Elections 2010 Slaa amtaka Shimbo kueleza zilikokwenda sh bil 155 za Meremeta

Tamko lilitolewa na Shimbo la kututishia watanzania haliwezi kuachwa lipite hivihivi na waitakiao amani nchi yetu.

Sitaki kuamini kuwa Shimbo hana ufahamu wa kutosha kuelewa kuwa kuna watu wenye ufahamu mkubwa wa kuelewa mambo kwa kusoma hata katikati ya mistari!

Tofauti na wanavyotaka tuamini kuwa JW na polisi wanajali sana amani ya tanzania katika kipindi hiki cha uchaguzi; tamko lao linaonyesha, kwa uwazi mkubwa sana, lengo lililokusudiwa na wakubwa hawa. Hakuna jingine ni kutaka kuisadia chama wanachukitumikia, ingawa wanadai wao si wanachama wa chama chochote kwa mujibu wa kazi zao na bosi wao mkuu kuendelea kushika madaraka ya nchi kwa gharama yoyote ile!

Ni ukweli uliowazi kuwa katika chaguzi mbalimbali na hasa ambazo zina ushindani kama huu wa sasa kunaweza kutokea mambo yafuatayo; kwanza ni lazima mshindi apatikane, pili, kama ukuchaguzi ni huru na / au wa haki basi mshindi atapatikana kwa halali na tatu, kama uchaguzi si huru na si wa haki basi mshindi anweza kupatikana isivyo halali na hapa ndiyo tatizo litakapoanzia kwani umma utataka kudai haki yao.

Umma wa watanzania ni pamoja na wafanyakazi, wakulima, wasio na kazi, wanajeshi wa JW, polisi, magereza na wengine wote ili mradi ni raia halali wa tanzania wakubwa kwa wadogo, wazee kwa vijana, wanaume kwa wanawake.

Shimbo anaposema lazima matokeo yakubaliwe kuna walakini. Matokeo yanayokubalika ni yale to yakiyo halali. Nilitegemea Shimbo asema LAZIMA MATOKEO HALALI YAKUBALIWE NA KUHESHIMIWA. Haiwezekani umma wa watanzania wakubali matokeo yoyote yale hata kama yamechakachuliwa eti tu kwa sababu shimbo ametishia kwa tamko lake!

Hakika hatutaki kumwaga damu lakini kama haki yetu itapatikana kwa kumwaga damu basi hatuna budi kuimwaga.

kwa kutokujua ama kujisahau, pengine kwa sababu ya maisha bora aliyonayo yeye, hafikirii kuwa hata wanajeshi anaotutishia nao, wale askari wa kawaida kabisa, wavuja jasho, wachovu, wanaodai maisha bora na mishahara mizuri, wanaolala kwenye mahanga na mahema watakuwa pia wanadai haki yao, wanaweza wakawa ni sehemu ya umma utakaokuwa umeporwa haki yao (kama ikitokea haki imeporwa) na hivyo wakawa upande wa kudai haki yao ndiyo maana nasema nguvu ya umma ni kubwa kuliko tamko la Shimbo.

Ni jambo la ajabu sana kwamba chaguzi zinazohusisha vyama vingi zimefanyika mara tatu katika nchi yetu, hakukuwa na vitisho vya akina Shimbo, uchaguzi wa mwaka huu una nini cha ziada kilichomkurupusha Shimbo kutoa tamko ‘biased' kama alilolitoa? Kwa mtu makini anayechunguza mwenedo wa kampeni ataona kuwa ‘pepo ni za kusi na jahazi la anachokitumikia linaelekea kaskazi na bahari imechafuka ni ya mawimbi makubwa'.

NGUVU YA UMMA NI KUBWA KULIKO TAMKO LA SHIMBO.
 
Huyu Askari si akubali tu kwamba alilikoroga halafu akae pembeni (ajiuzulu) ili kulisafisha jeshi?
 
Jamani, hawa watu hawajui kusoma historia hata ile ya hivi karibuni.

Mnakumbuka raisi Suharto wa Indonesia aliachia vipi madaraka? Yule wa Romania je? Pamoja na majeshi yote yenye nguvu, pia wao ni wahanga wa mfumo uliozoeleka wa CCM.

