Smartphone za bei rahisi unazoweza kununua

Smartphone za bei rahisi unazoweza kununua

Mkuu chief mkwawa nimekukubali na nimejifunza mengi kutoka kwako...mimi ninashida ya kupasua vioo vya simu ningependa kujua ni smartphone gani ambayo iko na uwezo mzuri ambayo siyo touch screen? Asante chief
 
hapo kwenye kupoteza imei nadhani ni kwa wale tu wanaopenda kufanya rooting na kuweka custom roms tatizo ambalo lipo sana hata kwenye samsung. updates za kitkat za mtk mbona zipo sema ni kwa makampuni machache sana ila wenye tecno wasitegemee updates.
alafu mbona mtk6582 zina perfomance nzuri tu japo ni A7 antutu score ya 17000 plus is good enough kwa matumizi ya kawaida.
downside kubwa ni kwamba mediatek devices zinazopatikana bongo ni zile zenye quality mbovu at higher price sanasana tecno.

hakuna simu ya Android isiyocheat benchmark. ni useless clone zinafikisha had 30000. na hio imei officially mediatek wametoa bado tool ya kufix sasa wewe ukikataa sijui inakuaje

pia humu jf search watu kibao wanalalamika wana tecno na imei zimecorupt
 
sasa hivi ipo dola 59 juz ndio ilikua hio 49 sema simu za ruzuku unajua mpaka uzi unlock?

Amazon.com: Nokia Lumia 520 GoPhone (AT&T): Cell Phones & Accessories

Mkuu hapo nimekuelewa. Ila nilitaka kujua kwa hapa bongo iko bei gani? Na ni mara nyingi tu huwa naingiaga katka mitandao kama ebay na amazon. Kinachonishinda kununua simu ni kwamba, sijui ni jinsi gani nitaupokeaje mzigo wangu na ni wapi? Kwa posta nasikia kuna upotevu wa mizigo. So inakuwa ngumu kufanya hyo inshu ya kununua online
 
Mkuu chief mkwawa nimekukubali na nimejifunza mengi kutoka kwako...mimi ninashida ya kupasua vioo vya simu ningependa kujua ni smartphone gani ambayo iko na uwezo mzuri ambayo siyo touch screen? Asante chief

siku hizi ni ngumu kupata smartphone ambayo sio touchscreen ya kisasa.
 
Mkuu mimi nina swali kuhusu galaxy mega 6.3 ina maana hii simu kioo chake hakina protection mfano gorilla glass kama zilivo s3 n.k ? pia nauliza ina maana jelly bean yake ndo imeishia hapo hapo kwenye 4.2.2 ?? Tatu na mwisho os vesrsion inapozidi kuwa updated ina faida gani,mfano 4.2.2 ina tofauti gani na 4.4.2 ??
 
Thanks C/Mkwawa for useful info, nauliza, nikitaka kumnunulia mtu zawadi Samsung S 5 ya clone mpya ambaye sio mtaalam wa mambo ya sim, je ataweza kujua kama hio sio original ? Yaani kuna namna awezagundua kirahisi ?

Ha ha bila shaka ni mupenzi loo nimechoka.
 
Ha ha bila shaka ni mupenzi loo nimechoka.

Not at all dear Amu..kuna watu wengine wanaokutengenezea mambo yako huwezi kumshukuru kwa pesa, unampa zawadi ya kitu, tena humpi yeye, unampa mwanaye..they'll never forget you easily..!!
 
Not at all dear Amu..kuna watu wengine wanaokutengenezea mambo yako huwezi kumshukuru kwa pesa, unampa zawadi ya kitu, tena humpi yeye, unampa mwanaye..they'll never forget you easily..!!

Hiyo ni nzuri zaidi nimeipenda ila bana achana na miclone tafuta you will get genuine one with affordable price Huawei g 525 350,000 nafikiri sahivi itakuwa imeshuka.
Ninaitumia haijansumbua kabisa nainjoy
 
bei yake ni kama hizi tu 150,000 hadi 300,000 sema haina hadhi nayo ya kuwa hapa sababu
1.processor yake ni single core za hapo juu zote ni dualcore
2.kioo cha 3.5 chenye resolution ndogo
chief-mkwawa vipi kuhusu Sony Experio C laini mbili? nataka kuinunua,
 
Last edited by a moderator:
Kila simu inategemea wewe unahitaji nini, kumuuliza chief mkwawa bila wewe kueleza unahitaji nini hasa kwenye simu ili na yeye anapoiangalia aweze kushauri kulingana na mahitaji yako. Sasa ukimwambia hii vipi nataka kuinunua utakuwa unataka aingie akilini mwako kujua nini unafikiria au yeye akushauri kulingana na mahitaji yake.
 
niliwahi kuandika thread kama hii kuhusu simu za bei rahisi za android mwaka 2012 lakini sasa hv imepitwa na wakati na siku zimesogea mbele watu wameomba ile thread tuiupdate ili waweze kufanya maamuzi tena. nimeona nichague simu best za windows phone na android ambazo ni za bei rahisi (chini ya laki 3) ambazo unaweza kutumia ukapata perfomance kubwa kiasi usahau kama ni simu ya bei rahisi nimetumia vigezo vifuatavyo

1. power ya simu -interms ya processor, ram na gpu
2. support- kama itakua updated kwenda version nyengine
3. camera
4. storage
5. battery
6. display
7. weakness zake
mambo kama speed ya internet yamepitwa na wakati simu zote sku hzi zina hspa hivyo speed ipo kama simu ipo slow ni wewe eneo ulipo na mtandao wako ndio munahusika.

hizi hapa ndio simu za bei rahisi nilizokusanya.

