Kwanni serikali imeamua kubeba mzigo wa kuwatafutia maeneo wamachinga? Hawa wanaojiita wamachinga ni wahalifu maana wamekiuka Sheria na taratibu mbalimbali za nchi kwa kuamua kujenga mabanda barabarani ama kupanga bidhaa mbele ya maduka ya wafanyabiashara.
Nilitegemea watu hawa, mmoja mmoja ama kwa umoja wao wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Ama kwa kuhurumiwa wafurushwe bila huruma kutoka ktk maeneo hayo haramu halafu wao wenyewe watafute mahala sahihi pa kwenda.
Kama serikali inaona ni sahihi kuwatafutia wahalifu (wamachinga) maeneo mbadala, basi ifanye hivyo pia ktk makundi mengine ya wahalifu kama ifuatavyo:-
1. Waliovamia na kujenga kwenye hifadhi ya barabara, open spaces na taasisi za serikali wapewe viwanja.
2. Wafugaji wanaochungia maeneo ya hifadhi wahamishiwe maeneo yenye malisho.
3. Iwajengee nyumba ombaomba wote nchi nzima.
4. Wapiga debe wote wanunuliwe mabasi na serikali.
5. Wavuvi wanaotumia nyavu haramu (makokoro) serikali iwapatie nyavu halali. Siyo kama ilivyo sasa amabapo wavuvi huchomewa nyavu zao na kuachwa masikini kabisa
Watu wote ktk makundi yote haya wamekiuka Sheria na taratibu ndiyo maana huwa wanatiwa nguvuni wakikamatwa. Iweje hawa wahalifu (wamachinga) ambao wamevunja Sheria za nchi machana kweupe wananyenyekewa??
N.B. Wamachinga waondolewe kwa nguvu maeneo yasiyoruhusiwa. Wasibembelezwe.
NIMEJENGA HOJA, NAOMBA NIJIBIWE KWA HOJA. NISIBEZWE.