Sleeper Agent: Mbinu ya kupandikiza jasusi mahali atakayetumika siku za baadaye

Sleeper Agent: Mbinu ya kupandikiza jasusi mahali atakayetumika siku za baadaye

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506
Sleeper agent au sleeper cell ni jasusi anayepandikizwa katika nchi fulani au taasisi fulani nyeti kwa ajili ya kufanya upelelezi siku za baadaye, au damage fulani mara atakapotakiwa kuanza upelelezi wake.

Majasusi hawa mara nyingi huwa wanapewa sharti moja la kutokujihusisha na ishu zozote za kijasusi kwa kipindi kirefu hata miaka 20 au 30, huku wakiendelea na maisha yao ya kawaida kama raia mwingine mtiifu wa nchi/organization hiyo.

Sekta ambazo mara nyingi hutumiwa sana kupandikiza majasusi wa namna hii ni kwenye dini, wafanya biashara wakubwa, vikundi vya kigaidi, viongozi wa kisiasa, international scholarships na sekta nyingine ambazo zinahitaji mtu kukaa muda mrefu na kuaminika kabla ya kupanda ngazi(cheo).

Mbinu mpya ambayo inatumiwa kwa sasa kupambana na ugaidi wa kimataifa ni ku-infillitrate hawa ma sleeper agents wengi kwenye vikundi vya kigaidi ambao huendelea kuwa magaidi kama magaidi wengine kwa kipindi kirefu hata miaka 10 bila ya kujulikana wala kufanya kazi yoyote ya kijasusi huku wakipanda ngazi za vyeo na kuzidi ku-gain trust, lakini pindi muda wao ukifika wa kuanza kazi huanza kuvujisha siri kama kawaida kwa mabosi wao.

Katika mambo magumu ambayo mashirika na taasisi za kijasusi ya nchi fulani huwa yanapata wakati mgumu ni kuwajua hawa sleeper agents waliopandikizwa na nchi nyingine ndani yao, unaweza kufanya kazi na boss wako hata miaka 20 na akawa ni mwaminifu sana kwenye kazi zake, mchukia rushwa, mpenda haki, hana skendo yoyote na ukamuamini kwa 100% na uka-share siri za ndani kabisa za kampuni au za kitaifa kumbe ni sleeper agent ambaye anasubiri miaka 25 ijayo aanze kazi ya kuvujisha taarifa.

Katika ulimwengu wa kijasusi sleeper agent bora kabisa ni yule ambaye hahitaji kulipwa na nchi iliyompandikiza mahali yaani ni yule anayeishi kwa kujitegemea kabisa huku akifanya kazi halali kabisa inayomuingizia kipato cha kuishi.
Mara nyingi taasisi za kijasusi ili kuwabaini majasusi pandikizi waliopandikizwa ndani yao kutoka mataifa mengine hutumia mbinu ya kufuatilia miamala ya kifedha kubaini kama kuna fedha zinaingizwa kwa mtu wanayemshuku kutokea nje au ndani ambazo zinaleta wasiwasi, mbinu hii inapofika kwa Sleeper agent huwa inakwama kwa kuwa huishi maisha halali ya kipato halali bila kuwa na mawasialiano na mataifa ya nje kwa muda mrefu wala kutumiwa fedha kutoka nje.

Sifa nyingine ambayo wanaipenda sana kutumia kupandikiza majasusi wa namna hii ni uzawa.
Ili jasusi anayefanya kazi kwa ajili ya nchi nyingine asiwe rahisi kutambulika, hutafutwa mtu ambaye ni mzawa wa nchi hiyo hiyo ambaye anaijua lugha vizuri ya nchi hiyo, mfano Mtanzania anayekijua kiswahili chetu hiki tunachotumia tofauti na mtu aliyejifunzia ukubwani.

Wengi wao wa majasusi hawa hufundishwa kazi za kijasusi wakati wa scolarships, japo si kila mtu anayepata scholarship ni jasusi, ila mara nyingi nchi kubwa zinapotaka ku-recruit hawa sleeper agents hutangaza scholarships say ya watu hata 1000, kati ya hao 1000 wanaweza kuchukuliwa watatu tu wakafundishwa kazi ya kuja kufanya miaka 20 ijayo, huku wale 997 wakiachwa waendelee na life yao kama kawaida.

