Smartphone za bei rahisi unazoweza kununua

Smartphone za bei rahisi unazoweza kununua

chief-mkwawa Nimefanikiwa kupata HTC Sensation XE.. second hand from UK tatizo limebaki Ku-unlock Network>>>Nimesikia mtaani wanafanya kuanzia 15000 nipeni maujanja wadau niweze unlock mwenyewe

google, kila aina ya simu na mtandao wake una njia za ku unlock hua havifanani. na mara nyingi ku unlock kitu ni hela hua haiwi bure completely
 
Last edited by a moderator:
wakuu kwa yeyote anayejua au mwenye uzoefu kuhusu hizi simu za android naomba anijuze, ni simu gani ya android ni ya bei rahisi kuliko zote?
 
vodafone ya vodacom ndiyo androidphone ya bei nafuu than others.inauzwa 100000 tu.
 
Vodaphone ndio inatangazwa na vodacom kuwa cheapest smartphone lakin kuna matapeli wanaiuza laki 1 na 20 na wengine mpaka laki na 50,cha muhimu tembelea vodashop kwenyewe,,,,,,,ukisha nunua inatumia lain ya voda 2 na inakuwa na mapromoshen kibao kama 3gb za intanet,,,,,,ila unaweza kuiflash ikatumia laini zote
 
Vodaphone ndio inatangazwa na vodacom kuwa cheapest smartphone lakin kuna matapeli wanaiuza laki 1 na 20 na wengine mpaka laki na 50,cha muhimu tembelea vodashop kwenyewe,,,,,,,ukisha nunua inatumia lain ya voda 2 na inakuwa na mapromoshen kibao kama 3gb za intanet,,,,,,ila unaweza kuiflash ikatumia laini zote

shukran mkuu
 
niliwahi kuandika thread kama hii kuhusu simu za bei rahisi za android mwaka 2012 lakini sasa hv imepitwa na wakati na siku zimesogea mbele watu wameomba ile thread tuiupdate ili waweze kufanya maamuzi tena. nimeona nichague simu best za windows phone na android ambazo ni za bei rahisi (chini ya laki 3) ambazo unaweza kutumia ukapata perfomance kubwa kiasi usahau kama ni simu ya bei rahisi nimetumia vigezo vifuatavyo

1. power ya simu -interms ya processor, ram na gpu
2. support- kama itakua updated kwenda version nyengine
3. camera
4. storage
5. battery
6. display
7. weakness zake
mambo kama speed ya internet yamepitwa na wakati simu zote sku hzi zina hspa hivyo speed ipo kama simu ipo slow ni wewe eneo ulipo na mtandao wako ndio munahusika.

hizi hapa ndio simu za bei rahisi nilizokusanya.

nokia lumia 520
kama hujali kutotumia android huwezi pata simu bora zaidi ya lumia 520 kwa bei rahisi, imeuza unit zaidi ya milioni 25 naweza kusema ndio simu maarufu ya bei rahisi zaidi duniani.
nokia-lumia-520.jpg


why ununue hii simu?
1.power- ina processor kubwa kabisa ya s4 snapdragon 1ghz dualcore krait cortex a15, ram 512mb (ipo version ya 1gb inaitwa lumia 525) na gpu yake ni adreno 305
2.suport- simu hii ina windows phone 8 na mwez wa 6 itapata update ya windows phone 8.1
3.camera- ina 5megapixel bila front camera wala flash
4.storage- ina internal 8gb na inakubali memory card
5.battery- 1430mah
6.display- kioo ni 4inch wvga 480x800

weakness zake
1.haina flash ya camera wala camera ya mbele
2. ina apps chache kuliko android

motorola moto e
imezinduliwa muda sio mrefu na ni moja kati ya simu nzuri za bei rahisi inayokupa ram ya 1gb, hebu tuone inapambana vipi na wenzake
motorola-moto-e.jpg


why ununue hii simu
1.power- processor ya 1.2ghz cortex a7 dualcore snapdragon 200 ikiwa na ram 1gb na gpu ya adreno 302
2. support- simu hii inakuja na android kitkat 4.4.2 na motorola wamesema itapata update zijazo
3.camera- ina camera 5mp bila flash wala camera ya mbele
4.storage- simu hii inakuja na internal storage ya 4gb na inaingia memory card
5.battery- 1980mah
6. diplay- ina kioo cha 4.3 inch qhd resolution ya 540x960 kioo chake pia kina gorila glass 3

weakness
1. haina flash wala camera ya mbele
2.processor za cortex a7 zimepitwa na wakati

