Siungi mkono Serikali kuwatafutia maeneo wamachinga. Hawa ni wahalifu walipaswa kuchukuliwa hatua

NIMEJENGA HOJA, NAOMBA NIJIBIWE KWA HOJA. NISIBEZWE.

Fikiri zaidi ya ulivyofikiria.
Machinga si waharifu na serikali inajukumu la kumtafutia nafasi kila mmoja wao kwa sababu-:

SERIKALI ILIWAHURUSU kufanya shughuli zao katika maeneo hayo. KITAMBULISHO CHA MACHINGA umekisahau? Kwenye flyover unayopanda pamoja kodi zako usisahau humo kuna jasho la 20,000/ za hao unawaita waharifu.

Hii ikupe akili kwamba wanasiasa si watu wa kuwaamini. Tumaini langu utafikiri upya.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Na mvuvi haramu nae akale wapi mnapo mnyang'anya nyavu zake?
Jibu zuri sana hili mkuu. Wavuvi walilia sana kwa kunyang'anywa mitumbwi na nyavu zao kipindi Luhaga Mpina akiwa waziri. Hatukuona hatua za kuwapatia mitumbwi na nyavu
 
SERIKALI ILIWAHURUSU kufanya shughuli zao katika maeneo hayo. KITAMBULISHO CHA MACHINGA umekisahau? Kwenye flyover unayopanda pamoja kodi zako usisahau humo kuna jasho la 20,000/ za hao unawaita waharifu.
Wafugaji wanaofukuzwa kila mahala nchi hii nao wanalipa Kodi. Wavuvi wanaochomewa nyavu zao pia wanalipa Kodi.

Hivyo kisingizio Cha kulipa Kodi isiwe sababu ya kubariki ubaguzi hui. Kama wamachinga wanasaidiwa kwa kutafutiwa maeneo basi wavuvi, wafugaji na makundi mengine wasaidiwe pia
 

Na mvuvi haramu nae akale wapi mnapo mnyang'anya nyavu zake?
Kazi kwelikweli!! Ila fahamu aliyewanyima machinga, ni huyohuyo aliyekupa wewe! Hakuna anayependa shida ni maisha tu haya, unatakiwa ukue mkuu,!
 
Ukiwa kula kulala huwezi jua Hakuna apendae kuwa machinga au bodaboda
 
SIKU ZOTE ASHIBAYE HAMJUWI MWENYE NJAA.
 
Wachukulie hatua halafu uone jinsi watakavyoanza kuchoma moto maduka ya watu Kariakoo na kuwatia watu hasara.
Tunaweka wazee wa mabaka (JW) wawe wanafanya jogging mitaa ya Kariakoo na mingine kwa miezi mitatu tuone kama watachoma...
 
Kama unaona wamachinga watafaidika una hiari ya kuwa mmachinga
 
Wafugajina wakulima ni wengi Sana mkuu ((~80%). Wafugaji kwa miaka can mingi wameporwa mifugo yao. Kuna mwaka waliambiwa wahamie mikoa mingine wakapoteza Sana mifugo yao
Mbona maeneo ni mengi tu wahamie
 
Naunga mkono kuwa wasitafutiwe maeneo, hao ni wahalifu na wavunjaji sheria. Mheshimiwa rais usiwabembeleleze, hii nchi siyo ya wamachinga peke yao. Wapo watu wengi tu wenye adabu na nidhamu. Wamachinga hawafai, ni wahuni na wachuuzi tu, haiwezekani tuwe Taifa la wachuuzi. Waondoshwe kwa nguvu hao wabakaji, wezi na wauaji.
 
Mapato ya serikali yanakosekana dhidi ya wakwepa kodi wakubwa na wenye mamlaka kukosa weledi na uaminifu dhidi ya viapo vyao
 
Huyu mzee hakika alikuwa mwamba na hatatoka akikini mwenu nyie gays
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…