Siyo sahihi Waziri Mkuu kumkemea Mkaguzi wa Ndani MSD

ego

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2013
Posts
1,620
Reaction score
1,407
Yawezekana mimi ambaye sijawahi kupitia chuo cha uongozi "Uongozi Institute" sijui namna bora ya kuongoza lakini kwa busara tu za kawaida siyo sahihi kabisa kwa waziri mkuu kumkaripia mkaguzi wa ndani wa MSD.

Ilitakiwa waziri mkuu kuonyesha ukali kwa waziri wa afya, na kuhoji haya yanatendeka akiwa wapi? na kutoa maagizo kwa wote waliohusika kuchukuliwa hatua.

Waziri Mkuu akishamuwakia waziri naye anashuka chini na kuwashia moto mkurugenzi na bodi.

Mkurugenzi na bodi nao wanauwasha kwa waliohusika ndani ya MSD.

Lakini sasa waziri mkuu anawaruka watu wote hawa na kwenda chini kumuwashia moto mkaguzi.

Hawa wa kati kati hawa wanabaki kama jambo haliwahusu.

Ni lazima jambo linapotukia kwenye taasisi basi kila kiongozi aliyeko kwenye chain apate ile kashi kashi ili kesho wote wanaohusika wawe makini mambo hayo yasitokee tena.

Na kama hayo ndiyo wanafundishana uongozi institute basi na kwenyewe tubadirishe mitaala haraka sana
 
Ukipishan na Mke wa kijana wako anaingia Lodge .

Utakaa kimya na kuacha aendelee huku usubiri kijana wako atoke alikokua, ndo umuulize Ulikua wapi mpaka mkeo anaingizwa Lodge???.

Kiongozi ni Kiongozi unawajibika katika Kila Mahali unapokua .

Nilichogundua kwako, Ni wale Jamaa wavivu Sanaa, alafu mnapenda kubembelezwa na kupewa nafasi ya pili sababu ya udhaifu wenu !!.
 
Ni sawa na leo hii useme Kamishina Mkuu wa TRA au Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, asiwakemee maofisa wa mikoani pale wanapofanya sivyo, kwa sababu huko kuna Mameneja wa mikoa.
 
Ukipishan na Mke wa kijana wako anaingia Lodge .

Utakaa kimya na kuacha aendelee huku usubiri kijana wako atoke alikokua, ndo umuulize Ulikua wapi mpaka mkeo anaingizwa Lodge???.

Kiongozi ni Kiongozi unawajibika katika Kila Mahali unapokua .

Nilichogundua kwako, Ni wale Jamaa wavivu Sanaa, alafu mnapenda kubembelezwa na kupewa nafasi ya pili sababu ya udhaifu wenu !!.
Na wewe utakuwa umefuata nini Lodge
 
Alichofanya mbona kipo sahihi,tena hivyo ndio itamuamsha waziri wa afya kujiuliza alikuwa wapi mpaka Waziri mkuu anatoka alipotoka kuja kumuwajibisha Mkaguzi mkuu wakati yeye yupo!...that's an indirect criticism to Waziri wa Afya na wote walio juu ya Mkaguzi.

#bampa2bampa
#mpaka2025
 
Yawezekana mimi ambaye sijawahi kupitia chuo cha uongozi "Uongozi Institute" sijui namna bora ya kuongoza lakini kwa busara tu za kawaida siyo sahihi kabisa kwa waziri mkuu kumkaripia mkaguzi wa ndani wa MSD.

Ilitakiwa waziri mkuu kuonyesha ukali kwa waziri wa afya, na kuhoji haya yanatendeka akiwa wapi? na kutoa maagizo kwa wote waliohusika kuchukuliwa hatua.

waziri mkuu akishamuwakia waziri naye anashuka chini na kuwashia moto mkurugenzi na bodi.

mkurugenzi na bodi nao wanauwasha kwa waliohusika ndani ya MSD.

lakini sasa waziri mkuu anawaruka watu wote hawa na kwenda chini kumuwashia moto mkaguzi.

hawa wa kati kati hawa wanabaki kama jambo haliwahusu.

Ni lazima jambo linapotukia kwenye taasisi basi kila kiongozi aliyeko kwenye chain apate ile kashi kashi ili kesho wote wanaohusika wawe makini mambo hayo yasitokee tena.

Na kama hayo ndiyo wanafundishana uongozi institute basi na kwenyewe tubadirishe mitaala haraka sana
Huyo aondolewe hapo, ndio anapitisha madili ya wizi, halafu anamwambia Waziri mkuu "utakavyoona inafaa" baada ya kuulizwa afanyweje
 
Back
Top Bottom