Baada ya Scholarship wale ma-agents hurudishwa nchini mwao wakiwa kama wazalendo wengine wa kawaida wakiendelea kuitumikia nchi yao huku wakisubiri wakati wa kuanza ujasusi ufike.

Nchi nyingi zenye mapigano kama Somalia, Rwanda,Nigeria,Burundi, Congo, Angola, Sudani ya Kusini, Syria, Iraq na ambazo raia wake wanakimbia nchini mwao kwenda nchi nyingine kutafuta hifadhi ya ukimbizi huwa zimejaa sana hawa ma sleeper agents maana wengi hufundishwa ujasusi wakati wakiwa huko ukimbizini kwa ajili ya kazi ya siku za usoni kuvujisha taarifa za siri mara watakaporejea nchini mwao.

Mchezo huu wa ku-insert sleeper ajant huyu ni kama kamali maana karibu 50% hushindwa kufanya kazi mara muda unapofika kuanza kufanya kazi zao kutokana na sababu za kibinadamu au kupandikizwa mahali ambapo sipo, ndio maana huhitajika ku-train wengi ili hata kama nusu wakishindwa basi nusu itaendelea na jukumu lao.

Nchi ya Urusi mara nyingi huitumia nchi ya Canada kama sehemu ya kuwa-train hawa ma-agents kabla ya kuwapandikiza Marekani na Uingereza kutokana na undugu na kufanana kwa tamaduni baina ya Canada na Mmarekani.

Mara nyingi hutafutwa Mkanada kwa siri kubwa sana na kufundishwa ujasusi na Warusi na baadaye Mkanada huyu huomba kibali cha kuishi Marekani au Uingereza.
Baada ya kufanikisha kupata kibali hukaa muda mrefu akiendelea na kazi zake kama kawaida mpaka kipindi cha kazi kitakapowadia, na kwa kuwa muingiliano kati ya Mmarekani na Mkanada ni mkubwa sana ni ngumu sana kujua ni nani aliyepenyezwa na ni lini kapenyezwa.

Israel pia imekuwa ikutumia sana mbinu hii kwa nchi za kiarabu hususani Syria na Iran, siri nyingi za mahali mahandaki ya silaha yaliyokuwa yamefichwa kwenye milima ya Golan zilivujishwa na hawa ma-sleeper agents na kupelekea mafanikio makubwa katika vita ya siku sita.
Mara nyingi Wa-Iran wamekuwa wakilalamika siri zao kuvuja na wanasayansi wao wakubwa kuuliwa na wa-Israel kimya kimya lakini ilikuja kukugundulika kuwa wengi wa wanaovujisha siri hizi na kufanya mauwaji haya ni ma sleeper agents ambao walipandikizwa miaka hata 20 huko iliyopita na wameshajipenyeza kwenye nyadhifa nyeti za kiutawala huku wakiwa watumishi watiifu na wazalendo kwa taifa lao na wengine wakiwa ni hao hao wanasayansi.

Mifano ya hawa ma Sleeper agents waliowahi kufanya misheni zao kwa mafanikio makubwa:
  • Jasusi Otto Kuehn na familia yake waliopandikizwa Hawaii Marekani na Wajerumani kabla ya vita ya pili ya dunia, hawa aliisaidia sana Japani kuweza ku-plan shambulio la Bandari ya Pearl.
  • Kim Philby alifundishwa ujasusi na Warusi wakati anasoma Chuo Kikuu na baadaye pandikizwa kwenye Serikali ya Uingereza, alifanikiwa kupata vyeo vikubwa na hatimaye kuwa kuingo maalum sana wa joint operations za kijasusi za Uingereza na Marekani bila kujulikana huku akiwafanyia kazi Urusi.
  • Shirika la Kijasusi la Nigeria liliwakamata aksari wake wawili waliokuwa wamepenyezwa kwenye jeshi lake na kikundi cha waasi cha NDA kama sleeper agents, walikuja kukamatwa baada ya plot yao ya kumuua kamanda mmoja mahiri aliyekuwa anaongoza operations za kijeshi kwenye jimbo la Kaduna kushindwa.
  • Mwaka 2015 Serikali ya Pakistani iligundua uwepo wa sleeper agents 200 waliokuwa wamepandikizwa kwenye makundi ya kigaidi yaliyoko Pakistani kutokea India, Hii ilitokea baada ya majasusi wanne kugundulika na mamlaka za Pakistani na baada ya kuteswa walivujisha siri kuwa shirika la kijasusi la India la RAW limepandikiza majasusi 200 ndani ya Pakistan ambao wanafanya kazi kama sleeper agents kwenye makundi ya kigaidi wakiwa na kazi ya kuwaua wanasiasa wa Kipakistani na watu wengine mashuhuri.
Nchi tajiri zikishasoma trend ya nchi fulani kuwa soon itainuka kiuchumi, hutumia mwanya huo ku train ma sleeper agents wa kutosha na kuwapenyeza kwenye nafasi nyeti za nchi hiyo ili baadaye kutumika kuvujisha siri siku za usoni.
 
