Smartphone za bei rahisi unazoweza kununua

Smartphone za bei rahisi unazoweza kununua

niliwahi kuandika thread kama hii kuhusu simu za bei rahisi za android mwaka 2012 lakini sasa hv imepitwa na wakati na siku zimesogea mbele watu wameomba ile thread tuiupdate ili waweze kufanya maamuzi tena. nimeona nichague simu best za windows phone na android ambazo ni za bei rahisi (chini ya laki 3) ambazo unaweza kutumia ukapata perfomance kubwa kiasi usahau kama ni simu ya bei rahisi nimetumia vigezo vifuatavyo

1. power ya simu -interms ya processor, ram na gpu
2. support- kama itakua updated kwenda version nyengine
3. camera
4. storage
5. battery
6. display
7. weakness zake
mambo kama speed ya internet yamepitwa na wakati simu zote sku hzi zina hspa hivyo speed ipo kama simu ipo slow ni wewe eneo ulipo na mtandao wako ndio munahusika.

hizi hapa ndio simu za bei rahisi nilizokusanya.

nokia lumia 520
kama hujali kutotumia android huwezi pata simu bora zaidi ya lumia 520 kwa bei rahisi, imeuza unit zaidi ya milioni 25 naweza kusema ndio simu maarufu ya bei rahisi zaidi duniani.
nokia-lumia-520.jpg


why ununue hii simu?
1.power- ina processor kubwa kabisa ya s4 snapdragon 1ghz dualcore krait cortex a15, ram 512mb (ipo version ya 1gb inaitwa lumia 525) na gpu yake ni adreno 305
2.suport- simu hii ina windows phone 8 na mwez wa 6 itapata update ya windows phone 8.1
3.camera- ina 5megapixel bila front camera wala flash
4.storage- ina internal 8gb na inakubali memory card
5.battery- 1430mah
6.display- kioo ni 4inch wvga 480x800

weakness zake
1.haina flash ya camera wala camera ya mbele
2. ina apps chache kuliko android

motorola moto e
imezinduliwa muda sio mrefu na ni moja kati ya simu nzuri za bei rahisi inayokupa ram ya 1gb, hebu tuone inapambana vipi na wenzake
motorola-moto-e.jpg


why ununue hii simu
1.power- processor ya 1.2ghz cortex a7 dualcore snapdragon 200 ikiwa na ram 1gb na gpu ya adreno 302
2. support- simu hii inakuja na android kitkat 4.4.2 na motorola wamesema itapata update zijazo
3.camera- ina camera 5mp bila flash wala camera ya mbele
4.storage- simu hii inakuja na internal storage ya 4gb na inaingia memory card
5.battery- 1980mah
6. diplay- ina kioo cha 4.3 inch qhd resolution ya 540x960 kioo chake pia kina gorila glass 3

weakness
1. haina flash wala camera ya mbele
2.processor za cortex a7 zimepitwa na wakati

sony xperia e1
sony nao hawakua nyuma kutoa simu nzuri ya bei ya chini tuangalie nayo ipoje
sony-xperia-e1.jpg


ina sifa hizi
power- ipo kama moto e ikiwa na dualcore 1.2ghz cortex a7 na adreno 302 sema hii ina ram 512mb
support- simu hii inakuja na android 4.3 na itapata update ya kitkat
camera-ina 3mp bila camera ya mbele
storage- ina internal 4gb na memorycard inaingia
battery-1700mah
diplay- kioo cha inch4 wvga 480x800

weakness
-camera 3mp bila camera ya mbele inapitwa na wapinzani wote
-processor cortex a7 ni ya kizaman

hizo hapo juu ndio simu tatu ambazo nimeona ndio best kwa simu za bei ya chini. kama unataka dualsim kwenye windows phone kuna lumia 635 sijaieka sababu inafanana vitu vingi na hio 520 na bei yake pia ni kubwa kidogo. kuna baadhi ya simu nyengine nzuri nitazimention sijazieka sababu nimeona hazifai kuwa hapo juu.

1.nokia x, x+ na xl sijazieka sababu ya processor ndogo kama huna matumizi makubwa unaweza kuzinunua
2. motorola moto g sijaieka sababu zinauzwa bei kubwa kidogo
3. samsung duos na trend series sijazieka sababu touchwiz ni nzito kwa simu za bei ya chini
4. sijaeka simu yoyote ya mediatek sababu zinacorupt imei, huwezi kuzi update na ni inferior kwa simu za qualcom (simu za mediatek ni kama tecno, galaxy clone, itel na wengineo)
5. huawei y300 pia sjaieka sababu ina processor kama ya nokia x series hivyo kama huna matumizi makubwa haina neno.

kama kuna simu unayoona inafaa iwepo na sijaiweka unaweza kuitaja

Nini maana ya dual sim?
 
Mi nna Lumia 710, yaani ni choo cha kike, nifanyeje ili niweze kudownload na kutumia huduma za pesa pesa?
Wana JF jaribuni kuipata TECNO PHANTOM A PLUS, hapa wameweza kwa kweli
 
Hivo vimeo vyote, ni vya very low end users....
Bora kutunza hela kununua simu decent.. hizo CPU na GPUs hata decent games hazipeleki labda anayecheza flappy birds.. kama mtu unahitaji smarphone kwa nini utake cha quality mbovu. Tunza hela ununue basi hata nexus 5 $350 au subiri mpya inakuja june inaitwa OnePlus One ambayo itakua $299...
 
