea na hata kuwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba. Hata hivyo, kwa Chama cha CCM ni ndoto za mchana kwa Sitta kupitishwa kugombea hiyo nafasi.

Hamna hiyo kitu ya kupitishwa na chama ni uamuzi wa mtu binafsi kugombania au kutokugombania unachotakiwa ni kuwa na sifa tuu
 
Hili suala la Mwenyekiti wa Bunge la Katiba ni vyema vyama vikakaa kando ili Wajumbe wa Bunge Maalum wajichague wao wenyewe....

Nyerere alishawahi kunukuliwa akisema; "Muda wa kuchagua viongozi wetu kwa mizengwe umepita". Lazima busara na haki itumike kupata viongozi waliobora..
 
Simuungi mkona Sitta hadi nijue ana msimamo wa serikali ngapi.. Mbili, tatu au moja. Msimamo wangu ni serikali moja
 
Wakuu hili ni jambo ambalo ni vizuri kwa ma great thinkers mkaisaidia jamii.Sita ni ccm na isitoshe anauzoefu mkubwa tu na labda angefaa kuwa spika wa kututengenezea katiba.Sasa wao na sikia wanataka Chenge na wala sikumbuki kama aliwahi kuongoza mihadhara yoyote mikubwa.Kuna nini hapa?
 
Watanzania, nchi hii ni ya ajabu. Chenge kwa usafi upi,uadilifu upi (moral authority) alio nao kugombea nafasi inayohitaji uadilifu wa hali ya juu kama hii ya mwenyekiti wa Bunge la katiba. Kweli nchi hii imelaaniwa! CCM bila aibu mnampendekeza Chenge!
 
Watanzania, nchi hii ni ya ajabu. Chenge kwa usafi upi,uadilifu upi (moral authority) alio nao kugombea nafasi inayohitaji uadilifu wa hali ya juu kama hii ya mwenyekiti wa Bunge la katiba. Kweli nchi hii imelaaniwa! CCM bila aibu mnampendekeza Chenge!

Ni masikitiko tu, hata huyo Sitta pia ukktafakari kwa kina huwezi kukubali kwa haraka haraka, Hapo ni kuangalia ni nani ana afadhali kidogo. Maana hivi ni nani safi CCM? Yaani ambaye jina lake likitajwa kila mtu anakubali kwamba amaa kweli huyo ni safi?

 
Sina hakika kama mafisadi watamkubalia!!!!! I think he is the right candidate!!!
 
huyo nijembe.We ukiona mtu mafisadi hawampendi,huyo ujue anafaa.Sikuzile walimtoa kwenye usipika ccm wakatubambika huyo mama Mbena.Ona sasa alivyo haribu!
 
Mbona hueleweki Au umekunywa viroba vyenu!!
 
huyo nijembe.We ukiona mtu mafisadi hawampendi,huyo ujue anafaa.Sikuzile walimtoa kwenye usipika ccm wakatubambika huyo mama Mbena.Ona sasa alivyo haribu!

Mbona hata haueleweki,ninini?
 
Sitta anaunga mkono muungano wa serikali tatu lakini anapinga muungano utakaozaa marais watatu. Spika wa aina hii atafaa sana kwani kwa mtazamo huu atakuwa fairly balanced;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom