Sizipendi tabia hizi niwapo ndani ya daladala....!

Sizipendi tabia hizi niwapo ndani ya daladala....!

hilo la kuchungulia cm niliwahi kumkomesha bibi mmoja hivi kwenye daladala alikuwa anachungulia utadhani ile simu ameniazima, nikajisemea cha kufia nini wakati huo bando la chuo ndo jipya, nikaingia tube 8 na kuendelea kupata radha, kilichoendelea si akaanza kuwaka vijana wengine sijui hawana wazazi au ni laana

Safi sana Mkuu ulimkomesha vizuri sana. Wapo wengi kweli wenye hiyo tabia ndani ya Madaladala yetu haya. Nami Kesho au mbeleni nitaiiga hii uliyomfanyia huyo Bibi.
 
Wale wanaoongea na simu saa zima tena mambo ambayo ni personal.. Kwenye daladala inatakiwa kuongea brief au kama ni kuongea kwa kirefu iwe mambo muhimu ya kazi au biashara...
 
Duh hio namba 8 ilinikuta ndani ya ndege kuna mijamaa sijui kama wa mbele au nyuma yangu ilikuwa inajamba hatareee mwanzo mpaka mwisho wa safari. Halafu nilikaa na demu mkali wa kizungu kushuka naona ananiangalia mie kama ndie niliekuwa najamba. Nilitamani nimfuate nimuulize mbona unaniangalia hivyo? Lakini nilikuwa nasubiri Luggage yangu tu.
 
Pole sana Mkuu ila huyo Mzungu aliondoka na alama ya kudumu juu yako kuwa Wewe ndiye " ulijamba " na usishangae yawezekana hata Picha alikupiga na sasa Wajukuu zake huko Ulaya wakitaka kucheka anawaonyesha tu Picha yako ya Mjambaji maarufu ndani ya flight. au ulijamba kweli Mkuu?
 
Yan tunalazimishwa kuwa na tabia moja, tabia sawa.......
Bila hizo kero daladala hazina wapandaji........
 
Pole sana Mkuu ila huyo Mzungu aliondoka na alama ya kudumu juu yako kuwa Wewe ndiye " ulijamba " na usishangae yawezekana hata Picha alikupiga na sasa Wajukuu zake huko Ulaya wakitaka kucheka anawaonyesha tu Picha yako ya Mjambaji maarufu ndani ya flight. au ulijamba kweli Mkuu?
[emoji1] hapana mkuu sikujamba mimi.
 
  1. Mtu kukulazimisha kwa lugha yake ya mwili ( body language ) umlipie Nauli na ni hasa hasa kwa Mabinti na Wanawake watu wazima kabisa.
  2. Mtu amepanda daladala halafu bahati mbaya au sijui nzuri ile anaingia tu akakuona na yeye akaenda kukaa siti ya mbali kidogo na Wewe kisha anaanza kukuita na kukuongelesha kwa sauti ya juu kabisa kwamfano " Oya Gentamycine uko poa lakini? Shemeji hajambo? Vipi uliona jana Messi alivyokosa lile goli? ".
  3. Unajisomea Gazeti lako jirani yako kila page unayoifungua yeye lazima tu " ataikodolea " sasa basi bora akodolee tu kwa mbali mbali au kwa kujishtukia lakini Lijitu linasogeza kabisa Uso lake sambamba na Uso wako huku pumzi zetu zikipishana tu njia nalo linasoma Habari ile ile.
  4. Unamwomba namba ya Simu Mdada au Mwanamke kwa utaratibu kabisa uliotukuka Yeye anakutajia kwa sauti au anakuomba umpe Simu yako akuandikie kitu ambacho kwa upande fulani " kinawachoresha " sana Mabazazi.
  5. Umekaa siti moja na Demu tena hata hamjuani halafu Konda linatoka huko lilikotoka likija kuchukua nauli ukimpa kwa mfano " buku " utasikia anakuuliza na huyo au? Hii hali hutufanya sisi wenye aibu kujikuta hata kama hukuwa na nia ya kumlipia nauli huyo Demu basi unakubali tu Konda akate nauli ya Wawili hivyo kukuharibia kabisa bajeti yako.
  6. Mtu mzima kasimama pembeni yako lakini kila unachokifanya katika Simu yako yeye atakukodolea tu mwanzo mwisho wakati huo huo na Yeye Simu anayo lakini yake haiangalii na mkazo upo kuangalia unachochati.
  7. Dada ambaye kapanda daladala kisha akavutiwa na Wewe halafu baadae anajifanya anakuuliza kama Simu yako ina credits za kutosha na ukimwambia ndiyo anakuambia tafadhali ipige hii namba nina shida na huyu Mtu kisha ukianza kuipiga ile namba yeye huku katika Simu yake anaipunguza sauti na ikiita huku haipokelewi haraka haraka anakuambia basi achana nayo labda yupo busy halafu mkishashuka tu katika daladala baadae anakupigia na " Kujitongozesha " kwako.
  8. Mtu yeye mwenyewe tu na yawezekana ni kwa bahati mbaya " anajamba " na Wewe ukiisikia ile harufu unaweza kujua inatokea direction gani lakini huyo Mhusika ndiyo anajifanya kuichukia hiyo harufu huku akisonya sonya mule ndani na kukemea.
  9. Kuazimana Gazeti. Kama unapenda Gazeti fulani si ununue tu lako ili " tusichoshane? "
Hizi ni baadhi tu zangu na Wewe unaweza pia ukaongezea na zako. Tunaopanda daladala " mwanzo mwenga " na wenye haya " maudhi " haya au " kero " hizi hebu tujirekebishe basi.

Naomba kuwasilisha.
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Mama anampigia simu binti wa kazi nyumbani: HALAFU DADA USISAHAU MTOTO AKIHARISHA UFUE HIZO NEPI ZAKE ZITAKATE NISIKUTE ZINA MIHARO PIA MATAPISHI UYAFUTE KABISAA NGUO ZISIBAKIE NA HARUFU MBAYA
hahahahahahahah daah hatar sana,, afu yeye yupo konfotabo
 
Duh hio namba 8 ilinikuta ndani ya ndege kuna mijamaa sijui kama wa mbele au nyuma yangu ilikuwa inajamba hatareee mwanzo mpaka mwisho wa safari. Halafu nilikaa na demu mkali wa kizungu kushuka naona ananiangalia mie kama ndie niliekuwa najamba. Nilitamani nimfuate nimuulize mbona unaniangalia hivyo? Lakini nilikuwa nasubiri Luggage yangu tu.
hahahahahaha
 
Back
Top Bottom