Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Naamini hujauliza swali hapo. Ila naamini kwamba yeye kama mnadhimu wa JESHI anazo taarifa sahihi za kutuambia sisi wenye jeshi letu kuhusu tuhuma za jeshi kutumika kama kichaka cha kupitishia dili zisizo safi.Kaka kuna mengine unayoyajua ya Jenerali Shimbo yamekufanya ufikie kutoa hatia hii ama ni hili la kukemea/kutishia ukombozi wenu tu...
Salaam
Unajua hatutafuti ukombozi wetu bali tunapigania kubadilisha serikali iliyoko madarakani baada ya kushindwa kulinda heshima ya nchi na kufanya mambo ya hovyo hovyo. Kama serikali na idara zake haviheshimu na kuwathamini raia wake ujue hakuna cha kuwaonea haya.
Jeshi ambalo limajifahamu kuwa ni la ulinzi basi halipaswi kuwatishia wale linalowalinda. Hoja yangu ya awali ktk thread fulani ni kwamba, SHIMBO angewaita wanaotoa uchochezi kisha awape hayo maneno yake kisha wangeleta ukaidi ndo angekuja frontier na kuelezea juhudi walizofanya na tishio la kauli hizo. Kwa tamko lake naona jeshi limejivika jukumu la MAHAKAMA kuamua kama kuna uhalali wa ushindi au la!
Kama aliwapa majibu wasingekuja tena hadharani kumuuliza na kutaka maelezo tena. Tatizo lenu wengi ni kwamba, yeyote mwenye fikra sahihi MNAMWONA NI msaliti. NDO MAANA MNAKUMBATIA MAJAMBAZI NA WAHALIFU huku mkisema mnatumia turufu ya kufahamika kwao na kukubalika (kuogopwa) kwao mbele ya jamii.Haya ya Meremeta si walimuuliza katika kamati za bunge na akawapa majibu. Wanashindwa nini kuyasema sasa? By the way hata Msanii anaweza kujibu mwenyewe