Sitta: Nyaraka zinazosomwa makanisani ni za kipuuzi

Sitta: Nyaraka zinazosomwa makanisani ni za kipuuzi

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Mwenyekiti wa Bunge la Katiba,Samweli Sitta,bila haya wala kumungunya maneno,amethubutu kusema baadhi nyaraka zinazosomwa makanisani ni upuuzi kabisa.

Akiwakaribisha wageni ambao ni waumini wa makanisa bwana(sidhani kama anafaa kuitwa mheshimiwa) Sitta amesema na hapa namnukuu "muwe waangalifu huko makanisani kwani baadhi nyaraka zinazosomwa huko ni za kipuuzi".Huenda sijanukuu maneno yote kwa usahihi ila kikubwa amesema nyaraka hizo ni za kipuuzi!

Wadau,nafikiri wote mnankumbuka waraka wa jumuiya ya kikiristo Tanzania(CCT) uliokuwa unasomwa makanisani na waraka huo ulikuwa unapinga kuendelea kwa bunge hilo.

Sasa mdau tafakari mwenyewe mzee Sitta alikuwa anaongelea nyaraka gani na utapata jibu alafu jiulize mwenyewe athari ya kaulu kama hiyo kwa mchakato huu na Taifa kwa ujumla.

Alafu,hivi kila mwenye kuvaa suti na kuwa na mnvi anastahili kuwa kiongozi?

Mods,naomba msiunganishe huu uzi ila watu waelewe na waone alichosema.Mods nawasihi hii kauli isimame peke yake.
 
Huyu mnyamwezi mwenzangu kapoteza direction ya hii nchi na hata ya kwake mwenyewe. Halafu anataka kuwa head of state wa hii nchi,you just lost it my home boy
 
Kuna haja Rais ajaye, aje awachukue watu kadhaa na kuwapeleka kwenye Mahakama ya Kijeshi.

Tafadhali, hapo sijaandika nani aende..............
 
Mod please usifikirie hata kuunganisha hii.

Kweli dunia imeisha, sitta mwenyekiti wa bunge la katiba lililokosa uhalali kutokana na kutekwa na chama cha mapinduzi ni ulimi umekuteleza au shetani kakuingia mpk ukaamua kusema nyaraka zinazo somwa makanisani kuhusu mchakato wa katiba mpya ni upuuzi mtupu hazina utukufu.

Sitta Samuel uliteuliwa na nani hapa duniani kupima waraka wa viongozi wetu wa dini kua zina utukufu au la !!!!?

je viongozi wetu wa dini hawana mamlaka wa kukemea uovu unaoendelea dodoma??

nijibu sitta.
 
Mod please usifikirie hata kuunganisha hii.

Kweli dunia imeisha, sitta mwenyekiti wa bunge la katiba lililokosa uhalali kutokana na kutekwa na chama cha mapinduzi ni ulimi umekuteleza au shetani kakuingia mpk ukaamua kusema nyaraka zinazo somwa makanisani ni upuuzi mtupu hazina utukufu.

Sitta Samuel uliteuliwa na nani hapa duniani kupima waraka wa viongozi wetu wa dini kua zina utukufu au la !!!!?

Six anazidi kupoteza...
 
'hujafa hujaumbiaka' ...alikuwa ameshaonekana kama icon muhimu kwa maisha ya Watanzania, tangia Tabora School, UDSM mpaka Spika na hata watu hawakushtuka sana pale alipoanza kutoka kwenye mstari kwa kujenga ofisi ya spika jimboni kwake. Hakika Mungu ana njia nyingi za kuonyesha rangi halisi za waja wake!
 
Viongozi wa dini watoe taarifa ya kulaani kauli yake,na aombe radhi,amevimbiwa karanga na asali, anapumua tu
 
Mod please usifikirie hata kuunganisha hii.

Kweli dunia imeisha, sitta mwenyekiti wa bunge la katiba lililokosa uhalali kutokana na kutekwa na chama cha mapinduzi ni ulimi umekuteleza au shetani kakuingia mpk ukaamua kusema nyaraka zinazo somwa makanisani kuhusu mchakato wa katiba mpya ni upuuzi mtupu hazina utukufu.

Sitta Samuel uliteuliwa na nani hapa duniani kupima waraka wa viongozi wetu wa dini kua zina utukufu au la !!!!?

je viongozi wetu wa dini hawana mamlaka wa kukemea uovu unaoendelea dodoma??

nijibu sitta.

Anatangaza vita asiyoijua,angejua watu walivyo na utii kwenye mambo ya Imani asingesema hivyo.
 
Mpuu.i sana anataka tumsikilize yeye kwasababu anakwapua 150 m za vikao visivyokuwa na tija.
 
Mpuu.i sana anataka tumsikilize yeye kwasababu anakwapua 150 m za vikao visivyokuwa na tija.
Mkuu, Sitta amepoteza direction. Anatakiwa kuongoza vikao vya BMK sio kuongoza viongozi wa dini.
Hapo anakosea.....tena sana, sasa watu ndio wanamjua kwamba ni mpuuzi kama wapuuzi wengine wa Fisiem.
 
Usiwe na hofu ndugu linalotokea kwa sasa ndani ya ccm ni kama vile wale watu walioujenga mnara wa babeli baada ya Mungu kuona wanafanya sivyo akaamua kuwagonganisha lugha ili wasielewane ndivyo ilivyo ndani ya ccm Mungu anatuonyesha njia waja wake waache waendelee kutubeza tu 2015 october siyo mbali.

Ndugu yangu unamaneno yaukweli hawa jamaa IPO mda watakuwa hawaongei lugha moja
 
Mpuuzi ni yeye lakini siyo viongozi wetu wa kidini waliotuandalia huo walaka
 
Back
Top Bottom