Tecno zina tatizo gani mkuu mkwawa? mimi sina ujuzi wa simu kabisa..

tecno zinatumia chip ya mediatek na chip ya simu inajumuisha vitu kama hivi.
-processor
-gpu(kwa ajili ya games na app kubwa)
-fm radio
-network radio mambo ya 3g na 2g

hivyo tunaweza kusema chip zinazoekwa kwenye simu ndio kila kitu sababu mambo yote muhimu yapo kwenye hio chip, chip ikiwa mbaya na simu pia itakua mbaya. mediatek ina matatizo mengi kama.
1.inacorupt imei number na ikicorupt basi huwez piga simu wala kupokea wala kufanya karibia shughuli zote za kisimu hadi uifix.
2. huwezi kuiupdate simu ya mediatek kama inakuja na android 4.1 ili iende 4.2 inabidi ununue simu nyengine
3. simu zote za mediatek zinatumia cortex a7 ila wanatoka processor ya cortexa15 soon. hii processor ya a7 haina nguvu sana.
4. sometime vitu kama gps wifi au bluetooth pia huzingua

ina matatizo mengi meadiatek na pia simu zake ni bei rahisi sana.

incase ndio huna budi inabidi ununue simu ya mediatek zipo simu kali za around dola 130 kama xiaomi hongmi aka red rice na huawei honor 3c unaweza ukazigoogle uone zilivyokua na specs kubwa kwa bei ndogo
 
Hivo vimeo vyote, ni vya very low end users....
Bora kutunza hela kununua simu decent.. hizo CPU na GPUs hata decent games hazipeleki labda anayecheza flappy birds.. kama mtu unahitaji smarphone kwa nini utake cha quality mbovu. Tunza hela ununue basi hata nexus 5 $350 au subiri mpya inakuja june inaitwa OnePlus One ambayo itakua $299...

actual lumia 520 haina c-r-a-p specs sababu even gs3 haina krait ina cortex a9, na lumia 525 inahandle game lolote la kwenye windows phone hadi magame makubwa kama gta san andrea na halo. pia si kila mtu ana uwezo wa kununua simu ya dola 300 ambayo huku itauzwa laki 6 kupanda juu.
 
Mi nna Lumia 710, yaani ni choo cha kike, nifanyeje ili niweze kudownload na kutumia huduma za pesa pesa?
Wana JF jaribuni kuipata TECNO PHANTOM A PLUS, hapa wameweza kwa kweli

1. tecno phantom plus si budget phone sababu bei yake inazidi hio laki 3
2. hata ingekua inauzwa bei ndogo chip yake haikidhi mahitaji ya kuwa hapa.

kuhusu lumia yako unaweza kuihack sababu hio peke ake ndio lumia yenye uchochoro wa kufanya unavyotaka
 
1. tecno phantom plus si budget phone sababu bei yake inazidi hio laki 3
2. hata ingekua inauzwa bei ndogo chip yake haikidhi mahitaji ya kuwa hapa.

kuhusu lumia yako unaweza kuihack sababu hio peke ake ndio lumia yenye uchochoro wa kufanya unavyotaka

Chip ya phantom haikidhi kivipi?
Nipe mautundu ya kufanya kuhusu hii Lumia 710 iweze kuwa rafiki
 
Chip ya phantom haikidhi kivipi?
Nipe mautundu ya kufanya kuhusu hii Lumia 710 iweze kuwa rafiki

chip ya phantom plus ni mediatek soma hapo juu nimetaja matatizo yake na hata kama ndio unanunua hio simu ya mediatek why utoe laki 5 wakati zipo za laki 2 zenye specs kama hio?

kuhusu hio 710 google lumia 710 jailbreak utaona tutorial zake ila pima ugumu wake kama huwez achana nayo
 
actual lumia 520 haina c-r-a-p specs sababu even gs3 haina krait ina cortex a9, na lumia 525 inahandle game lolote la kwenye windows phone hadi magame makubwa kama gta san andrea na halo. pia si kila mtu ana uwezo wa kununua simu ya dola 300 ambayo huku itauzwa laki 6 kupanda juu.

Afadhali umesema maana thread yenyewe inajieleza lkn mtu bado anakuja kusema eti simu ni za very low end users. Yeye kama anataka hizo decent basi azifungulie thread then atoe elimu yake atuache wengine tuchambue hizi za bei rahisi.
 
vipi kuhusu lumia naskia hazisupport huduma za kipesa!! Naomba kujua kwa lumia520 kama nayo haisupport!
 
vipi kuhusu lumia naskia hazisupport huduma za kipesa!! Naomba kujua kwa lumia520 kama nayo haisupport!

inaitwa ussd simu zinazotumia windows phone 7 hadi 7.8 hazikubali ussd. ila simu za wp8 na wp8.1 zinakubali ussd hivyo lumia 520 inakubali pia.

ussd.jpeg
 
Nimeipenda sony xperia e1 ingawa hiyo moto e ni kali zaidi,bei ya hiyo sony inarange vp dukani?
 
bei yake ni kama hizi tu 150,000 hadi 300,000 sema haina hadhi nayo ya kuwa hapa sababu
1.processor yake ni single core za hapo juu zote ni dualcore
2.kioo cha 3.5 chenye resolution ndogo

Asante mkuu kuna mtu alitaka kuniuzia 350000 nikagoma
 
Naomba mnielekeze na aina ya vioo ambavyo havivunjiki kirahisi hasa simu ikidondoka, maana uzembe wangu upo kwenye kupasua vioo.
 
Back
Top Bottom