Sky Walker kwa hili la Diamond na Davido umeonyesha udhaifu

mr gentleman

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,222
Reaction score
4,689
Ishu ya Diamond na Davido imeleta mitazamo tofauti. Kuna ambao wanaona Diamond kamkosea Davido kwa kujibu mapigo na kuna wanaoona Davido kawakosea adabu watanzania kwa ujumla kutokana na tweet zao,haya mawazo ya watu na yote yanapaswa kuheshimiwa. Ila mimi nitaongelea mtazamo wa Sky Walker mwandishi ninaemwelewa sana hapa bongo kwa changamoto zake kwenye
tasnia ya burudani, Sky yeye ameenda mbali kusisitiza kupitia tweets zake na maandiko yake bongo5 kwamba Diamond inabidi ayamalize na Davido kwani bado anamuitaji Davido la sivyo ataluuz kitu. Jamaa ameshupalia sana
pengine ni kwa kuutakia mema muziki wetu ila Sky umekuwa inferior sana kwa hili.

Natofautiana na Sky , kwanza kama kuyamaliza ayamalize vipi? Aombe msamaha au? Kwanza alikuwa anatetea kwamba Davido ametafsiliwa vibaya akumaanisha habari za ushindi wa BBA na CH O ila muendelezo wa tweets zake umeonyesha wazi Davido alimaanisha alichokisema na ameendelea kukisimamia so hapa
inaonyesha ni namna gani anaamini Mtz hawezi kushinda mbele ya mnaija na akishinda basi ni hujuma wamefanyiwa. Hii ni dharau.

Point ya msingi nayotaka kusema ni kwamba anachotaka kuamini SKY na wenye mtazamo kama wake kwamba Diamond bado anamuhitaji sana Davido na kwa namna yoyote hatakiwi kumuudhi mimi nasema hapana,Diamond alimuitaji Davido hapo nyuma na sasa hamuitaji tena kama ni heshima kampa za kutosha sote ni mashaidi ila mtu anapoonyesha dharau unyenyekevu wa kitanzania inabidi tuuweke kando. Fid Q anasema nipe heshima yangu au niichukue kwa nguvu.

Pia wabongo tujiamini tuache tabia ya kupapatikia watu wa nje huu ni ugonjwa wetu mkubwa . Muziki wetu kwa sasa una nguvu sana East na Central Africa ni wasanii wetu tu hawaitumii hii nafasi ila tuna nguvu kubwa kwa sasa ila ameachiwa Diamond peke yake ndio maana tukipata challenge kwa watu tunaoona wakubwa tunatetemeka sana Diamond amefanya kolabo na Waje, Iyanya, Bracket, KCee, Mafikizolo , Don Jazzy na zingine zinakuja awa wote walimfata hii ni kuonyesha ni kiasi gani wanatambua nguvu yake East Africa na umuhimu wa kupenya EA. SKY na wenzako msiwe wanyonge wabongo tunaweza kura za BBA na Ch O zinamaana kubwa ukizisoma haswa kwetu watanzania.TUJIAMINI !!

Nimemaliza gazeti langu !!!
 
Diamond mtu wa kawaida.. wala hapaswi kulinganishwa na davido
Tunakosea
 
Diamond mtu wa kawaida.. wala hapaswi kulinganishwa na davido
Tunakosea

Kwani Davido ana nini special saaana cha kushindwa kumlinganisha na Diamond?? wabongo tuache ushamba kuogopa wazungu sawa ila hii ya kutetemekea ata vichwa box wenzetu tunajidharaulisha sana.
 
Kwani Davido ana nini special saaana cha kushindwa kumlinganisha na Diamond?? wabongo tuache ushamba kuogopa wazungu sawa ila hii ya kutetemekea ata vichwa box wenzetu tunajidharaulisha sana.

hapa si swala la uzungu au utaifa , just reality diamond hamfikii davido hata wimbo walioimba wote diamond kafunikwa mbaya
 
Kwani Davido ana nini special saaana cha kushindwa kumlinganisha na Diamond?? wabongo tuache ushamba kuogopa wazungu sawa ila hii ya kutetemekea ata vichwa box wenzetu tunajidharaulisha sana.

Davido sio mzungu..cha kwanza. Pili ana millions of followers ukilinganisha na folowers laki moja wa diamomd twiter. Nne davido tayari amesha break through ila diamond anategemea fadhila za saidi fella na ruge, tano si sahihi kutafuta kiki kupitia davido na kuanza kuwaona wanaijeria hawafai wakati hajiti reginald mengi anajiita chibu dangote aachanw basi na hilo jina...biff za diamond ni yeye na akina wema, batuli, ally nipishe na ali kiba.

Lakini kukosolewa kwa chibu bin laden msikuchukulie kama chuki kuweni na werevu ni katika kumjenga coZ naona mnamtetea kuliko wake zake
 
hapa si swala la uzungu au utaifa , just reality diamond hamfikii davido hata wimbo walioimba wote diamond kafunikwa mbaya

Ni mtazamo wako finyu wa kitanzania,cha nyumbani hakiwezi kukizidi cha wa nje........ndio maana wazungu wanatuibia matrioni kwenye madini tunaona ni haki yao hakitokea mbongo mwenzao apate million katika hiyo zitaundwa kamati na bunge kurushwa live kila chanel....sikushangai.
 
wewe punguani nani kasema Davido mzungu, au wewe kila anaeongea kingreza ni mzungu??

Unasema Diamond sio level hizo wakati tweet moja tu inamsumbua Davido mpaka kesho,kabaki kuandika taarab tu.

Tweet moja hiyo imemuibua mpaka Wizkid from nowhere kaanza kutafuta ushikaji, we punguani unaongea nini.
 
Ujinga mwingine bana eti wizkid anatafuta ushkaji na diamond. dogo unaongea utumbo wa kuku.. ngoja niende kusoma hard news huffington post.. wewe mmatumbi bado hujui kinachoendelea
 
Ujinga mwingine bana eti wizkid anatafuta ushkaji na diamond. dogo unaongea utumbo wa kuku.. ngoja niende kusoma hard news huffington post.. wewe mmatumbi bado hujui kinachoendelea

wewe ni punguani ndio maana mnanunuliwa na wanasiasa...alafu wenyewe mnajionaga conscious na hard news zenu wakati mifuko imewatoboka mnashupaa shingo wenzenu wananeemeka ,umevamia jukwaa nenda kibaruani jukwaa la siasa.
 
Wewe comment zako zilivyo its obvious una viroba vingi kichwani,pili chuki za kike zmekujaa. Sasa km Davido ana followers wengi Kwahiyo nn sasa. Ndo iweje kwa Nasibu. Unaumwa kweli Wewe
 
wewe ni punguani ndio maana mnanunuliwa na wanasiasa...alafu wenyewe mnajionaga conscious na hard news zenu wakati mifuko imewatoboka mnashupaa shingo wenzenu wananeemeka ,umevamia jukwaa nenda kibaruani jukwaa la siasa.

Mkuu huyo achana nae. Anachuki za ndani na anazjua mwenyewe.
 
Sky Walker ni k gani tena,,? anaongeaje u pmbi ka huo.
 
bint una gubu kama ndugu wa mume! bin laden mwanzo mwisho hutaki pita kushoto mbona nyie mna ma hero wenu wakina bush na obama na watu wanajiita obama wa bongo hamsemi kitu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…