nokia lumia 520
kama hujali kutotumia android huwezi pata simu bora zaidi ya lumia 520 kwa bei rahisi, imeuza unit zaidi ya milioni 25 naweza kusema ndio simu maarufu ya bei rahisi zaidi duniani.
nokia-lumia-520.jpg


why ununue hii simu?
1.power- ina processor kubwa kabisa ya s4 snapdragon 1ghz dualcore krait cortex a15, ram 512mb (ipo version ya 1gb inaitwa lumia 525) na gpu yake ni adreno 305
2.suport- simu hii ina windows phone 8 na mwez wa 6 itapata update ya windows phone 8.1
3.camera- ina 5megapixel bila front camera wala flash
4.storage- ina internal 8gb na inakubali memory card
5.battery- 1430mah
6.display- kioo ni 4inch wvga 480x800

weakness zake
1.haina flash ya camera wala camera ya mbele
2. ina apps chache kuliko android

motorola moto e
imezinduliwa muda sio mrefu na ni moja kati ya simu nzuri za bei rahisi inayokupa ram ya 1gb, hebu tuone inapambana vipi na wenzake
motorola-moto-e.jpg


why ununue hii simu
1.power- processor ya 1.2ghz cortex a7 dualcore snapdragon 200 ikiwa na ram 1gb na gpu ya adreno 302
2. support- simu hii inakuja na android kitkat 4.4.2 na motorola wamesema itapata update zijazo
3.camera- ina camera 5mp bila flash wala camera ya mbele
4.storage- simu hii inakuja na internal storage ya 4gb na inaingia memory card
5.battery- 1980mah
6. diplay- ina kioo cha 4.3 inch qhd resolution ya 540x960 kioo chake pia kina gorila glass 3

weakness
1. haina flash wala camera ya mbele
2.processor za cortex a7 zimepitwa na wakati

sony xperia e1
sony nao hawakua nyuma kutoa simu nzuri ya bei ya chini tuangalie nayo ipoje
sony-xperia-e1.jpg


ina sifa hizi
power- ipo kama moto e ikiwa na dualcore 1.2ghz cortex a7 na adreno 302 sema hii ina ram 512mb
support- simu hii inakuja na android 4.3 na itapata update ya kitkat
camera-ina 3mp bila camera ya mbele
storage- ina internal 4gb na memorycard inaingia
battery-1700mah
diplay- kioo cha inch4 wvga 480x800

weakness
-camera 3mp bila camera ya mbele inapitwa na wapinzani wote
-processor cortex a7 ni ya kizaman

hizo hapo juu ndio simu tatu ambazo nimeona ndio best kwa simu za bei ya chini. kama unataka dualsim kwenye windows phone kuna lumia 635 sijaieka sababu inafanana vitu vingi na hio 520 na bei yake pia ni kubwa kidogo. kuna baadhi ya simu nyengine nzuri nitazimention sijazieka sababu nimeona hazifai kuwa hapo juu.

1.nokia x, x+ na xl sijazieka sababu ya processor ndogo kama huna matumizi makubwa unaweza kuzinunua
2. motorola moto g sijaieka sababu zinauzwa bei kubwa kidogo
3. samsung duos na trend series sijazieka sababu touchwiz ni nzito kwa simu za bei ya chini
4. sijaeka simu yoyote ya mediatek sababu zinacorupt imei, huwezi kuzi update na ni inferior kwa simu za qualcom (simu za mediatek ni kama tecno, galaxy clone, itel na wengineo)
5. huawei y300 pia sjaieka sababu ina processor kama ya nokia x series hivyo kama huna matumizi makubwa haina neno.

kama kuna simu unayoona inafaa iwepo na sijaiweka unaweza kuitaja

Chief Mkwawa na wataalam wengineo,naomba msaada wenu ipi bora kati ya Xperia M na Motorola Moto G?
 
chief-mkwawa ningependa kujua hizi simu za huawei,
Ukinunua na ukitoa betri zinakuwa na series.
Mfano: huawei Y300-100 au huawei Y300-151,je zinautofauti wowote?half inakuwa made in China.

Ahsante.
 
Last edited by a moderator:
Nimepitia specs zake naona kama moto bi zaidi lakini kuna maeneo sikupenda. Muda wa kukaa na charge haujazungumziwa ingawa battery ya moto ni kubwa kuliko ua sony. Pia moto haina expandable memory kwa hiyo kama ni mtu wa kutunza madude mengi kwenye simu haikufai.
 
Mi nna Lumia 710, yaani ni choo cha kike, nifanyeje ili niweze kudownload na kutumia huduma za pesa pesa?
Wana JF jaribuni kuipata TECNO PHANTOM A PLUS, hapa wameweza kwa kweli

Mimi mwenyewe Lumia 610 imenikera hapo tu. Nani atusaidie wajamaa
 
CHIEF MKWAWA

Salute kwako mkuu. Swali,kwa hiyo hiyo simu zote za lumia zenye window 8 hadi 8.1 hazina shida na mambo ya tgopesa,mpesa au airtel money? Maana kuna hii taarifa kua wp zinazoishia na 20 mfano lumia 520,620 ndio zinakubali tu zingine zinagoma. Kwa hiyo hiyo hiyo 8 na 8.1 zimemaliza hilo tatizo?

Napenda sim za wp sema hilo tatizo linaniogopesha Chief. Nipe uhakika nihamie window phone.
 
Last edited by a moderator:
Nimepitia specs zake naona kama moto bi zaidi lakini kuna maeneo sikupenda. Muda wa kukaa na charge haujazungumziwa ingawa battery ya moto ni kubwa kuliko ua sony. Pia moto haina expandable memory kwa hiyo kama ni mtu wa kutunza madude mengi kwenye simu haikufai.

Thanx Kiongozi
 
Back
Top Bottom