Siungi mkono watu Kumchukia Diamond kisa aliipigia kampeni CCM

Siungi mkono watu Kumchukia Diamond kisa aliipigia kampeni CCM

COARTEM

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2013
Posts
3,603
Reaction score
3,658
Wanaharakati wa Twitter hasa kutoka CHADEMA wakiongozwa na Kigogo 2014, Hilda Newton, Martin M.M, Boniface Jacob wanaendesha kampeni ya chuki kwa Diamond asishinde tuzo ya BET AWARDS 2021. Wanaharakati hawa wa CHADEMA wao wanampigia kampeni Burna Boy kutoka Nigeria ili awe mshindi.

Hivi unajiuliza hawa CHADEMA hizi kampeni zina mkono wa chama chao au ni kikundi cha watu tu wa CHADEMA wameamua kukichafua hicho chama.

Nchi hii ipo huru kuwa mpenzi wa chama chochote, iweje mtu akiwa mpenzi wa CCM aonekane ni msaliti?

Diamond ameanzisha Wasafi Radio na Wasafi TV. Kupitia hivyo vyombo vya habari ametoa ajira nyingi kwa watanzania. Ni mwanamuziki gani mwingine wa Tanzania ambaye ameweza kuanzisha vitu vinavyoajiri watu wengi kiasi hicho?

Hebu tuache chuki za kijinga.

1622450906024.png

 
Wako huru kumsapoti yeyote kama wewe ulivyo huru kumsapoti diamond, halafu kama ni wanaharakati wa kisiasa wako sahihi kwanini unataka wamsapoti aliyeungana na watesi wao CCM kuwateka, kuwaua, kuwanyanyasa na kuwabeza kwa nyimbo zake?
 
Haya mambo ya TV/Radio. These are petty issues. Kuna vutu FUNDAMENTAL. Huyu alikiuka fundamental obligation ya kupinga udhalimu wa CCM. Alishirikiana na watesi, wauaji, wabakaji, watekaji, wauaji, wabambkia kesi etc etc. Hivyo Nasibu apingwe kwa kila hali. Wanachokifanya uliowataja, wako sahihi kabisa.

NOTE: CDM haihusiki na hilo. Hakuna kauli ya CDM kuhusu hilo. Do not speculate
 
Hawa ndo Chadema bana, Wana roho mbayaaaa ilopitiliza, Wana Husda, uharamia wa nafsi, utashangaa Hawa ndo wapingaji wa kinachoitwa unyanyasaji na udhalilishaji, huku wakikrnua meno na kufurahia mambo mabaya ya mkutayo binadamu.

Kuanzia wanachama mpaka viongozi wao,😂😂😂.

Leo wanamfanyia hivyo huyo kijana, vipi akitunga nyimbo na yeye ya kuitangaza vibaya Chadema je wataskia raha?

Yani ni kikundi cha kihuni chenye laana ya nchi.
 
Mtu yeyote yupo huru kumpigia kampeni yeyote yule.

Kwa upande mwingine, kuna kazi nyingine, hutakiwi kujishikamanisha na chama fulani moja kwa moja. Ukiamua kujishikamanisha na chama moja kwa moja, hiyo shughuli yako itaonekana ina mahusiano ya moja kwa moja na hicho chama, na kuhasimiwa na upande mwingine au kundi neutral ni halali, na kukosa wapenzi tika kwa makundi hasimu siyo ajabu. Kwa hiyo wasanii wapo huru kushikamana na vyama lakini wawe huru pia kuyapokea matokeo.

Kwa ule uchafu, ushetani na uharamia uliokuwa umefanywa na marehemu Magufuli, kabla na wakati ya uchaguzi, yeyote aliyeunga mkono au kushiriki, anakuwa sehemu ya ushetani. Anastahili kulaaniwa na kila mtanzania mwenye akili timamu, mdemokrasia na anayelipenda Taifa lake, japo kuna nafasi ya kujirudi na kujisahihisha, kwa waliokuwa wamekengeuka. Kwa kuoitia mtu mmoja Taifa lilinajisiwa, na kwa kupitia mmoja Taifa linaweza kuponywa.
 
Chama Cha mapinduzi,
Hakina kosa lolote kilikuwepo toka tunaita TANU,Ni chama kinachojulikana sehemu kubwa Sana Tanzania nzima.

Kimemulika kata huko vijijini ndani ndani ambako wakazi wa huko hawajui hata maana ya Chadema,CUF n.k,ukweli unaouma Ni kuwa Diamond platinum anaonewa Sana ,Tena Sana.

Pasi na Shaka Mimi najua wasanii wengi hata siasa hawajui vizuri,wanachoangalia wao Ni wapi wakijiunga watajipatia mkate wao wa kila siku,

Sanaa Ni ofisi yao,Ni kazi yao,Ni sehemu ya vipato vyao,hata ingekuwa mimi aina ya serikali ya awamu iliyopita Ni msanii gani angeonesha kutokusapoti?nisieleweke vibaya ila adui akikushinda nguvu ungana nae,

Sisi tupo huku nyuma ya keyboard tunakosoa tutakavyo kwakuwa si rahisi sisi kuonekana, Diamond platinum Ni brand tayari inayoonekana,

Myself nitampigia kura Diamond platinum,kwakuwa Ni mtanzania mwenzangu,na ni sehemu ya kuendelea kumuunga mkono

Burna boy Ni mega artist kwa Sasa ana vigezo vingi japokuwa Mimi simpigii kura

NB: kila mmoja ana Uhuru wa kumchagua amtakaye awe,Chadema, CCM,Simba,Yanga,awe timu kiba,n.k
 
Wako huru kumsapoti yeyote kama wewe ulivyo huru kumsapoti diamond, halafu kama ni wanaharakati wa kisiasa wako sahihi kwanini unataka wamsapoti aliyeungana na watesi wao CCM kuwateka, kuwaua, kuwanyanyasa na kuwabeza kwa nyimbo zake?
Kama unaanzisha kampeni ya kuhamasisha watu wasimpgie kura mwanamziki kisa alikuwa chama tofauti na chama chako, siku ukipata madaraka utakamata hata mali za waliokuwa wanakupinga, unaweza kuwaweka ndani pia.

Hizi ni tuzo za mziki siyo za kiongozi bora. Sasa hata wanaodai demokrasia wameanza kutumia njia ya au uko nasi au wewe ni adui yetu, same as waliyekuwa wanamlaumu kuwa anataka kugeuza nchi yote kuwa ya ccm.
 
Kama unaanzisha kampeni ya kuhamasisha watu wasimpgie kura mwanamziki kisa alikuwa chama tofauti na chama chako, siku ukipata madaraka utakamata hata mali za waliokuwa wanakupinga, unaweza kuwaweka ndani pia...
Tatizo sio chama bali ni kuungana na wadhulmati hata angeungana na wasaliti wa Chadema covid 19 bado wangekuwa sahihi kutomsapoti.
 
Back
Top Bottom