Safari hii tusiogope tena
 

Source yako ni ipi? Au basi tuweke hio kauli ya FemACT! But whatever the case, this is the right move, I hope other societies will pick it up. Ningefurahi sana Workers Unions kama THTU, TUCTA, TUGHE, RAAWU nao wangekemea! Bila hivyo hawa JWTZ wanaitwa wapiganaji na wanapokaa siku nyingi bila kuzipiga au kupigwa inawawia vigumu sana. Inabidi kuwakemea. Tungekuwa na Ombudsman nchini angetusaidia kazi hii.
 

Hapana kabisa Nd Africana. Lugha uliyotumia si ya kistaarabu hata kidogo!!! Si ya busara na wala haiwezi kuwekwa kwenye kipimo kimoja na hao unaowashabikia hapa. Ujumbe wako ni mwepesi na wa haraka kudakwa, hukuwa na haja ya kutumia maneno haya mazito! Tena unaonekana mcha Mungu, lakini huwezi ukatumia such a vulgar language for a good cause. Please stop it!!!!! Sidhani kama hapa ni pake, na Mod nisamehe kama nimeingilia kazi yako
 
mbona tbc wamesema kinyume chake au wameichakachu?

Ndugu yangu, usiyajali hayo. LEO TAARIFA YA HABARI HAWAKUONYESHA PICHA ZA MIKUTANO YA DR SLAA. Waliweka sauti tu ya mtangazaji wao wakati kampeni za Lipumba zilionyeshwa picha. Nafikiri ni mkakati wao wa kutowaonyesha WaTZ mikutano yake inavyojaa. Nasikia kule Sumbawanga maduka yalifungwa kila mtu akaenda kumsikiliza Slaa.
 

I agree 100%
 
Heri haya yaongelewe bungeni lakini sio kwenye majukwaa ya siasa... Slaa is not doing good for this nation.

Nenda kamwambie Shimbo hayo, kumbuka "Every Action has an Equal and Opposite Reaction"
SHIMBO kalileta kisiasa kikampeni atajibiwa kikampeni anatakiwa ajue hilo na yeyote ajue hilo. RO (UWT) yeye kaamua kutulia haji kwenye media. Shimbo kajiona yuko juu ya Vichwa vya watanzania. Sisi ndio wanajeshi, sisi ndio tunashika silaha, sisi ndio tunalipwa masimbi halafu wanataka kulianzisha kwa vitenda vyao uchwara , tumegoma.

Moto kwenda mbele wakimwaga ugali, mboga zitamwagwa mpaka kieleweke.
 
Jana niliwasikia watetezi wa haki za binadamu wakina nkya, kiwanga na wangineo wakiongelea kauli ya shimbo kwa niaba jwtz, wametoa hisia zao kuhusu ile kauli.ni kweli kuwa jeshi limechemka kwa kutoa vitisho wakati hakuna dalili zozote za uvamiaji wa mipaka yetu na kampeni zinaendeshwa kawa amani kabisaaa, na wao kazi yao sio usalama wa raia ni ulinzi wa mipaka yetu, kwa hili wameingilia kazi ya polisi wetu.

Mi napata wasiwasi kuona kuwa ccm wanajiandaa kuchukua nchi kwa nguvu hata kama wameshindwa kwenye uchaguzi ujao.

Tulishapata habari kuwa katika watumishi waliolipwa mishahara mipya ya tsh 235,000/= ni jwtz kwa matiki kuwa wawe upande wa serikali ya ccm na kwa kauli ile inadhihilisha kuwa wamewekewa maslahi yao yawe bora ili waweze kuwatisha wananchi wachague ccm kwa lazima kuepuka vita isiyopo.

Nakumbuka mahita nae alisema amekamata visu vyenye nembo ya cuf 2005 kumbe si kweli na ikafanya cuf iliyokuwa na nguvu mwaka ule ikakosa support.

Watanzania si wajinga wanaona na kuelewa na hawatishwi na hizo kauli kwani wanjua wajibu wao na kiongozi wao wamtakae, tunamtaka shimbo afute kauli yake na kujiuzuru kwani imejaa uvunjifu wa haki za binadamu na kukipendelea chama cha ccm dhahiri kabisa.

Peoplesssssssssssss powerrrrrrr, kutuua watuue ila hatutaacha kutetea na kupigania haki zetu za kikatiba na pia kuwang'oa mafisadi madarakani.
 
Nilisoma mahala fulani kuwa Shimbo anahusika na deal ya power tillers. hebu soma impact ya hiyo deal hapa....
 
Hivi jamii forums huwa wanafuta posts zingine? Nilipost sababu kumi kwa nini kikwete amelaaniwa na kwa mshangao wangu imefutwa haipo!!!! Nini maana ya kutoa mawazo kwa uhuru au na wao wamenunuliwa?
 
