mysteryman
JF-Expert Member
- Aug 4, 2011
- 1,065
- 365
ahahaa mkuu great moments sana zile ukiwa wa kwanza unapewa madaftari matatu pia unaosha sana jinaNakumbuka ushirikiano uliokuwepo kati ya shule na wazazi...ukitoroka tu mdingi anakupeleka skuli na kukuadhibu yeye mwenyewe mbele ya walimu na wanafunzi...dah ilikua soo....nakumbuka tarehe za kufunga shule mnakaa chini ya mti afu kuimba kwa sana huku viroho vikidunda kinoma unasubiri cjui utakuwa wangapi...mana ilikua hamna kupewa ripoti mlikua mkisomewa siku ya kufunga shule matokeo yenu......nakumbuka mmefungua shule yanasomwa majima ya ambao hawakwenda zamu kufanya usafi wakati wa likizo mnachezea stiki sana tu.....
yaani malimao yalikuwa matamu kuliko hata chungwa yaani mnakula kila kitu anzia ganda hadi mbegutulikuwa tukipata malimao yaloiva
maganda ni starter
huli limao unless umeshow solidarity katika kula ganda
uwe unaskia chungu au tamu
lazima ule, si unajua darasa la 3 hadi la 5
mkikubaliana kitu ni lazima wote mfanye
la sivyo unatengwa
ahahaa mkuu great moments sana zile ukiwa wa kwanza unapewa madaftari matatu pia unaosha sana jina
Dah! Mlikuwa wezi kweli..lol
Saa hiyo maza keshatembeza kichapo cha kutoweka, kuiba mazambarau ya watu na kutojifunza kupika na dada. Ukipumua. Tu dingi anaingia na kutembeza kichapo cha hujaoga hadi saa hizi,kwani ulikua kazini? Kha! Afu kesho tena unarudia, raha kweli!
Kongosho umenichekesha sana dah!tulikuwa tukipata malimao yaloiva
maganda ni starter
huli limao unless umeshow solidarity katika kula ganda
uwe unaskia chungu au tamu
lazima ule, si unajua darasa la 3 hadi la 5
mkikubaliana kitu ni lazima wote mfanye
la sivyo unatengwa
kwa kweli labda uwe umeiona hiyo picha au unaijua hadithi nyuma ya picha huwezi kukumbuka kitu... ndio mimi hapa...
Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia
Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.
Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.
Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.
Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho wake akachoka, kachoka hata mkia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Sungura nakuambia.
Sizitaki mbichi hizi Sungura akagumia,
Naona nafanya kazi, bila faida kujua,
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.
Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.
Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi
Ili ni shairi tu, lilisomwa na watoto wa shule za msingi darasa la nne kama kumbukumbu zangu zipo sahihi, lakini ukiwa mtu makini mwenye kutafakari uwezi kukosa kugundua hazina iliyo jificha ndani ya ili shairi.
Tafakari kisha chukuwa hatua.
X-Paster anatabasamu, anasema thanx very much... Darasa la tatu.Darasa la tatu. Darasa la nne ni lile la Kama mnataka mali mtayapata shambani