Mkuu Hagonga,Dr Slaa alikuwa anazijua Tuhuma hizi,Lakini hapakuwa na nafasi ya kuzisema,Lt.Gen Shimbo alipokosea kutamka aliyoyasema kuhusu matokeo ya Uchaguzi ndio ikabidi Dr Slaa amrudie na kuweka wazi maovu yake....Dr Slaa anajua mengi kuhusu Watendaji hawa wa Serikali ya Kikwete kuliko unavyofikiri.
Hali iliyopo sasa sio katika Jeshi tu bali hata katika Taasisi nyingine za Serikali,Walioaminiwa kupewa dhamana wamekuwa wanatumia nafasi hizo kujinufaisha kuliko kuihudumia Jamii.Ndio Tatizo la kuwapa Wafanyabiashara dhamana ya kuongoza Jamii.Lt.General Shimbo kama ilivyo kwa Mkuu wa majeshi (CDF) Kwa Taaluma ni Makachero Jeshini,na bila uoga naweza kusema hali hii ya kuwa Wafanyabiashara zaidi walijifunza kutoka kwa CDF Mstaafu Mboma.Uzalendo wa kuitumikia Jamii umeondoka miongoni kwa Watendaji wengi wa Umma.
Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka mikoa ya Mbeya,Iringa,Morogoro na hata Dodoma kuwa Matrekta hayo madogo (Power Tillers) yapo kwenye viwango dahaifu,na mara nyingi yanashindwa kufanya kazi sawasawa kutokana na ugumu wa ardhi,kumekuwa na malalamiko kutoka Wilaya ya Mbalali ambako wameagiza matrekta hayo zaidi ya 850,ambayo huuzwa kwa wakulima kwa kiwango cha Tshs 4m mpaka 6m.
Imefika wakati sasa tuseme "NO" kwa Wafanya biashara waliojipenyeza kunyonya wananchi maskini kwa kofia ya Uongozi.