Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,662
- 6,888
"Mteja wetu wa Kachumbari ulinufaika sasa hivi una nafasi ya kujishindia milioni 40, Pikipiki 64 na baiskeli 200. Tuma neno CCM kwenda 15016 Kujiunga ni bure." Ujumbe huu umeniudhi sana baada ya kuupata asubuhi hii. Sasa CCM wanaendesha hii bahati nasibu wakati huu wa kampeni kwa nini? Huku sio kuwaghiribu wapiga kura kweli? Sheria ya gharama za uchaguzi na maadili ya uchaguzi yanakubali kweli kitu hiki? Ni sahihi kutunisha mfuko wa kampeni kwa njia hii kweli?
Kwanza sielewi nitume neno CCM kwa misingi ipi? Hivi hivyo vitu wanavyo chezeshea hiyo bahati nasibu vitajumuishwa kwenye gharama za uchaguzi? Na hiyo gharama ya kutuma ujumbe huo bure itaingia kwenye gharama za uchaguzi? Tendwa jamani huko wapi? Mbona unakuwa kama pilato wakati wa hukumu ya Yesu!
Ili nisipate tena SMS kutoka CCM nimei-block hii namba!