Siungi mkono wachezaji wa Yanga kumgomea kocha mazoezi

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Nikiwa kama mdau wa mpira sijapendezwa na kitendo kilichofanywa na wachezaji wa YANGA kwa kumgomea kocha Mazoezi kwa sababu za kutolipwa mshahara wao karibia siku 20.

Kocha sio mwajiri wao mwajiri wao ni club Ya Yanga hivyo sikuona sababu za kumgomea kocha na pale kuna Kaptaini,Msaidizi wa kaptaini sidhani kama walishindwa kuzungumza na uongozi juu la suala hilo.

Sikatai siku izi Pesa kwanza uzalendo baadaye ila wangezingatia itifaki kabla ya kuchukua jukumu la kugoma.

Kama mchezaji labda aligoma kwa Ajili ya mshahara wa Milioni 10 mfano ndo ijumaa Yanga angekua anacheza na Simba akaja mtu akampa millioni 30 ili Auze au acheze chini ya kiwango sidhani kama angekataa.

Hapa ndo napata Picha kwanini Sir ALEX FERGUSON aliwauza wachezaji wakiwa kwenye fomu yao kama Vile David Beckam,Jaap Staam..nk yule mzee alikua mfuasi sana wa Nidhamu katika timu.

Mgomo ni Hatua za mwisho mwisho kabisa endapo njia zote za kutafuta muafaka zimegoma.

Wachezaji wa Yanga na Tanzania kwa ujumla bado mnasafari ndefu sana kaeni na viongozi wenu mtatue matatizo yenu kwa njia ya maridhiano.

Ni hayo tu.
 
Kawalipe wewe basi
 
Gazeti la champion lina sababu tofauti na mshahara
 
Manji kaamua kuwanyoosha,Mzee Akilimali hivi hawezi kuwalipa?..
 
Wanataka kugoma kupinga bomu Chirwa kupewa mshahara wa milioni 10 kwa mwezi huku hana mchango wowote wa maana kwenye timu.
Sasa ndo kumgomea kocha hawajui kuwa kocha anaprogramu zake na nani aliyemsajili chirwa kwani?
Waache migomo wacheze mpira mpira bila nidhamu ni sawa na mwandishi wa habari bila kalamu.
 
Hata hvyo bado mgomo upo kwa mechi niliyoiona leo co Yanga ninayoijua
Mpira nimefanikiwa kuangalia anzia dkk 66... mwishoni walicheza kwa jitaida kutafuta goli la kuzawazisha nala ushindi ila sijajua kipindi cha kwanza.

Wachezaji wajue mpira ni kama Ajira zingine na Yanga ni mwajiri wao hivyo hashindwi kuvunja mikataba nao muda wowote,Kama waliliokuwa wanalitaka wacheze mpira waache blaa blaa nahisi wanawajua washabiki wa Yanga Muda wowote ule hawachelewi kubadilika.
 
Walipeni mishahara acheni bla bla nyingi. Na X-mas hii mnafikiri familia zao zitakula maneno.
 
Jeshini ukipewa adhabu unafanya kwanza halafu ndo unaenda kumwambia kiongozi ile adhabu ilikua ngumu sana.

La msingi kuna njia sahihi za kutatua mambo kama hayo sasa unamgomea kocha wakati yeye sio mwajiri wako what do you expect?

Kwa mfumo huu utasikia tuu kila siku Wanyama anachezea Totenham,Olunga yuko Swedeni,Halafu Kaenda South Afrika Kashindwa majaribio karudi
 
Si mliwazoesha "wakimataifa" sasa mnalalamika nini?Mmetoa droo. Look at the positive side. Mngeweza kufungwa. Pointi 1 sio haba hasa ukitilia maanani marefarii wanaogopa kuwabeba baada ya mkwara wa mwenzao Saanya.
 
Mpira nimefanikiwa kuangalia anzia dkk 66... mwishoni walicheza kwa jitaida kutafuta goli la kuzawazisha nala ushindi ila sijajua kipindi cha kwanza.

Wachezaji wajue mpira ni kama Ajira zingine na Yanga ni mwajiri wao hivyo hashindwi kuvunja mikataba nao muda wowote,Kama waliliokuwa wanalitaka wacheze mpira waache blaa blaa nahisi wanawajua washabiki wa Yanga Muda wowote ule hawachelewi kubadilika.

Uwezi kufanya kazi kama ujalipwa. Sio wajinga kugoma ni wanataka stahiki zao. Ndio maana ujasikia wakilalamikiwa na viongozi kwasababu ni haki yao.
 
ndo nimeona pia marefa Wa bongo hawafai wanazibeba timu kubwa Leo dk 45 za kwanza zilivyoisha meza iliongeza dk 3 lakini refa alipiga dk 6 likewise kipindi cha pili inamaana alitaka kuibeba yanga au Hanna connection na Wa mezani?
 
Mkuu hapo umeongea kishabiki yule kipa wa African Lyon alijiangusha na kupelekewa kuzawadiwa kadi ya njano hivyo ilibid refa kufidia ule muda wa nyongeza sheria za sasa ni tofauti na zamani hata zile dakika za nyongeza muda unasimamishwa
 
Back
Top Bottom