Elections 2010 Slaa amtaka Shimbo kueleza zilikokwenda sh bil 155 za Meremeta

Elections 2010 Slaa amtaka Shimbo kueleza zilikokwenda sh bil 155 za Meremeta

Haya ya Meremeta si walimuuliza katika kamati za bunge na akawapa majibu. Wanashindwa nini kuyasema sasa? By the way hata Msanii anaweza kujibu mwenyewe

Tuambie wewe alijibu nini?
 
Shimbo sio mlinzi wa raia,yeye na genge lake wapo kimaslahi zaidi,hiyo ndo tz bwana labda kama dr phd akishinda ndio tuanze upya

Kweli, kama alivyoanza upya Hayati J. K. Nyerere 1964.
 
Defence mechanism ya huyu Shimbo imeback-fire, sasa hata yale yalikuwa yamejificha kizani yanaekwa wazi upenuni..si kafungua pandora box yeye mwenyewe?
 
Kwa mfumo wa jeshi sasa Mnadhimu ndio msemaji wa Jeshi....TIMING MIGHT BE WRONG BUT HE WAS FULFILING HIS DUTY na hilo ni lazima liheshimiwe kama kweli tunataka tujenge taifa makini na lenye kuthamini uwajibikaji...

Mfumo wa JWTZ (Jeshi La Wakur.y.a Tangu Zamani) au mfumo wa Jeshi lipi?

Msemaji wa Jeshi (lenye ukubwa kama letu hapa Tanzania or anywhere in Africa except RSA) HAWEZI kuwa na "RANK" zaidi ya Lt. Col (!)::::
 
pic.jpg


“I want to say that we are under no instruction whatsoever from any quarters geared at ensuring some political party wins the elections.”

Constitution inasema lazima apewe amri kama inavyosema ibara ya 32 (1), (2), (3). Yeye anasema hivi ' while the security forces had nothing to do with the campaigns, they would effectively enforce their peacekeeping role, as provided for in the Constitution'

Source: Africa Review Africa Review - Tanzania warns against poll chaos
 
Geshi letu lilivamiwa pindi Gen. Mbona alipoongoza JWTZ!!! Ameset precedent wengine wanafuata tu!! Hii defence mechanism inaonyesha kujisahau na utamu, unagutushwa na akina Slaa; lazima aje mbogo.

Wao bana wamuachie Said Mwema hiyo ndiyo kazi yake, kwani haja-declare kushindwa ebo!!
 
Akitaka kupinduliwa aanze hizo ngebe za kufanya mizaha na jeshi. Mimi nafikiri, siku Dr. Slaa akiingia madarakani akae nao aone ni namna gani wanaweza kufanya naye kazi bila vikwazo. Lakini akiingia na kutaka kuanza kuwadodosa juu ya wanayofanya au waliyofanya ilahali wao wenyewe ndiyo wanaomlinda, wala hawatamwacha.
Na sisi hatuta waacha. Nguvu ya umma inashinda ya jeshi.

 
Shimbo anahusika pia kwenye sakata la wanajeshi wa kulinda amani sudan waliokuwa Msata, ambapo walitakiwa kulipwa $1200 kwa mwezi kwa kama sikosei figure, badala yake alilazimisha walipwe $800 na taxes juu kwa kisingizio wanajeshi hao ni waajiriwa wa JWTZ na siyo UN. Hiyo ilipelekea wanajeshi wagome mpaka waliokuwa Sudan wakataka kurudi bongo ili waende wenye tamaa.

Will follow on this. Thanks
 
Mradi maalum wa JWTZ! Wanajiandaa kuwa WACHUUZI wa Power-Tiller! shame on THEM!

Jamani si nyie ndio mlikokuwa mkilalamika kwanini Kampuni ya NYUMBU haitumiki kusaidia maendeleo ya taifa. Sasa wakijihusisha katika kutengeneza ama kuwezesha mradi kama huu ambao unamsaidia mtanzania mnayedai kumpigania inakuwa kosa tena????
 
Umefanya vema, kwani omarilyas amesema nimeshindwa kutafuta story nzima wakati preview inatosha. Kama anataka full article anunue mwenyewe.

No wonder mnashabikia watu wanaokusanya "data" jamii forum na kukimbilia kuzilipua bungeni ama katika kampeni.....
 
Nafikiri shule yako ni ndogo kidogo, ungekuwa umekwisha andika papers, usingeuliza swali lako kwenye red kwani reference imejitosheleza kwa wengine kupata full article na kuisoma!

