mng'ato
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 29,200
- 49,076
Hahah Museveni hana uwezo wa kumu assasinate PK nina uhakika huo,PK akitaka hata kesho kumfurusha Museveni ana uwezo huo kabisaa.Yani m7 acheze na Former CMI wake haiwezekani hio.Unazidi kudhihirisha uwezo wako mdogo ktk espionage issues.
Israel ina mahusiano makubwa ya kidiplomasia na Rwanda, Tanzania haina mahusiano mazuri na Israel ,na majuzi tu ilidhihirika UN.
kwa hiyo spies wa Rwanda hupelekwa Israel na kupewa mafunzo na trainers wa MOSSAD, yote haya hufanyika kwa maslahi mapana ya Israel.
Israel kwa miaka ya hivi Karibuni imekuwa ikiidukua Tanzania kijasusi kupitia Rwanda,zamani waliitumia Kenya.
Usidhani watu tunakurupuka tu kuandika thread, tunajua mengi ya uvunguni.
Yupo wapi yule kanali wa JWTZ mtaalamu wa IT aliyetoweka ghafla wakati wa utawala wa Kikwete?
Rwanda ilijuaje kuwa Balozi aliyekuwa anapelekwa Kigali kuiwakilisha Tanzania alikuwa ni jasusi wa TISS?
Unajua who is behind Mtikila's mystery death? And why?
Unajua ni nani ameifanya Congo isiwe stable Hadi leo and why?
Tanzania ilikuwa vizuri Sana kijasusi lakini sasa hivi hamna kitu, kuendekeza siasa kwenye kila jambo ndo kunaenda kuligharimu taifa letu.
Wewe ukikurupuka Sana kumu under rate Mr slim.
Halafu kukurupuka kwako unataka kuona Uko sawa.
Museveni keshamshtukia ndo maana alikuwa anapanga kumfanyia assassination, Gazeti la Reddpepper lilipofichua likafungiwa.
Huyu wa kwetu ndo anamwona best, hakuna urafiki Kati ya binadamu na nyoka.
Sent from my TECNO-Y2 using JamiiForums mobile app
Au hukumbuki Uganda alivyopewa kichapo pale Rwanda na Congo walipogeukana kule Congo kipindi kile wanagombea madini na wkt huo Rwanda ilikua hata haijasimama kijeshi kiviile ndo ilikua imetoka kwenye Genocide nadhani.
Ambacho hukielewi khs kinachoendelea Uganda ni kwamba Nyamwasa yule Mkuu wa majeshi wa zamani aliyekimbilia S/Africa alianza movement za kuchukua wanyalu wanaoishi Uganda kwny makambi ya wakimbizi na kuwapeleka Congo kuwatrain so tension ikaanzia hapo Kati ya Kigali na Kampala na kama huna taarifa hata kuna bus lilikamatwa hapahapa Bongo likitoka Uganda likisafirisha hao wanyalu ili wavuke kwenda Congo lkn walikamatwa wakarudishwa Uganda na kuna mashitaka mahakamani dhidi ya hao wanyalu huko Uganda.
Kwa E/Africa naamini kwa dhati mbabe wa PK ni Tz tu hao wengine hawafurukuti hata Kenya hamna kitu,Uganda,Burundi,Congo hio haihitaji maelezo mengi panaeleweka vzr tu,South sudani wao ndo hata hawakoromi kwa jamaa maana wale m23 walipelekwa na PK kumsaidia rais wao Salva kiir dhidi ya Muasi Machari so wanaijua in&out.