Elections 2010 Sitta: Wananchi msidanganyike

Elections 2010 Sitta: Wananchi msidanganyike

Yaani Slaa anasema kwa uwezo wa hali ya juu. Tunamshukuru Mungu kwa kutupa kiongozi wa hali ya juu kiasi hiki.

Sikuwa naelewa kwamba Sitta kajenga Ofisi ya Spika KWAO. Sasa, kama anavyouliza Slaa, utatumiaje shilingi milioni 500, pamoja na shilingi nyingine milioni 155 za fenicha, kujenga ofisi ya Spika kwenu kama kwamba wewe utakuwa Spika milele? Angejenga Ofisi Ya Mbunge kingeeleweka.

.
Naona Slaa hakutaja fedha anazotumia Sitta kwa ajili ya pango (wakati nyumba ya serikali ya Spika ilikuwepo). Amemhurumia.

Tunawaombeni CHADEMA mzidishe ulinzi wa Slaa. Hili la watu kusukuma gari lake linaniogopesha. Mtajuaje ni wazuri wote?

Mwezi mmoja kabla ya kuvunja bunge, Sitta alifanya ziara uturuki kwa wiki mbili. Hii ilikuwa ni mkakati wa kukusanya allowance kabla ya kuondoka. Hakukuwa na sababu ya yeye kwenda ziara hiyo kwakujua kuwa hatakuwa spika kwa namna yoyote. CCM hawamtaki na wananchi wamegundua kuwa akitishiwa posho mbili anafyata. Huyu mzee haeleweki. Nawapenda sana Selelii, Mpendazoe, Kimaro kwasababu wanasimamia kile wanachoamini ni kweli hata kama kufanya hivyo ni kwa gharama zao. Mr 6 ni ndumila kuwili, jemedari anyeweza kuuza kikosi cha askari ilimradi awe salama.
Ni kweli ofisi yake imegharimu sh 500 million, Nyumba 10 million kwa mwezi, mshahara lol sisemi, halafu anasema elimu bure haiwezekani. Ni huyu huyu mzee ana kashafa ya kughushi vyeti vya dawa,sijui imeishia wapi.
JK atuonyeshe risiti moja aliyowahi kulipia ada,toka chekechea hadi chuo kikuu ili tujue elimu bure haiwezekani. risiti moja tu!
Sitta atuonyeshe nyumba moja tu ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi yenye thamani sawa na choo cha ofisi yake ya sh 500 million
 
Dk. Slaa awakaanga Kikwete, Spika Sitta
• Asema Sitta si saizi yake, asijitafutie umaarufu asiostahili