sony xperia e1
sony nao hawakua nyuma kutoa simu nzuri ya bei ya chini tuangalie nayo ipoje
sony-xperia-e1.jpg


ina sifa hizi
power- ipo kama moto e ikiwa na dualcore 1.2ghz cortex a7 na adreno 302 sema hii ina ram 512mb
support- simu hii inakuja na android 4.3 na itapata update ya kitkat
camera-ina 3mp bila camera ya mbele
storage- ina internal 4gb na memorycard inaingia
battery-1700mah
diplay- kioo cha inch4 wvga 480x800

weakness
-camera 3mp bila camera ya mbele inapitwa na wapinzani wote
-processor cortex a7 ni ya kizaman

blackberry z3
usije kuchanganya na bb z30 hii ni smartphone ya bei rahisi ya blackberry imeanza kuuzwa indonesia specs zake hazina mfano
blackberry-z3-new.jpg

power- inakuja na snapdragon 400 1.2ghz dualcore ram 1.5gb na adreno 305
support-inakuja na bb os 10.2.1 hii ni os yao mpya
camera- camera ya nyuma ni 5mp na ya mbele ni 1.1mp ina uwezo wa kurekodi full hd camera yake.
storage-ina internal 8gb na inaingia memory card
battery- 2500mah
display- inakuja na kioo 5inch chenye qhd 540x960

weakness yake ni kwamba bbos haina native apps nyingi compare na wp, android na ios japo ina uwezo wa kufungua android apps

huawei y530
huawei nae hakuwa nyuma kutoa simu za bei rahisi simu hii kama ilivyo moto e inakuja na specs za kisasa
huawei-y530.jpg


perfomance- simu hii inatumia snapdragon 200 dualcore cortex a7 sawa na moto e na kwenye gpu ina adreno 302 pamoja na ram 512mb
support- simu hii inakuja na android 4.3 na haijulikan kama itapata future updates ila ina ui kama ya kizee hivi
-camera ina 5mp nyuma na flash pamoja na camera ya mbele ya vga
-storage ina 4gb internal pamoja na memory card
-baterry ni 1700mah
-display yake ni 480x854 kioo cha ukubwa wa 4.5inch

weakness
1. chip yake ni ya kizaman cortex a7
2. ina ram ndogo 512mb

hizo hapo juu ndio simu nne ambazo nimeona ndio best kwa simu za bei ya chini. kama unataka dualsim kwenye windows phone kuna lumia 635 sijaieka sababu inafanana vitu vingi na hio 520 na bei yake pia ni kubwa kidogo. kuna baadhi ya simu nyengine nzuri nitazimention sijazieka sababu nimeona hazifai kuwa hapo juu.

1.nokia x, x+ na xl sijazieka sababu ya processor ndogo kama huna matumizi makubwa unaweza kuzinunua
2. motorola moto g sijaieka sababu zinauzwa bei kubwa kidogo
3. samsung duos na trend series sijazieka sababu touchwiz ni nzito kwa simu za bei ya chini
4. sijaeka simu yoyote ya mediatek sababu zinacorupt imei, huwezi kuzi update na ni inferior kwa simu za qualcom (simu za mediatek ni kama tecno, galaxy clone, itel na wengineo)
5. huawei y300 pia sjaieka sababu ina processor kama ya nokia x series hivyo kama huna matumizi makubwa haina neno.

kama kuna simu unayoona inafaa iwepo na sijaiweka unaweza kuitaja
 
Hivi Samsung galax Fame inauzwaje unaweza tujiza sifa zake?
 
Hivi Samsung galax Fame inauzwaje unaweza tujiza sifa zake?

bei yake ni kama hizi tu 150,000 hadi 300,000 sema haina hadhi nayo ya kuwa hapa sababu
1.processor yake ni single core za hapo juu zote ni dualcore
2.kioo cha 3.5 chenye resolution ndogo
 
Nilikuwa naiwazia y300, kumbe si kitu!

sio kwamba ni mbaya ni simu nzuri ila hizo hapo juu ni nzuri zaidi. moto e inauzwa huko duniani dola 117 ndo hzo hzo bei za y300 so ni simu zinazolingana bei ila moto e ina ram 1gb kulinganisha na 512mb ya y300, moto e ina kioo kikubwa cha 4.3 chenye resolution kubwa na battery moto e ni kubwa hata processor ya moto e ni cortex a7 ni kubwa kuliko cortex a5 ya y300
 
Naomba utaje na simu nzuri ambazo ni bora sana za kuanzia 500k hadi milion moja kama hutojali ambazo hazifi haraka chember ya sim Card
 
Back
Top Bottom