Ni kweli kashule kangu ni kadogo sana ndio maana nawasihi wenye shule kubwa kama wewe mjitahidi kusoma zaidi ya previews kabla hamjafikia kutoa mitazamo yenu. Inaelekea mzee wewe ni mtu wa kuandika papers kwa kutumia our mighty tabloids headlines, previews, preface na hata quotations za anonymous great thinkers wa jamiiforums...With this mentality and u still dare to blame mediocrity ya system yetu.
 
Kaka kwa unavyojua maadili na mfumo wa jeshi unadhani kuwa Shimbo alijiamulia tu kusema aliyoyasema kama wagombea wetu wanavyokuwa majukwaani? Hivi kweli unafikiri Shimbo alijipendekeza tu kwenda kufanya mkutano ule pamoja na wanadhimu wenzake wa majeshi mengine bila ya kuamriwa na CDF? Hivi unadhani Shimbo mpaka ameteuliwa kuwa mnadhimu mkuu katika jeshi letu na akakubalika na wanajeshi wenziwe atakuwa mtu wa hovyo kiasi cha kukurupuka kutoa onyo kali kama lile bila ya kupima madhara yake?

Ndio maana nasmea kuwa kama kuna mtu ana mapungufu yake mengine Jenerali Shimbo ayataje ili tuweze kutumia kama kigezo cha kumhukumu kama wengi wafanyavyo hapa.

Ni kweli katika vyombo vyetu kuna vicheche lakini siamini kuwa kila aliyeko huko ni kicheche. Wapo watu makini, wazalendo na waadilifu ambao hawalali kuhakikisha kuwa mimi na wewe tunaweza angalao kwenda kulala vyumbani mwetu bila ya kuogopa kumwagwa damu zetu. Siasa hizi za kshabiki ambazo ni wazi zina chimbuko linaloeleweka zisitufanye tufuate upepo wa kubomoa kabisa asasi zetu chache ambazo bado zinajitahidi kutekeleza wajibu wake. Na katika hili la Jeshi letu, ni kutulinda na maadui wa ndani na wa nje pamoja na amani ambayo yeweza kuwa si timilifu lakini inayotuwezesha kujenga mazingira ya kufikia amani timilifu tunayopaswa kuwa nayo.


Again kama kuna mapungufu ama maovu yanayomhusu moja kwa moja jenerali Shimbo basi yataje ili nasi tufungue macho zaidi...
Kwa yeye SHIMBO kuja mbele kutoa maneno ambayo yana tafsiri ya VITISHO ndo imetufanya tuzame ndani zaidi kumchambua. Ila naona wewe unasisitiza tutaje madhaifu yake mengine. naamnini kama kuna mwenye maishu yake atayamwaga hapa ila kwa sasa tunajadili usafi wake mbele ya umma na nafasi yake kama kioo. Kama anatajwa katika maskandali fulani fulani basi anapaswa sana kuwa mwerevu kwa kila hatua anayopiga.

Kuhusu jeshi letu. Mimi kwa mtazamo wangu naona hawa makamanda wetu wanapaswa kubalidika liwe jeshi la uwekezaji zaidi ya kusubiri amri. Wawekeze kwenye sayansi na teknolojia, uchumi na tafiti za kilimo ili tujue tunalindwa nyanja zote. najua wewe umeshapitiapitia FACEBOOK, unajua imewekezwa na nani? Wakubali kuajiri wataalam ambao watakuwa na tija kwa jeshi na taifa na sio kuajiri elimuless kama inavyofanya sasa. Let our army procure first class employees. Hapo ndipo inapokuja suala la kuibadilisha serikali iliyopo sasa maana wamewekeza kwenye siasa ndo maana viongozi wetu wengi ni wanajeshi watsaafu.
 
No wonder mnashabikia watu wanaokusanya "data" jamii forum na kukimbilia kuzilipua bungeni ama katika kampeni.....
Naona umeanza kufanya assumption sasa na unafanya kazi yako vyema kuisemea serikali humu. nakupa kudos.
Ila una uhakika kwamba milipuko yote ya bungeni chanzo chake ni JF? kama ndivyo basi JF imefanya kazi kubwa ya kizalendo kuweka data za ukweli na uhakika ambazo zimetumika kuiletea heshima serikali.
Amen
 
Lt Gen Shimbo ni mteule wa JK sio wa Rais. Atafanya kila lililo ndani ya uwezo wake kuhakikisha JK anabaki madarakani. Lt Gen Shimbo hakustahili kuwa CoS wa jeshi letu. Ni hii sera isiyo rasmi ya CCM na JK wake ya kupanga safu za uongozi wa Nchi na vyombo vyake Kikristo na Kiislamu.
 
Back
Top Bottom