MGOMBEA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amewarushia kombora Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mgombea urais wa chama hicho, Jakaya Kikwete na aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, kuwa ni wabadhirifu na wapenda anasa, ndiyo maana hawaamini kama elimu inaweza kutolewa bure.
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana mjini Arusha alipokuwa akizungumza kwenye mikutano yake ya kampeni, ambapo alisema kuwa nchi ina fedha nyingi lakini kwa sababu ya ubadhirifu wa viongozi ambao wanapenda anasa, fedha hizo zimekuwa zikitumika kwa manufaa ya wachache.
Alisema Rais Kikwete na Sitta, kamwe hawawezi kuelewa au kuikubali sera ya elimu ya bure inayonadiwa na CHADEMA kwa sababu wamezoea kuzitafuna rasilimali za umma huku wakiwaacha wananchi wakiishi maisha ya tabu.
“Hawa viongozi (Sitta na Kikwete) ni wabadhirifu, mioyo yao imejaa mambo ya anasa, ndiyo maana wanaposikia CHADEMA tunaweza kutoa elimu bure wanashangaa na kukataa kuwa hatuwezi kutekeleza, sisi tutaitoa elimu bure, kwa sababu tunajali masilahi ya walio wengi,” alisema.
Dk. Slaa alitumia nafasi hiyo kupuuza ombi la Sitta ambaye alitaka mdahalo naye kujadili sera ya kutoa elimu bure, ambapo alisema spika huyo aliyemaliza muda wake si saizi yake, bali anafaa kupambanishwa na mgombea ubunge wa CHADEMA katika Jimbo la Urambo Mashariki, Msafiri Mtemelewa.
Hoja hizo za Dk. Slaa zimetokana na Rais Kikwete kumtaka aachane na sera ya kutoa elimu bure, kwa sababu ni jambo lisilowezekana na hata kama analisema hivi sasa ni katika lengo la kutafuta kura za wananchi.
Kauli hiyo ya Kikwete ilishabihishwa na Spika Sitta, ambaye alisema kuwa sera hiyo haitekelezeki na kama Dk. Slaa anabisha uitishwe mdahalo baina yao wawili wajadili hoja hiyo.
Dk. Slaa alisema serikali yake itatoa elimu bure kwa watoto wote wa Tanzania, kutoka chekechea hadi kidato cha sita, kwa sababu anajua fedha za kufanya hivyo zipo, isipokuwa zinatapanywa na viongozi wasiojali masilahi ya umma.
Alitoa mfano wa matumizi mabaya ya fedha za umma yaliyofanywa na Sitta akiwa spika, akasema wakati gharama ya ujenzi wa ofisi ya mbunge ni kati ya sh milioni 40 na 50, Sitta alitumia sh milioni 500 kujenga jengo la ofisi ya spika katika Jimbo la Urambo, kana kwamba kuna vikao vya Bunge vinavyofanyikia Urambo.
“Utadhani Sitta anajiandaa kuwa spika wa maisha. Huu si ubadhirifu wa fedha za umma. Nimefanya hesabu, kiasi hicho cha pesa kinatosha kujenga zahanati 10 zilizokamilika na kinaweza kujenga madarasa 71 yaliyokamilika,” alisema Dk. Slaa.
“Sitoi takwimu hizo kwa kubahatisha ndugu zangu … ninazo nyaraka ambazo zinaonyesha namna fedha hizi zilivyotumika, kampuni zilizopewa tenda za ujenzi huo, sasa kama Sitta atasema ninasema uongo anijibu,” alisema Dk. Slaa.
Alisema serikali ya Kikwete imekuwa ya anasa, kiasi cha kutenga bajeti ya sh bilioni 30 kwa ajili ya chai na vitafunio, pesa ambazo zingeweza kutumika kwenye masuala ya maendeleo.
“Kama hakuna pesa, mbona wanajitengea sh bilioni 30 kwa ajili ya chai. Si wangezielekeza kwenye elimu na afya? Hawafanyi hivyo kwa sababu wanajua hawatafanya ubadhirifu wala kuendelea na maisha yao ya anasa,” alisema.
Alisema kwa kuonyesha kuwa viongozi wetu ni wafujaji wa rasilimali za taifa, Rais Kikwete alikodi ndege mbili kwenda Urambo kufungua jengo la spika ambalo liligharimu mamilioni ya fedha za walipa kodi.
Alibainisha kuwa samani (fenicha) zilizowekwa katika jengo hilo zina thamani ya sh milioni 155, kiasi ambacho ni kikubwa mno, na kwamba hizo ni katika ofisi moja tu ya spika, bado ofisi nyingine za umma ambazo kila kukicha zimekuwa zikisifika kwa kununua samani za bei ghali.
Alisisitiza kuwa kama fedha hizo zingeokolewa na kutumika katika huduma, zingeweza kutumika kulipia huduma nyingine za kijamii.
Dk. Slaa aliwasisitizia wakazi wa Arusha kuwa elimu bure na afya bure ni mambo yanayowezekana, na CHADEMA imeamua kutoa vipaumbele kwa sekta hizo, kwa sababu zinagusa moja kwa moja masilahi ya wananchi wengi.
Aliongeza kuwa Sitta na Kikwete hawapaswi kuzungumza kuwa kutoa elimu bure haiwezekani, kwa sababu wao walipata elimu bure wakati wa utawala wa Baba wa Taifa, Julius Nyerere, lakini wanasahau jambo hilo na kuwa kikwazo cha kutoa elimu hiyo.
Alibainisha kuwa kwa serikali makini yenye kujali masilahi ya wananchi ambao ndio walipa kodi, ni jambo la lazima kuangalia matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi badala ya kutafuta sababu za kushindwa kutimiza wajibu.
“Nataka nimwite Sitta kuwa ni mnafiki wa wazi, kwa kuwa anatumia fedha ya wananchi bila huruma, wakati yeye mwenyewe pamoja na wanaodai kuwa elimu bure haitawezekana walisoma katika serikali ya CCM wakati huo ikiongozwa na Mwalimu Nyerere bure,” alisema.
Dk. Slaa alipata mapokezi makubwa wakati anaelekea uwanja wa Mbauda, ambapo alilakiwa na wananchi walioacha kazi zao na kuzuia msafara wake, wakaandamana kumsindikiza hadi uwanjani hapo kwa kulisukuma gari lake.
Katika mkutano wa jioni uliofanyika katika viwanja vya Kimandolu - Tindigani, maelfu ya wananchi yaliandamana kumsindikiza uwanjani, huku akiwa anasindikizwa na magari, pikipiki na watembea kwa miguu chini ya ulinzi wa polisi.
Dk. Slaa pia alisema mishahara minonno ya wabunge inachangia umaskini wa Watanzania, ambapo alitoa mfano wa posho na mshahara wa mbunge mmoja anavyolipwa katika vikao vyake kwa mwaka ni sawa na mishahara ya miaka 50 ya askari polisi au mishahara ya miaka 70 ya hakimu wa Mahakama ya Mwanzo.
“Mimi naona mgombea mwenzangu wa CCM - Kikwete hana sababu ya kuendelea kuzunguka, kwa kuwa ahadi ambazo anazisema kwa wananchi hajawahi kuzitekeleza hata moja.
“Wakati nazindua kampeni zangu Jangwani, nilizungumza kuhusu fedha zilizochotwa na CCM katika mfuko wa matumizi ya kawaida (Other Charges) kwa ajili ya kufanyia kampeni zirudishwe, vinginevyo suala hili nitalilipua …lakini nashukuru kwamba agizo langu limetekelezwa, kwani fedha zote zimerejeshwa hata kabla sijaingia Ikulu,” alisema.


