Sizitaki Mbichi Hizi!!

Sizitaki Mbichi Hizi!!

Nakumbuka ushirikiano uliokuwepo kati ya shule na wazazi...ukitoroka tu mdingi anakupeleka skuli na kukuadhibu yeye mwenyewe mbele ya walimu na wanafunzi...dah ilikua soo....nakumbuka tarehe za kufunga shule mnakaa chini ya mti afu kuimba kwa sana huku viroho vikidunda kinoma unasubiri cjui utakuwa wangapi...mana ilikua hamna kupewa ripoti mlikua mkisomewa siku ya kufunga shule matokeo yenu......nakumbuka mmefungua shule yanasomwa majima ya ambao hawakwenda zamu kufanya usafi wakati wa likizo mnachezea stiki sana tu.....
 
Nakumbuka ushirikiano uliokuwepo kati ya shule na wazazi...ukitoroka tu mdingi anakupeleka skuli na kukuadhibu yeye mwenyewe mbele ya walimu na wanafunzi...dah ilikua soo....nakumbuka tarehe za kufunga shule mnakaa chini ya mti afu kuimba kwa sana huku viroho vikidunda kinoma unasubiri cjui utakuwa wangapi...mana ilikua hamna kupewa ripoti mlikua mkisomewa siku ya kufunga shule matokeo yenu......nakumbuka mmefungua shule yanasomwa majima ya ambao hawakwenda zamu kufanya usafi wakati wa likizo mnachezea stiki sana tu.....
ahahaa mkuu great moments sana zile ukiwa wa kwanza unapewa madaftari matatu pia unaosha sana jina
 
tulikuwa tukipata malimao yaloiva
maganda ni starter
huli limao unless umeshow solidarity katika kula ganda
uwe unaskia chungu au tamu
lazima ule, si unajua darasa la 3 hadi la 5
mkikubaliana kitu ni lazima wote mfanye
la sivyo unatengwa
yaani malimao yalikuwa matamu kuliko hata chungwa yaani mnakula kila kitu anzia ganda hadi mbegu

 
Kama ni kipanga ndo ilikuwa siku ya kuosha jina kwa kweli

ila kama ni mchokozi unaviziwa kupigwa
unakaa kiroho juu juu
jamani wavulana walikuwa wanatuonea
sitamsahau Yona
alipoacha shule, nilipop shampeni
duh nilikuwa mnyonge wake

ahahaa mkuu great moments sana zile ukiwa wa kwanza unapewa madaftari matatu pia unaosha sana jina
 
View attachment 43266

Imekukumbusha nini.....

Sizitaki mbichi hizi, sungura alisema hivyo baada ya kushindwa kuzifikia ndizi zilizo iva kwa kuwa zilikuwa mbali, alijalibu sana kuruka akashindwa akabaki kuzikashifu,
Watu wengi wakikosa kufikia malengo yao hubadilika nakutukana au kuchua hali ya hewa nakusema kwanza mbaya, hanahadhi yakuwa na mm, mchafu, masikini namengineyo mengi.
 
Saa hiyo maza keshatembeza kichapo cha kutoweka, kuiba mazambarau ya watu na kutojifunza kupika na dada. Ukipumua. Tu dingi anaingia na kutembeza kichapo cha hujaoga hadi saa hizi,kwani ulikua kazini? Kha! Afu kesho tena unarudia, raha kweli!

Hapo kwenye red na adhabu ya kudeki, kuosha vyombo, kufagia uwanja wiki mbili bila kupumzika he he he bado ya dingi sasa mahesabu mihomowork kibao na adhabu nyingine ndani ya wiki mbili usome vitabu viwili kwa wiki na kutoa summary umeelewa nini mwehhee
 
Habari ndo hiyo hapo chini kwa wakongwe kama sie"


Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia


Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.


Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.


Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.


Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho wake akachoka, kachoka hata mkia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Sungura nakuambia.


“Sizitaki mbichi hizi” Sungura akagumia,
“Naona nafanya kazi, bila faida kujua”,
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.


Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.


Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi
 
tulikuwa tukipata malimao yaloiva
maganda ni starter
huli limao unless umeshow solidarity katika kula ganda
uwe unaskia chungu au tamu
lazima ule, si unajua darasa la 3 hadi la 5
mkikubaliana kitu ni lazima wote mfanye
la sivyo unatengwa
Kongosho umenichekesha sana dah!
Sie ilikuwa kila mtu lzm apigane na haijalishi unamweza mpinzani wako au humwezi,
Hiyo grupu ya wababe wa darasa ndio inapanga ratiba ya kupigana kila ijumaa sitasahau lol!
Mbona nilijitolea kubeba mkoba wa mwalimu wa darasa mapak darasa la tano ili nikwepe kupiganishwa!!
 
Kiukweli kusoma st kayumba raha sana,
Nakumbuka hivyo vitabu tuligaiwa wakati wa kusoma darasan then kipindi kikiisha vinakusanywa na mwalimu anaondoka navyo,
Mie si nikaondoka nacho sikukusanya nikaenda kugandamizia hiyo picha ya sungura anavyorukia ndizi,
Kesho yake nikagongewa kengele mstarini nilipewa stiki za kutosha mpaka nikapata homa lol,sitasahau kwa kweli.
 
karudi baba mmoja toka safari ya mbali,
kavimba yake mapaja na kutetemeka mwili,...
imenikumbusha nyakati tunaimba hizi huku tukisoma sizitaki mbichi hizi.
 
karudi baba mmoja toka safari ya mbali,
kavimba yake mapaja na kutetemeka mwili,...
imenikumbusha nyakati tunaimba hizi huku tukisoma sizitaki mbichi hizi.
 
Miaka hiyo nadhani ndio ila maana ya stick ilikuwa clear sana.....
Pia darasa lilikuwa limejaa majeba ile mbaya.....
Nakumbuka st kayumba yangu moja mitaa ya mgulani hapo!
Mkononi nina fagio na dumu la lita 5,
shati langu lina renki kuonyesha darasa....
Enzi hizo mchakamchaka lazima, then mnachukua namba
 
kwa kweli labda uwe umeiona hiyo picha au unaijua hadithi nyuma ya picha huwezi kukumbuka kitu... ndio mimi hapa...

hahaha! We hata kama hukumbuki jilipue tu. Sema unakumbuka TF wakati yupo mdogo alivyokuwa mroho wa vitu vya watu.
 
Wekeni basi KAMA MNATAKAMALI MTAYAPATA SHAMBANI! Miss those memos!!!!!!
 
Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia

Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.

Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.

Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.

Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho wake akachoka, kachoka hata mkia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Sungura nakuambia.

“Sizitaki mbichi hizi” Sungura akagumia,
“Naona nafanya kazi, bila faida kujua”,
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.

Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.

Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi

Ili ni shairi tu, lilisomwa na watoto wa shule za msingi darasa la nne kama kumbukumbu zangu zipo sahihi, lakini ukiwa mtu makini mwenye kutafakari uwezi kukosa kugundua hazina iliyo jificha ndani ya ili shairi.

Tafakari kisha chukuwa hatua.


Darasa la tatu. Darasa la nne ni lile la Kama mnataka mali mtayapata shambani
 
Sungura.jpg
Ulikutana naye lini na wapi?
 
Back
Top Bottom