GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
- Mtu kukulazimisha kwa lugha yake ya mwili ( body language ) umlipie Nauli na ni hasa hasa kwa Mabinti na Wanawake watu wazima kabisa.
- Mtu amepanda daladala halafu bahati mbaya au sijui nzuri ile anaingia tu akakuona na yeye akaenda kukaa siti ya mbali kidogo na Wewe kisha anaanza kukuita na kukuongelesha kwa sauti ya juu kabisa kwamfano " Oya Gentamycine uko poa lakini? Shemeji hajambo? Vipi uliona jana Messi alivyokosa lile goli? ".
- Unajisomea Gazeti lako jirani yako kila page unayoifungua yeye lazima tu " ataikodolea " sasa basi bora akodolee tu kwa mbali mbali au kwa kujishtukia lakini Lijitu linasogeza kabisa Uso lake sambamba na Uso wako huku pumzi zetu zikipishana tu njia nalo linasoma Habari ile ile.
- Unamwomba namba ya Simu Mdada au Mwanamke kwa utaratibu kabisa uliotukuka Yeye anakutajia kwa sauti au anakuomba umpe Simu yako akuandikie kitu ambacho kwa upande fulani " kinawachoresha " sana Mabazazi.
- Umekaa siti moja na Demu tena hata hamjuani halafu Konda linatoka huko lilikotoka likija kuchukua nauli ukimpa kwa mfano " buku " utasikia anakuuliza na huyo au? Hii hali hutufanya sisi wenye aibu kujikuta hata kama hukuwa na nia ya kumlipia nauli huyo Demu basi unakubali tu Konda akate nauli ya Wawili hivyo kukuharibia kabisa bajeti yako.
- Mtu mzima kasimama pembeni yako lakini kila unachokifanya katika Simu yako yeye atakukodolea tu mwanzo mwisho wakati huo huo na Yeye Simu anayo lakini yake haiangalii na mkazo upo kuangalia unachochati.
- Dada ambaye kapanda daladala kisha akavutiwa na Wewe halafu baadae anajifanya anakuuliza kama Simu yako ina credits za kutosha na ukimwambia ndiyo anakuambia tafadhali ipige hii namba nina shida na huyu Mtu kisha ukianza kuipiga ile namba yeye huku katika Simu yake anaipunguza sauti na ikiita huku haipokelewi haraka haraka anakuambia basi achana nayo labda yupo busy halafu mkishashuka tu katika daladala baadae anakupigia na " Kujitongozesha " kwako.
- Mtu yeye mwenyewe tu na yawezekana ni kwa bahati mbaya " anajamba " na Wewe ukiisikia ile harufu unaweza kujua inatokea direction gani lakini huyo Mhusika ndiyo anajifanya kuichukia hiyo harufu huku akisonya sonya mule ndani na kukemea.
- Kuazimana Gazeti. Kama unapenda Gazeti fulani si ununue tu lako ili " tusichoshane? "
Naomba kuwasilisha.