source Tanzania daima


Hii imekaa vizuri sana wadau

Dk. Slaa pia alisema mishahara minonno ya wabunge inachangia umaskini wa Watanzania, ambapo alitoa mfano wa posho na mshahara wa mbunge mmoja anavyolipwa katika vikao vyake kwa mwaka ni sawa na mishahara ya miaka 50 ya askari polisi au mishahara ya miaka 70 ya hakimu wa Mahakama ya Mwanzo.
 
Bweza paul.jpg

Mjifariji zaidi
 
Majmbazi CCm yanashirikiana na idara za serikali kukausha hazina ya nchi.
Kwa ccm haiwezekani elimu ya bure kwa kuwa washazoea vya kunyonga
kwa ccm suala la maendeleo watakwambia ni mchakato wakati kuna waliokuwa nyuma yetu wametupita sasa (mf. Botswana)
kwa ccm USHINDI ni LAZIMA kwa kuwa hawana hulka ya uchaguzi huru na haki
Kwa ccm kumtoa mtu roho si jambo gumu ili kulinda maslahi ya CHAMA cha MAZEZETA
 
Alafu ilo la nyumba ya speaker ata aliingii akilini ivi mfano akija speaker mwingine ataitumia iyo ofisi let us say speaker ni mbunge wa jimbo la iringa mjini.
None sense kabsaaaaaaaaaaaaaa,au walikuwa wanampoza Speaker asikomae na mafisadi
 
sasa hivi tena mkitoa kura kwa ccmakamba hakuna kulaumiana mra ooo foleni, mara oo hospitali , mara oo ada ya mwanangu , mara oo sijui nini . Angalieni wenyewe mabo yamewekwa hadharani. -kweli sitta ni manafiki mkubwa
 
@ CCM, Hiyo elimu ya bure na huduma zingine zinaweza kuwa afforded at small price au bure ikiwa MTAACHA KUWAPA WAGENI na MAFISADI rasilimali zetu kwa bei mbuzi.
 
Kumbe Sitta ni mtu anaeabudu anasa eeh! Ni namna ya watu wanaolia kwenye msiba huku moyoni mwao wakisema afadhali hata ametupisha eeh?
Sasa spika na serikali yake ya ccm kuna mantiki gani ya kumjengea mtu mmoja ofisi ya gharama ya milioni 500 huku wananchi ambao kimsingi ndio wamewaajiri kusimamia mapato yao wakiwa hawana shule, madawati, maji safi nk?
Nafsi yako ee Sitta umeithaminisha juu ya nafsi za maelfu ya wana urambo ulieamua kujenga hekalu la kukuburudisha katikati ya nyumba za msonge za raia zako. Ni afadhali Lowasa anayejulikana wazi kuwa fisadi achukue usipika kuliko wewe uliyevaa ngozi ya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu mkali.
Sasa hata hivyo swali linabaki ni vipi hii ofisi ya spika itahamia jimboni mwa spika mpya? Au labda mawazo ya serikali ya kikwete ni kwamba kila mbunge atakaeukwaa usipika itamlazimu kahamishia makazi yake Urambo.
Ama kweli ukistajabia ya Msa utayaona ya Firaun
 
