Sizitaki Mbichi Hizi!!

mlikuwa na hatari kweli!!yaani petrol!!!!kumbe ufisadi tunaanza nao toka mashuleni!!!
kwa staili hiyo ya petrol sikuhizi kweli haugushi safari na kujilipa mamilioni!!!!
 
Vipi kuhusu ile ya chopeko na mnofu unaikumbuka?
 
Enzi hizooooo,...kama ni kweli kinaitwaje?

 
Standadi foo hiyo enzi hizo za mtunzi Mwl Shempemba......ila sungura gani mkubwa sawa na mkungu wa ndizi?
 
Enzi hizooooo,...kama ni kweli kinaitwaje?

...mkuu umenikumbusha mbali sana,kama kwenye maktaba yako utakutuwa na kitabu cha "MANENGE NA MANAWA",fanya juhudi nipate copy au ata photo copy yake coz nmeki-miss sana hicho kitabu...
 
Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia

Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.

Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.

Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.

Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho Wave akachoka, kachoka hata mk-Ia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Subgura nakuambia.

"Sizitaki mbichi hizi" Sungura akagumia,
"Naona nafanya kazi, bila faida kujua",
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.

Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.

Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi
 

Dah,loooong time iasee,..thanks a lot
 
Ebu toa moja basi
Hadithi inayokuja, ni ya sungura sikia.
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea.
Alitoka siku moja, njaa aliposikia.
Njaa aliposikia, sungura nakuambia.

Huo ni ubeti wa kwanza....niendelee?

 
Duuh! Wewe ni mkareeee!


 
Hadithi inayokuja, ni ya sungura sikia.
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea.
Alitoka siku moja, njaa aliposikia.
Njaa aliposikia, sungura nakuambia.

Huo ni ubeti wa kwanza....niendelee?


haha,hauja igilizia kwa safari kweli ?
 


Hii picha inanikumbusha mbali. Nimeipata sehemu ikiwa na mambo. Na hii je?

Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia

Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.

Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.

Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.

Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho Wave akachoka, kachoka hata mk-Ia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Subgura nakuambia.

“Sizitaki mbichi hizi” Sungura akagumia,
“Naona nafanya kazi, bila faida kujua”,
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.

Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.

Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi
 

SITAKI MBICHI HIZI darasa la tatu!
 
Imenikumbusha mbali sana

Hapo kama hukupita Kayumba style unatoka kapa. Hizi ni enzi za
  1. kidumu na maji,
  2. mfagio
  3. kiporo begani
  4. zawadi ya kiranja na monita
  5. Shati lillochafuka
  6. kibao cheusi
  7. miguu peku
  8. wawili kwenye dawati
  9. enzi za kutembea umbali mrefu
  10. kuvaa kibao cha kuongea kiswahili
  11. kiboko kikali ka mwizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…