GeniusBrain
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 4,315
- 309
- Thread starter
- #61
Inflation simply is too much money chasing a few goods. Yaani pesa nyingi kwenye mzunguko wakati uzalishaji ni mdogo. Hivyo mwenye fedha analazimika kununua kwa bei ya juu kwa sababu bidhaa ni kidogo.
Sasa sababu za kuwa na fedha nyingi kwenye mzunguko ziko nyingi. Mtoa hoja anataka kutuaminisha kuwa ajira imeongezeka na hivyo kusababisha kuwepo kwa fedha nyingi lakini hajiulizi hawa walioajiri wanawalipa kutoka wapi iwapo uzalishaji hakuna? Kwa mwajiri yeyote aliye makini hawezi kuajiri wakati uzalishaji hakuna, hivyo kuongezeka kwa ajira hakuwezi kusababisha inflation. Kwa Tanzania uzalishaji mdogo umesababishwa na tatizo la umeme, ufisadi (fedha ambazo zingewekezwa zimeliwa na chombo husika (BoT) kushindwa kutumia monetary measures ku-control inflation.
Tatizo la ufisadi ni kubwa kwani limesababisha ajira kutokwenda sambamba na labour-force. Mafisadi wanawekeza nje hivyo ajira zinatengenezwa nje, kodi kidogo inayokusanywa kwenye migodi inasababishwa na 10% ambayo wakubwa wanaiwekeza huko huko nje - je ajira local zitatoka wapi? Viwanda tulivyobinafsisha vingi havizalishi tena, mashine ziling'olewa na kupelekwa nje hivyo kutengeneza ajira nje na kudumaza ajira za ndani - haya yote yansababisha uzalishaji mdogo.
Hivyo mkuu anayesema ajira zimeongezeka kiasi cha kusababisha inflation has to think twice!
Hoja zako zime base kwenye ajira ambayo ni rasmi, kumbuka definition ya ajira ni kubwa zaidi ya hiyo unayoifikiria, wewe umeji confine kwenye very narrow definition of employment