“Wakati nazindua kampeni zangu Jangwani, nilizungumza kuhusu fedha zilizochotwa na CCM katika mfuko wa matumizi ya kawaida (Other Charges) kwa ajili ya kufanyia kampeni zirudishwe, vinginevyo suala hili nitalilipua …lakini nashukuru kwamba agizo langu limetekelezwa, kwani fedha zote zimerejeshwa hata kabla sijaingia Ikulu,” alisema.

Hii sehemu imenifariji sana na imethibitisha kuwa JK anafaanya kazi kwa maagizo ya Slaa kama alivyosema Slaa akiwa Musoma

Slaa = CHADEMA +++++ mwendo mdudo!
 
Ni kweli kabaisa aliyasema hayo, mimi nilikuwepo kwenye ho mkutano.

Kuna haja ya kuongeza ulinzi kwa Dr. Slaa
 
Kweli leo nimekuja kuamini kwamba POLITICS IS WHO GETS WHAT,WHEN AND HOW.DK SLAA alikuwa wapi muda wote huu kusema haya anayosema sasa kuhusu spika sitta na jk. SLAA alikuwa mbunge na alikuwa na nafasi ya kuyasema haya kama hoja binafsi ndani ya bunge .Mimi nauona huu ni unafiki tu unaotumiwa na wanasiasa wengi hapa nchini hasa kwa wale waliofilisika kisera
 
Kweli leo nimekuja kuamini kwamba POLITICS IS WHO GETS WHAT,WHEN AND HOW.DK SLAA alikuwa wapi muda wote huu kusema haya anayosema sasa kuhusu spika sitta na jk. SLAA alikuwa mbunge na alikuwa na nafasi ya kuyasema haya kama hoja binafsi ndani ya bunge .Mimi nauona huu ni unafiki tu unaotumiwa na wanasiasa wengi hapa nchini hasa kwa wale waliofilisika kisera
Usidhani kuwa unaweza kuwahadaa watanzania wewe, nani asiyejua kuwa Dr. Slaa ndio aliyetaja list of shame ya mafisadi. He has made so much noise kwenye swala zima la ufisadi. Kuna ufisadi mwingi sana TZ huwezi kupata nafasi ya kusema yote, nchi inaufisadi katika kila sector na mengi tu hujayasikia.

Dawa ni moja tu ONDOA KIKWETE na CCM yake madarakani
 
Mie nafikiri akina Sitta na wengineo ni bora wanyamaze cos kila watakaloliongea linajibiwa kwa kishindo kikubwa na Dr. Slaa. He is the master of content, the master of details.

I feel proud kuwa na rais mwenye uwezo wa kujenga hoja kama huyu. BIG UP DR. SLAA!!
 
Kweli leo nimekuja kuamini kwamba POLITICS IS WHO GETS WHAT,WHEN AND HOW.DK SLAA alikuwa wapi muda wote huu kusema haya anayosema sasa kuhusu spika sitta na jk. SLAA alikuwa mbunge na alikuwa na nafasi ya kuyasema haya kama hoja binafsi ndani ya bunge .Mimi nauona huu ni unafiki tu unaotumiwa na wanasiasa wengi hapa nchini hasa kwa wale waliofilisika kisera

pumba!
 
Aisee maneno ya Dr. Slaa ni matamu sana... hivi sasa hivi elimu ambayo sio bure serikali inatumia 1.3 Trillion eehh... na Afya ya sasa hivi ambayo sio bure serikali inatuma 0.9Trillion... ikiwa bure itakuwa kiasi gani... wadanganyika?
 
Yah kweli CCM wanamatumizi makubwa kwenye serikali yao chai beba ya kwako
 
Mi natamani kungekuwa na kupigiana kura, yaani ukoo wangu wote ningewaomba nikawapigie, na tulivyo wengi................................
 
Thats real,nchi inanuka ufisadi kila secta nd maana tunazidi kuwa maskini na tegemezi,tupende mabadiliko kwa kumchagua Dk Slaa na CHADEMA kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom