Elections 2010 Slaa aunguruma Mwembeyanga, LIVE TBC1

Elections 2010 Slaa aunguruma Mwembeyanga, LIVE TBC1

Asante Atigi kwa picha. Tuongezee muhtasari wa hotuba kama inawezekana.

Taifa letu liko tayari kufanya Historia. Historia ya kubadilisha chama tawala kwa mara ya kwanza. Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki kiongozi wetu mpendwa Dr. Slaa.
 
Safi sana Atigi maana mi nkifkiri hajafika upande huo' na mi ngoja nizipeleke maeneo zaidi wadau wazione!!
 
big up dakta slaa, we gona reach the appex of citizens' desire, which results to the death of ccm.
 
atigi, big up kwa picha jjapo suna tu. Maaskofu na Masheikh mbona hawasemi hili ni chaguo la Mungu au wanamuogopa makamba?
anyway, kazi inaonekana na nia pia imedhihiri. tunasubiri kuona ccm wakiwa bench wanafanya nini.
 
ikiwa huku ni 'kuteka', kule kunakofanywa na ccm na cuf zanzibar tutakuita 'kupindua' au?
 
My take: Kwanini huu mkutano waDr Slaa kuaga Dar es salaam usingefanyika jangwani?
Siujui vizuri huu uwanja wa Mwembeyanga lakini sidhani kama ni mkubwa kama wa jagwani.

Wenye kuujua watuhabarishe na maandalizi yanakwendaje?
 
Mambo ya Zenji

2qvb4nd.jpg

2uh3eki.jpg

16kdnj4.jpg

Vipi Habarii imekaaje?

MGOMBEA Urais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chadema, Dk Wilbrod Slaam, amesema ubinafsi wa viongozi wa Serikali ya CCM, umekwamisha uchimbaji wa mafuta katika visiwa vya Zanzibar.
Kwa mujibu wa Dk Slaam, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), liliwahi kuwasilisha bungeni, sampuli ya mafuta yaliyotafitiwa katika visiwa vya Zanzibar.
Alisema hata hivyo Serikali ya CCM haijachukua hatua kuchimba mafuta hayo na kwamba hiyo inatokana na ubinafsi wa viongozi wa CCM.
“Viongozi wa Serikali ya CCM, wameshindwa kuchimba mafuta yaliyoko Zanzibar kwa sababu ya ubinafsi wao wakihofu kuwa yatachukuliwa,” alisema Dk Slaam alipokuwa akizungumza katika mkutano wake wa kampeni, uliofanyika katika Jimbo la Mtoni katika Wilaya ya Mjini Magharibi.
Alisema hata hivyo kama atachaguliwa katika uchaguzi mkuu unatorajiwa kufanyika Jumapili ijayo, serikali atakayoiunda, itahakikisha kuwa mafuta ya Zanzibar, yanachimbwa.
“Mafuta ya Zanzibar yatachimbwa na hayatakuwa katika mambo yaliyoko katika orodha ya Muungano na badala yake, yatatumika kuendeleza Zanzibar, kama ilivyo kwa gesi inayopatikana Mtwara, ambayo inatumika kuinufaisha Tanzania bara pekee,” alisema Dk Slaa
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na idadi ndogo ya watu ikilinganishwa na mikutano mingine ambayo mgombea huyo amekuwa akikusanya umati mkubwa wa watu, alisema akichaguliwa pia ataimarisha Muungano.
Alisema yeye ni mmoja wa waumini wakubwa wa Muungano na kwa hiyo atauimarisha lakini ukiwa na mfumo wa serikali tatu na si serikali mbili kama ulivyo sasa.
Hali kadhalika alisema kama atachaguliwa, atachukua hatua za kuunda upya katiba ya Jamhuri ya .Muungano wa Tanzania na ile ya Zanzibar, ili zikidhi matakwa ya wananchi.
Dk Slaa alisema katiba hizo zitaundwa kwa kuwashirikisha wananchi ambao ndiyo wadau wakubwa.
“Katiba zilizopo sasa hazina sifa ya kuitwa katiba za wananchi kwa sababu hazikuwashirikisha wananchi. Tutaunda katiba zitakazotokana na mapendekezo na maoni ya wananchi,” alisema mgombea huyo.
Dk Slaa pia alisema serikali atakayoiunda kama atachaguliwa, itahakikisha kuwa rasimali za Zanzibar zitatumika kikamilifu
ili kuvifanya visiwa hivyo kuwa lulu na dhahabu.
“Zanzibar ni lulu na dhahabu ambayo hata hivyo haijatumika na hii ni kwa sababu, rasilimali zake haijatumika kikamilifu na kuifanya ipige hatua kubwa za kimaendeleo,” alisisitiza.
 
