Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 239
Mgombea urais kupitia Chama cha Maendeleo na Demokrasia, Dk wilbrod Slaa amerusha kombora kwa mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulrahman Shimbo, kumtaka awaeleze Watanzania zilikoenda Sh Bilioni 155, zilizopotea katika mradi wa kampuni ya kuchimba dhahabu ya Meremeta ambao unadaiwa ni mali ya jeshi hilo.
Alisema hatoogopa vitisho na yuko tayari hata kuuawa kwa kupigwa risasi ili mradi haki itendeke na kumtaka Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi Tanzania, (JWTZ), Luteni Jenerali Abdulrahaman Shimbo, kuwaeleza Watanzania zilikoenda sh bil. 155, zilizopotea katika mradi wa kampuni ya kuchimba dhahabu ya Meremeta.
Dk. Slaa alimtaka jenerali huyo wa jeshi kuwatendea haki Watanzania kwa kueleza ukweli namna fedha hizo zilizogunduliwa na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) zilivyotumika, waliohusika na wizi huo na hatua zilizochukuliwa dhidi yao.
Alibainisha kuwa CAG, alitoa taarifa ya wizi huo bungeni na wala si maneno ya kuokoteza mtaani au yake (Slaa) ambapo sh bil. 155 zilipotea baada ya kuibiwa katika mgodi wa dhahabu wa Buhemba.
"Nampa changamoto Jenerali Shimbo aeleze zimeenda wapi…wizi ni wizi tu hata kama umetokea jeshini, Watanzania ambao ndio walipa kodi wanayo haki ya kujua fedha hizo zilikoenda na hatua zilizochukuliwa dhidi ya wahusika," alisema.
Mgombea huyo alisema siyo kweli kuwa kutoa taarifa ya upotevu huo ni kuingilia siri za jeshi kwani Watanzania hawataki kujua masuala yanayohusu medani za kivita kama vile idadi na aina ya vifaru, mizinga, bunduki, mabomu wala ndege za kijeshi na uwezo wa JWTZ.
Alibainisha wanachotaka kujua ni wahusika walivyofanikiwa kuchota mabilioni hayo ambayo mpaka hivi sasa serikali imekuwa ikiupotosha umma juu ya matumizi yake kwa madai ni siri ya jeshi.
Katika hatua nyingine, Dk. Slaa, amewataka wakazi wa wilaya ya Kyela kutumia demokrasia kumchagua mgombea urais, ubunge na udiwani wanayemtaka.
Alisema iwapo wakazi hao wanataka kumpa ubunge mgombea wa CCM, Dk. Harrison Mwakyembe, yeye (Slaa) hana tatizo ili mradi kura za urais wampe kama wanavyomuaidi.
Alisema iwapo Dk. Mwakyembe atachaguliwa ni vyema wakamweleza kuwa mambo ya CCM yaishie nje na siyo bungeni kwa kuwa serikali yake itakuwa na wabunge wengi wa upinzani.
"Kama mtamchagua Dk. Mwakyembe na mimi nikawa Rais wake tutafanya kazi vizuri sana kwa kuwa wote tunapingana na mafisadi," alisema Dk. Slaa.
Chanzo: Tanzania Daima