Sizitaki Mbichi Hizi!!

Sizitaki Mbichi Hizi!!

Hadithi inayokuja, ni ya sungura sikia, hadithi uliyongoja, leo ninakuletea. Alitoka siku moja njaa alipisikia, njaa aliposikia, sungura nakuambia.

Endelea...
 
Siku hiyo akaenda, porini kutembelea,
akayaona matunda, mtini yameenea,
sungura akayapenda, mtini akasogea,
mtini akasogea sungura nakuambia...
Std III kwa mwalimu Manjoli.
 
Darasa la tatu. Darasa la nne ni lile la Kama mnataka mali mtayapata shambani

Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali
kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili
watoto wake wakaja, ili kumtaka hali
kama mnataka mali mtayapata shambani

Akatamka mgonjwa,ninaumwa kweli kweli
hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali


Duu nimechemka, hata hivyo nimebaki na kumbukumbu muhimu juu ya shairi hili hasa ninapojuiliza ni kwa nini baba yule alisema mali ipo shambani? Mbona hakusema viwandani ama ofisini? sasa walau najua huwezi kuzungumzia maendeleo au mali ya kweli bila kwanza kuwa na ardhi.

Tafakari.
 
ninaye ndege mzuri mrembo wa kusifika
rangi zake mashuhuri ni nne nawaeleza
ndizo rangi za fahari urembo kuutimiza
Ndege huyu ndege gani hapa kwetu Tanzania?
-------------------------
ni furaha kuzaliwa Tanzania, nchi yenye amani upendo,
watanzania wote twapendana,
kiswahili safi kinatuunganisha, utamaduni unatuimalisha..misingi imara walio tuwekea, watanzania wote tuwakumbuke, jk nyerere abed karume waasisi wa Tanzania, twatembea popote tanzania..
Dah!..nmechemka nyimbo zote. malizia. Mia
 
Sadiki sasa ashiba,
Chakula kingi kwa baba,
Nirudi tena kwa baba,
Nakufa hapa kwanin??
|
|
Sadiki na Sikiri!!
 
JE? WEWE UNAIKUMBUKA HII:-SIZITAKI MBICHI HIZI !!
http://1.bp.blogspot.com/-bYauF7ofh3M/TreRkhIhVwI/AAAAAAAADeE/9iUAlUoCsyM/s1600/DSCN2778.JPG Sungura.jpg

Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia


Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.


Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.


Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.


Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho Wave akachoka, kachoka hata mk-Ia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Subgura nakuambia.


"Sizitaki mbichi hizi" Sungura akagumia,
"Naona nafanya kazi, bila faida kujua",
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.


Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.


Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi.
 
du! imenikumbusha long kiaina ,sijui kama vile vitabu bado vinapatikana,
Mdau kakakiiza tafadhali nikumbushe na ile ya

karudi baba mmoja, toka safari ya mbali
watoto wake wakaja , ili kumtaka hali
wakataka na kauli, ili iwafae maishani

napenda ule ubeti wa mwisho unaosema " kama mnataka mali mtayapata shambani"
 
ni noma enzi hzo madaftari tunapewa shureni nice nakumbuka hata kuiimba
 
du! imenikumbusha long kiaina ,sijui kama vile vitabu bado vinapatikana,
Mdau kakakiiza tafadhali nikumbushe na ile ya

karudi baba mmoja, toka safari ya mbali
watoto wake wakaja , ili kumtaka hali
wakataka na kauli, ili iwafae maishani

napenda ule ubeti wa mwisho unaosema " kama mnataka mali mtayapata shambani"

Huo ubeti sasa hv inabd ubadilishwe, hauendani na hali ya sasa, unatakiwa usomeke...............
"kama unataka mali, utazipata B.O.T, bungeni, wizara ya nishati na madini n.k
 
ah..umenikumbusha mbali,enzi zile chini nna chachacha..mgongoni nna begi la dino!!!acha kabisa
 
Enzi hiyo mdingi mwl mkuu alikuwa analipwa mshahara elfu 4 kwa mwezi. Hata walimu wa primary nao waligombea ubunge na kushinda.
Sec school wanafunzi mnalipwa nauli ya kwenda na kurudi likizo.Tukawa tunafuta tiketi kwa petrol ili tuandike kiwango kikubwa.
 
duh darasa la tatu c muhimbili primary mwaka fulani hv remember that book
 
ah..umenikumbusha mbali,enzi zile chini nna chachacha..mgongoni nna begi la dino!!!acha kabisa

kumbe umesoma majuzi tu!!enzi za zamani hapakuwa na begi!!unachofanya ni kuchomekea shati halafu unayapenyeza madaftari mgongoni!!!
 
mi nilisoma mashairi haya....

huyu ni baba
baba ni mnene
baba ana ng'ombe
ng'ombe wake ni mweusi
baba anasema
kimbia ng'ombe
kimbia upesi
kimbia nyumbani
baba ana njaa

huyu ni roza
...
...
 
Back
Top Bottom