Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
WAKUU
Tusifanye masikhara huu mchezo unaofanyika pale Kawe na kule Kimara Temboni, haufai na hauna ustawi kwa afya ya Taifa letu. Na huwa ni nashangaa sana @Wizara Mambo ya ndani, wanalea na kutetea huu ujuha kwenye Taifa linalohitaji jitihada za ziada kujikwamua ili Wananchi wake waweze kujimudu kimaisha. Cha kushangaza hiyo Wizara na baadhi ya Viongozi Waandamizi ndio wamekuwa ndio kama moja ya wanaobariki haya mambo.
Kinachoumiza na kukera kwenye hili Taifa.
1. Watu wanaendelea kuwa masikini
2. Upatikanaji hata wa mahitaji ya muhimu ya Kibinadamu umekuwa na changamoto.
3. Wagonjwa wako wengi tu mahospitalini
4. Wanaohitimu elimu tena kwa kugharamiwa na Serikali wapo tu mitaani na ajira yao imekuwa ni Kubeti
5. Rasilimali za nchi hazina tena manufaa kwa Wananchi.
Badala yake Serikali imeruhusu mambo yasiyokuwa na ustawi wala manufaa kwa Wananchi watu wamezidi kuwa watumwa kwa hawa Matapeli wa miujiza na ulaghai. Watu wapewe elimu ya stadi za maisha sio kuruhusu wawe Watumwa kwa Walagai na Wanaotumia dini kujineemesha.
Nawasilisha.