Leo asubuhi clouds wamepiga wimbo wa jakaya kikwete kwa ajili ya birthday yake. Lakini sehemu kubwa ya wimbo ni kampeni badala ya birthday. Nilikuwa nawaamini gerald na babra lakini leo nimewaona hovyo!!! Acheni unafki!!
 

Naungana na wewe. hasira si nzuri. JK ana mazuri na mabaya, kama binadamu wote walivyo. Si vizuri kumwombea kifo wala wale wa Redet. Tunahitaji mawazo mbadala, si kulipizana kisasi. Mambo ya kisasi ndo yameifikisha CCM hapa. Naamini kama JK angekuwa na uhusiano mzuri na watangulizi wake, asingefikia hatua hii. Sidahni kama watu kama Mwinyi, Mkapa, Saklmu nk wangesimama pamoja kwenye kampeni za JK CCM ingefikia hali hii.....
Tuepuke visasi!
 

Umemsahau Rais Musharaff wa Pakistan, alinywea mwenyewe na sasa anaishi Uingereza/ Achanan na mbinyo wa Wenyenchi, nchii ni yetu sote!
 
Shimbooo, uliyaanzaje haya ukijua kuwa ni mchafu kiasi hicho?? hufai hata kuwa mgambo sasa...
 

I truly respect Mama Nkya lakini hapa nadhani amefanya kosa kama alilofanya jenerali Shimbo. Mama Nkya hawez kuwa objective when it come to maslahi ya CHADEMA na pia Dr Slaa. Angewaachia kina .....pekee waongee. Soon mtajua kwanini nalisema hili.....

Lakini pia kwa nini walitilia mkazo suala la kukubali matokeo tu bila kugusia suala la kauli za DAMU ITAMWAGIKA???
Pia kati ya hao wanaopaswa kukubali matokeo tunaona dalili zotezote kwa upande wao ama wa CHADEMA kuwaandaa wanachama wake kukubali matokeo ama vice versa??? Tayari kila siku mazingira yanajengwa ya kuaminisha watu kuwa CHADEMA watashindwa tu kutokana na hujuma za CCM, Usalama wa Taifa na sasa wameliingiza Jeshi na si vinginevyo.....

And we expect vyombo vyetu vyenye jukumu la kulinda usalama wa nchi yetu kutokana na maadui wa nje na wa ndani wanyamaze hadi damu ianze kumwagika halafu ndio waanze kutekeleza jukumu lao?

FemACT walipaswa kuanza na Arusha mjini ambako kuna mgombea wanamnyanyapaa eti kwa kuwa mwanamke, mjamzito, ameolewa na Mzanzibari na kashfa nyingine kibao za kijinsia. Lakini wamenyamaza kimya mradi tu yeye wanamuona si mwenzao???
 
Shimbo!................Mini niliwaza na kujiuliza sana, kama hii ishu ni ya kweli unakoelekea siko mtu wangu!
 
Jamani huyu Shimbo kwani alisemaje? manake naona amelikanyaga akidhani watu wanaogopa manyota yao
 
JWTZ WANAMAANISHA NINI? HAKUNA HAJA YA WA TZ KUPIGA KURA AU...?


KWANZA, JE HILI LILIKUWA TAMKO LA JWTZ AU LA SHIMBO? JWTZ AMBAO TUNAWAHESHIMU HIVI WANAWEZA KUCHIMBA WATU MKWARA WA KIPUUZI KIASI HIKI? NILIKUWA SIJUI KUWA SHIMBO NI KIMEO KAMA MAKAMBA! USWAHILINI MAKAMBA TWAMWITA msukule wa ccm, NA SHIMBO AMEINGIA KWENYE ORODHA YA WATZ VIMEO TULIONAO. JE, NAYE AITWE MSUKULE AU NDONDOCHA WA JESHI?

SWALI LA KUJIULIZA:

JE, KWANINI HASA KINA SHIMBO WAMEKURUPUKA NA KUROPOKA VILE KWENYE VYOMBO VYA HABARI WAKATI NCHI IPO SALAMA NA KAMPENI BADO ZINAFANYIKA KWA AMANI NA UTULIVU WA HALI YA JUU KUPITA MIAKA YOTE? JE, POLISI WAMESHINDWA KAZI HADI JWTZ WAINGILIE KAZI ZA POLISI?, TAASISI ZOTE ZA SERIKALI ZINA HAKI SAWA LAKINI HAWA JAMAA WANALIDHARAU JESHI LA POLISI KWA KUWAPIGA MAKOFI MATRAFIKI NA KUINGILIA KAZI ZA POLISI KAMA WANAVYOTAKA KUFANYA SASA! JE, KUNA HALI GANI YA HATARI WALIOIONA KINA SHIMBO HADI WAROPOKE HAYO YOTE?

