mr gentleman
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 3,222
- 4,689
Ishu ya Diamond na Davido imeleta mitazamo tofauti. Kuna ambao wanaona Diamond kamkosea Davido kwa kujibu mapigo na kuna wanaoona Davido kawakosea adabu watanzania kwa ujumla kutokana na tweet zao,haya mawazo ya watu na yote yanapaswa kuheshimiwa. Ila mimi nitaongelea mtazamo wa Sky Walker mwandishi ninaemwelewa sana hapa bongo kwa changamoto zake kwenye
tasnia ya burudani, Sky yeye ameenda mbali kusisitiza kupitia tweets zake na maandiko yake bongo5 kwamba Diamond inabidi ayamalize na Davido kwani bado anamuitaji Davido la sivyo ataluuz kitu. Jamaa ameshupalia sana
pengine ni kwa kuutakia mema muziki wetu ila Sky umekuwa inferior sana kwa hili.
Natofautiana na Sky , kwanza kama kuyamaliza ayamalize vipi? Aombe msamaha au? Kwanza alikuwa anatetea kwamba Davido ametafsiliwa vibaya akumaanisha habari za ushindi wa BBA na CH O ila muendelezo wa tweets zake umeonyesha wazi Davido alimaanisha alichokisema na ameendelea kukisimamia so hapa
inaonyesha ni namna gani anaamini Mtz hawezi kushinda mbele ya mnaija na akishinda basi ni hujuma wamefanyiwa. Hii ni dharau.
Point ya msingi nayotaka kusema ni kwamba anachotaka kuamini SKY na wenye mtazamo kama wake kwamba Diamond bado anamuhitaji sana Davido na kwa namna yoyote hatakiwi kumuudhi mimi nasema hapana,Diamond alimuitaji Davido hapo nyuma na sasa hamuitaji tena kama ni heshima kampa za kutosha sote ni mashaidi ila mtu anapoonyesha dharau unyenyekevu wa kitanzania inabidi tuuweke kando. Fid Q anasema nipe heshima yangu au niichukue kwa nguvu.
Pia wabongo tujiamini tuache tabia ya kupapatikia watu wa nje huu ni ugonjwa wetu mkubwa . Muziki wetu kwa sasa una nguvu sana East na Central Africa ni wasanii wetu tu hawaitumii hii nafasi ila tuna nguvu kubwa kwa sasa ila ameachiwa Diamond peke yake ndio maana tukipata challenge kwa watu tunaoona wakubwa tunatetemeka sana Diamond amefanya kolabo na Waje, Iyanya, Bracket, KCee, Mafikizolo , Don Jazzy na zingine zinakuja awa wote walimfata hii ni kuonyesha ni kiasi gani wanatambua nguvu yake East Africa na umuhimu wa kupenya EA. SKY na wenzako msiwe wanyonge wabongo tunaweza kura za BBA na Ch O zinamaana kubwa ukizisoma haswa kwetu watanzania.TUJIAMINI !!
Nimemaliza gazeti langu !!!