Isingekuwa neema ya mawasiliano basi tungedanganywa sana.

Eti Slaa aiteka Zanzibar! Mbona watu ni wachache hivyo.

Nikiingalia hiyo picha naona waandishi wawili wa habari wakiwa wamekaa chini. Karibu kabisa na dkt.Slaa ambaye amezibiwa na doti za kanga zilizofungwa na kamba ya katani.

Dkt Slaa mwenyewe amesimama kwenye kitu kifupi kama si stuli basi ni jiwe.Hakupata waandalizi,vyenginevyo hawakuona haja hiyo kwa vile mpaka dakika za mwisho hakukuwa na dalili za kupatikana wasikilizaji.

Ufupi wa mambo ni kuwa dkt.Slaa kaisha kabisa.Nikisema hivyo ni katika kila hali hata ya kiafya.

Kutokana na fani yangu naweza kusema kuwa dkt.Slaa ana tatizo la hypertension.Kampeni ziishe akapumzike kabla hajaanguka kwenye majukwaa.
 
ndugu mimi nilikuwa maeneo ya tukio,kwa nature ya zanzibar slaa alipata watu wengi sana kupita hata wale wa jk karatu ambao hata hivyo walibebwa kutoka ktk majimbo mengine kuficha haibu.kuhusu kuanguka kaka hapo utakuwa unamkashifu jk kwan yeye ndio mwenye ugonjwa wa kuanguka..usiwe na jazba ya siasa kaka.kama iko,iko tu.
 
Kuanguka ni tatizo la kiafya ambalo dkt Slaa analo sawa na mwenzake-Kikwete.Katika hali kama hii ni ushauri mzuri kuwa muda wa kupumzika umefika.

Katika tukiio la kampeni la Zanzibar ni wazi kuwa wapambe wa dkt.Slaa walitaka kuudanganya umma.Eti mpiga picha wake hakuwepo hivyo watu wasingeweza kuona picha za tukio hilo.Walisahau kuwa enzi hizi uchukuaji picha hufanywa na hata watoto wadogo katika ubora wa hali ya juu kwa kutumia simu tu.Yawezekana hawa wapambe wamekuwa wakifanya ubabaishaji aina hiyo maeneo mengine.
 
ANGALIZO: TBC wasije wakafanya mchezo mchafu kama waliyoyafanya Jangwani maana this time around it will cost them even more
 
Heko Dr.SLAA.kwa kufika Zenji,safari hii hatudanganyiki.chadema hoyeeeee!chimbua kila mahali tunataka badiliko.kuna mpuuzi nimemsikia anadai bilioni tatu!!! Eti kachafuliwa kawe jana,ha ha hai hai!
 
Kichuguu
Huwezi kutegemea nyomi la kufa mtu kwenye mikutano ya Slaa Zenj. Lakini huo umati unatia moyo. Ni watu wengi hao. Hata channel ya CCM, yaani TBC walionyesha watu wengi tena wenye hamasa.

Kura za Slaa zipo huko Zenj.
 
OK Mzee Slaa kamilisha kila kitu leo hapo Mwembeyanga kwani ndio kitovu
cha ukombozi wa WaTz kuwajua mafisadi na vilevile ndio kitakuwa kitovu
cha mageuzi kwa wananchi kuweka uongozi mpya Nchini Tanzania.
Kila KHERI Dr.Slaa.
 
Ss sijajua kampeni zitaanza sa ngapi!! Lkn vyovyote vile lazima niwepo pale, the finest ondoa shaka kuhusu kiwanja, kiwanja ni kikubwa, ufanyefanye kazi zako twende tukamsikilize rais wetu mtarajiwa.
 
Ss sijajua kampeni zitaanza sa ngapi!! Lkn vyovyote vile lazima niwepo pale, the finest ondoa shaka kuhusu kiwanja, kiwanja ni kikubwa, ufanyefanye kazi zako twende tukamsikilize rais wetu mtarajiwa.
i miss you suzane
 
Back
Top Bottom