JIBU HILI NI SAHIHI KABISA KWA MASWAI HAYO ILA WATZ WENGI HAWALIJUI HILO:
CCM NA SERIKALI YAKE WALIKUWA HAWATEGEMEI KTK UCHAGUZI HUU DR. SLAA ATASIMAMA KUGOMBEA URAIS. WALIFIKIRI CHADEMA WATAMSIMAMISHA MGOMBEA AMBAYE CCM INGEMBWAGA KIRAHISI. KITENDO CHA DR. SLAA KUKUBALIKA KWA KARIBU 74% YA WATZ KIMEWATIA KIWEWE CCM, WAMECHANGANYIKIWA, NA WAMEONA WAZI KUWA DR. SLAA TAYARI AMESHINDA NA ANASUBIRI OCTOBER 31 IPITE AAPISHWE! MAJI YAMEWAFIKA SHINGONI, KIZA KIMETANDA HAWAJUI KUSI, KASI WALA MASHARIKI! WAMEKIMBILIA JESHINI KUOMBA MSAADA!!! NA HII NDIO MAANA WAMEKUWA, TANGU AWALI WANASISITIZA KUWA IJE MVUA LIJE JUA USHINDI KWAO NI LAZIMA! HII KAULI YA CCM KUSHINDA KWA LAZIMA IMEKUWA IKIWASHANGAZA WATU WENGI KWANI KILA MMOJA WETU ANAFAHAMU FIKA KUWA WATZ HAWAITAKI CCM SASA HUO USHINDI WANAODAI WATAUPATA WATAUPATAJE?
WALIJIGAMBA KUSHINDA KUMBE SI KWA KURA BALI KWA NGUVU YA JWTZ!!

NDUGU ZANGU MSIOFAHAMU BAADA YA KURA KUPIGWA, HATA KAMA DR. SLAA ATASHINDA UCHAGUZI HUU, SHIMBO NA WENZAKE WATAMWAMURU JAJI MAKAME KUMTANGAZA KIWETE WAO KUWA MSHINDI NA NDIO MAANA JWTZ IMEMWAMBIA DR.SLAA AFUNGE MDOMO BAADA YA JAJI MAKAME KUTANGAZA MSHINDI AMBAYE JWTZ WANAMTAKA!!

KWA MAANA HIYO BASI, JWTZ INAWAAMBIA WATZ KUWA HAKUNA SABABU YA KUPIGA KURA KWANI HATA DR. SLAA AKISHINDA JAJI MAKAME HATAMTANGAZA MSHINDI NA DR. SLAA HATARUHUSIWA KUHOJI LOLOTE!!

KWA TAARIFA ZENU HUU SI UCHAGUZI WA DR. SLAA NI UCHAGUZI WA WATANZANIA. KAMA SHIMBO ATAMZUIA DR.SLAA KUKATAA MATOKEO BASI WATANZANIA TUTAYAKATAA TUONE SHIMBO ATATUFANYA NINI. KWA TAARIFA YAKO, USIDHANI KUMILIKI VIFARU NDIO UJANJA, GOMA LIKISANUKA HATA WEWE SHIMBO NA NDUGU ZAKO WOTE HAMTABAKI SALAMA. TENA ITABIDI MAHAKAMA YA THE HAGUE IKAE CHONJO KUKUSHUGHULIKIA ENDAPO UTALETA VURUGU NCHINI. HUU SI MUDA WA KUTISHIA WAKUBWA WENZAKO NYAU, KAMA NYIE WANAUME KWELI, BASI IBENI KURA OKTOBA 31 MUONE! CCM ENDELEENI KUIBIANA KURA ZENU KWENYE KURA ZA MAONI LAKINI SI KUIBA KURA ZA WATANZANIA. MAKAMBA ANAWALAZIMISHA WANA CCM KUWAKUBALI WABUNGE WASIO CHAGUO LAO NA JWTZ ITUCHAGULIE RAIS?! THUBUTU!


MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU MBARIKI RAIS WETU DR. WILBROAD PETER SLAA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…