Siungi Mkono Kujengea makaburi

Siungi Mkono Kujengea makaburi

Kiplayer

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2018
Posts
1,180
Reaction score
1,964
Huwa sielewi nini faida ya kujengea makaburi ingawa Huwa nashiriki. Ndugu wanagombana kisa michango, tunaingia gharama hadi kukopa kwa ajili hiyo.

Hakuna thamani inayoongezeka baada ya kufukiwa.
 
Wengine wana amini Kaburi ni nyumba ya marehemu. Nyumba lazima iheshimiwe haiwezi kuachwa katika mazingira mabovu

So lazima itengenezwe katika hali mzuri iwe na muonekano wa kuvutia.

Lakini pia kutengeneza unique kwa ajili ya utambuzi maana siku hizi makaburi yamefanywa kumbukumbu.

Yani sehemu yenye makaburi zaidi ya 2,000 ni ngumu sana kuweza kujua kaburi la ndugu yako iwapo makaburi yote yatakuwa ya udongo.
 
Kuna kipindi nli stuck kinoma mambo yakawa magumu (ugumu ambao hauelezeki) Aunty yangu akanishauri "nenda kafanye usafi kwenye makaburi ya wazazi wako uombe baraka zao" nlikua nna mda mrefu sana sija enda huko , basi nikaenda huko nikafanya usafi nikarudi zangu town mda si mrefu nikapata kazi

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Ukiwa mvivu na mnyimi/mchoyo Kila kitu cha kijamii utajoji na utaona kama wanakuibia.Lakini ukiwa mchapa kazi na usiye na roho ya uchoyo utaunga mkono Yale yanayofanywa na jamii kwa mantiki ya kuleta umoja na mshikamamo😃
 
Back
Top Bottom