Asante sana....interesting sana. Ila Sasa huyu sleeper kama hawez kulipwa kwa kuwa anaweza kugundulika....hyo kazi yake ambaye inaweza kumsababishikia kifo ina faida gan kwakweli?!
Mara nyingi huanza kulipwa kazi ikianza au fedha zake huwekwa offshore account, na wengine huwa wana taasisi za kijamii say taasisi inayoelimisha jamaa juu ya madhara ya kukeketa watoto wa kike, ambazo hupokea misaada ya kifedha kutoka kwa wafadhili, nyingi ya fedha za ufadhili wao hutoka huko.

Japo si wote wanaofadhiliwa ni ma agent.
 
Namtafuta aliyenidanganya kuwa Tanzania ni ya Tatu kwa ubora kwenye ulimwengu wa ushushu.
Vichaa Tanzania ni mashushushu
wapiga debe mashushushu
yaani kila MTU shushushu na ushushu hawaujui
ha ha ha
mkuu Bujibuji enzi zile za Ujinga alizokuwa anatawala Mwalimu mbinu hiyo ilikuwa inatumika sana hasa kukusanya taarifa za mitaani.

Ila inapofika suala la kukusanya taarifa kwenye ehemu nyeti kama sema wizara ya Ulinzi au fedha pale, huwezi kuweka kichaa.
 
Naamini wamejaa Sana Tz kutokea Marekani,Urusi.

Usikute hata mimi ni mmoja wao.🙂🙂🙂🙂🙂
TISS samahanini lakini!
Nchi hizi masikini ni dampo mkuu.

Kuna kila aina ya mtu humu, kama Marekani waliweza kupenyeza ma Sleeper agents ndani ya Serikali ua Urusi na KGB yao watashindwa kweli kupenyeza huku kwetu ambapo bado hata mawasiliano ya Ikulu yalikuwa yanatumia email za domain ya yahoo.??
 
Nchi hizi masikini ni dampo mkuu.

Kuna kila aina ya mtu humu, kama Marekani waliweza kupenyeza ma Sleeper agents ndani ya Serikali ua Urusi na KGB yao watashindwa kweli kupenyeza huku kwetu ambapo bado hata mawasiliano ya Ikulu yalikuwa yanatumia email za domain ya yahoo.??
Mkuu na mimi huwezi kunipandikiza sehemu? Hahahaha
 
Nchi hizi masikini ni dampo mkuu.

Kuna kila aina ya mtu humu, kama Marekani waliweza kupenyeza ma Sleeper agents ndani ya Serikali ua Urusi na KGB yao watashindwa kweli kupenyeza huku kwetu ambapo bado hata mawasiliano ya Ikulu yalikuwa yanatumia email za domain ya yahoo.??
Hizi njia siamini kama zinatumika sana kwa nchi za kiafrica ukitaka kupata data we toa mkwanja hadi nyaraka muhimu za ikulu unaletewa!

Waafrica wanapenda sana hela
 
niliwahi kuckia kuwa Yelestin Gorbachev rais wa Urusi zama zile inasemekana alipandikizwa na Marekani yaani kuwa alikuwa mmarekani pia, na Soviet ilikuja kuvunjikia mikononi mwake
Sahihisha jina Mzee... umekosea
Mikhail Gorbachev
Former General Secretary of the Communist Party of the Soviet Union
 
Back
Top Bottom