LiverpoolFC
JF-Expert Member
- Apr 12, 2011
- 11,483
- 3,369
Inanikumbusha miaka 1987!
Sungura kasema na sisitaki mbivu hizi!
Sungura kasema na sisitaki mbivu hizi!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hahaha..pazi..kibao kilimgeukia..
Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia
Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.
Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.
Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.
Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho wake akachoka, kachoka hata mkia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Sungura nakuambia.
"Sizitaki mbichi hizi" Sungura akagumia,
"Naona nafanya kazi, bila faida kujua",
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.
Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.
Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi
Nikisema sizikumbuki nitakuwa nawadanganya,mimi sizijui kabisa!!!
wewe umezaliwa jana? au hukusoma st kayumba za 90s?
Nadhani meri meri huyu.
hahahahaaa...!!!. naumia naumia...nihurumie nihurumie. mia
Nimekumbuka mbali sana, tulikuwa tunakariri shairi zima.
Umejuaje? siku tukikutana nakubeba kichwa chini miguu juu, we subiri nikupandie huko mlimani kwenu. Miaunacheka nini sasa au we ndo sikiri mwenyewe?
Inanikumbusha miaka 1987!
Sungura kasema na sisitaki mbivu hizi!