Mimi lawama zangu naanza kuzitupia media, toka saa sita usiku mpaka saa sita usiku wa siku nyingine vipindi vinavyowekwa ni miziki na filamu za kifilipino. Yanayooneshwa humo sidhani kama yana mchango mzuri kwenye ukuaji na elimu ya vijana wetu.
Tujiulize kwanza ni vipindi vingapi vyenye kumjenga kijana kielimu na kimaadili vinaoneshwa na media zetu. Matokeo yake wanakufa wahadhiri, madaktari bingwa, wanasayansi wenye kuletea taifa hili sifa, wanasheria na wanasiasa mahiri kama Kawawa hakuna vipindi maalumu vya maombolezo yao.
Lakini tumeona wamekufa wasanii(Kanumba, na huyu aliyekuwa anasifia mikasi, majani na mitungi sijui naitwa Ngwea) vinawekwa vipindi maalumu kwenye media kuomboleza. Ina maana Ngwea alikuwa anaitangaza nchi yetu vizuri nje kuliko Marehemu Kawawa, Dokta F. MASSAU,Wahadhiri wetu vyuo vikuu, Majaji, Wabunge na Mawaziri wetu.
Juzi kati wanajeshi wetu wamefariki huko Sudani wakitekeleza majukumu ya kitaifa, wanaojua wanieleze hapa ni TV, radio ilirusha live shughuli nzima toka miili ilipotua uwanja wa ndege mpaka ilipoagwa pale upanga na je kulikuwa na kipindi gani maalumu cha kueleza michango na japo historia zao tu kwa kifupi kama mashujaa wetu, hakuna!!!!!!!!!