Elections 2010 SMS kutoka CCM

Elections 2010 SMS kutoka CCM

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Posts
11,662
Reaction score
6,888
"Mteja wetu wa Kachumbari ulinufaika sasa hivi una nafasi ya kujishindia milioni 40, Pikipiki 64 na baiskeli 200. Tuma neno CCM kwenda 15016 Kujiunga ni bure." Ujumbe huu umeniudhi sana baada ya kuupata asubuhi hii. Sasa CCM wanaendesha hii bahati nasibu wakati huu wa kampeni kwa nini? Huku sio kuwaghiribu wapiga kura kweli? Sheria ya gharama za uchaguzi na maadili ya uchaguzi yanakubali kweli kitu hiki? Ni sahihi kutunisha mfuko wa kampeni kwa njia hii kweli?

Kwanza sielewi nitume neno CCM kwa misingi ipi? Hivi hivyo vitu wanavyo chezeshea hiyo bahati nasibu vitajumuishwa kwenye gharama za uchaguzi? Na hiyo gharama ya kutuma ujumbe huo bure itaingia kwenye gharama za uchaguzi? Tendwa jamani huko wapi? Mbona unakuwa kama pilato wakati wa hukumu ya Yesu!

Ili nisipate tena SMS kutoka CCM nimei-block hii namba!
 
Mbaya zaidi wengine tumepata saa nane za usiku:mad2:
 
Huu ni wizi mtupu
 
si mtume hilo neno muone kitakachotokea Oktoba 31.. au ndio wote mmekuwa "hamdanganyiki"?
 
Simple..just delete and ignore, ila wajinga wa kupenda dezo ni wengi watawapata kiasi fulani
 
sms hizo zinakera but the only way is to delete them or ignore.
 
Mwanakijiji,
kila mtu akijaribu aone nini Kinatokea, atakuwa kachangia CCM tayari kwa ushindi wa kishindo.
DAWA NI Kila apatae huo ujumbe wa Mandisshi afute bila hata kufikilia mara mbili.
 
CCM niwajanja wameona wameshabanwa wametumia pesa za serikali kwenye kampeni sasa wanatafuta njia ya kuzirudisha ili ionekane wao wamechangiwa na wananchi so hawajatumia pesa ya serikali.Tumesha washtukia janja yao hivyo tujitahidi kuwahamashisha na wengine kuwa wasijaribu kujibu maana unaambiwa ni bure ukituma utakatwa hela hakuna kitu cha bure jamani!!

SOTE KWA PAMOJA TUWE MABALOZI KWA WENZETU KUWASHAWISHI WASIJIBU WALA WASITUME SMS YEYOTE ILE KWENDA 15016 KUWA NI VIRUS ITAUWA SIMU ZAO :mad2::mad2::mad2::mad2::mad2:
 
Mtandao gan wamewaluhusu ccm hiv jamaa hawa hawana din au marafiki wa karibu wa kuwaambia ukweli.Tumshilikishe mungu jaman atusaidie
 
CCM niwajanja wameona wameshabanwa wametumia pesa za serikali kwenye kampeni sasa wanatafuta njia ya kuzirudisha ili ionekane wao wamechangiwa na wananchi so hawajatumia pesa ya serikali.Tumesha washtukia janja yao hivyo tujitahidi kuwahamashisha na wengine kuwa wasijaribu kujibu maana unaambiwa ni bure ukituma utakatwa hela hakuna kitu cha bure jamani!!

SOTE KWA PAMOJA TUWE MABALOZI KWA WENZETU KUWASHAWISHI WASIJIBU WALA WASITUME SMS YEYOTE ILE KWENDA 15016 KUWA NI VIRUS ITAUWA SIMU ZAO :mad2::mad2::mad2::mad2::mad2:
Ndugu yangu usithubutu kutuma sms kama hiyo ya kusema namba fulani ni kirusi wakati sio kwa kuwa litakuwa ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria ya mawasiliano. Fanya lolote ufanyalo lakini jitahidi usivunje sheria mwanawane!
 
Huwa najiuliza mfano namba yangu nani aliwapa,kama ni VODA then hawana ustaarabu as wametoa namba yangu bila ridhaa yangu.
They have been flashing izo msg na sometimes ukituma ondoa unashangaa zaendelea kuja MY GOODNESS
 
Kama wapo watakaochangia CCM karne hii uje tuna wajingi wengi;
 
"Mteja wetu wa Kachumbari ulinufaika sasa hivi una nafasi ya kujishindia milioni 40, Pikipiki 64 na baiskeli 200. Tuma neno CCM kwenda 15016 Kujiunga ni bure." Ujumbe huu umeniudhi sana baada ya kuupata asubuhi hii. Sasa CCM wanaendesha hii bahati nasibu wakati huu wa kampeni kwa nini? Huku sio kuwaghiribu wapiga kura kweli? Sheria ya gharama za uchaguzi na maadili ya uchaguzi yanakubali kweli kitu hiki? Ni sahihi kutunisha mfuko wa kampeni kwa njia hii kweli?

Kwanza sielewi nitume neno CCM kwa misingi ipi? Hivi hivyo vitu wanavyo chezeshea hiyo bahati nasibu vitajumuishwa kwenye gharama za uchaguzi? Na hiyo gharama ya kutuma ujumbe huo bure itaingia kwenye gharama za uchaguzi? Tendwa jamani huko wapi? Mbona unakuwa kama pilato wakati wa hukumu ya Yesu!

Ili nisipate tena SMS kutoka CCM nimei-block hii namba!

Fisadi Rostam Aziz anamiliki 35% ya hisa za VodaCom.Fungua http://www.vodacom.co.tz/docs/docredir.asp?docid=3336. Kuna Shareholder mmoja anaitwa Mirambo Ltd ambayo ni ya Rostam. Na Wabongo kwa kutojua kwao wanamchangia chilingi 550 au zaidi kufanikisha kinachoitwa Shinda Mkoko. Tuendelee hivyo hivyo. Wajinga ndiyo waliwao.

Vodacom ina wateja wanaokadiriwa kuwa milioni 4. Magari yako 100. kila gari naamini haizidi millioni 5.

sasa piga hesabu:

4000000*550 = 2 200 00000 (Bilioni 2, iwapo wateja wote wa vodacom watatuma angalau meseji moja. achilia mbali wanaotumia 50000 kwa kucheza huo upatu wa Rostam).

Magari 100*5000000 = 500 000 000.

Hii inatosha kujua Watanzania hatufikirii kwa kiasi gani, na ni namna gani huyu jamaa (Rostam) anavyowaona Watanzania kuwa ni mafala.

Kwa ufupi ni kwamba wanaoshiriki mchezo wa Shinda Mkoko wanachangia CCM bila kujijua.
 
Wakinitumia mimi ninawapeleka mahakamani. Hawa PushMobile wasijifanye wajuaji, uswahiba wao na CCM ni wa kipuuzi!

Sijawahi kuwa mteja wa Kachumbari yao, kwa hiyo wakituma tu, huo ni ushahidi kamili wa kuwapeleka mahakamani kudai fidia ya usumbufu na kuingiliwa faragha yangu (Tort/Infringement of Privacy).

Wanasheria tunao wengi humu ndani, au mnasemaje? Tuwatie kash-kash hawa wapuuzi!

Hahaha!

Anyway, sikutarajia miujiza kutoka kwa mafisadi hawa! Hawana mbele wala nyuma. Wanataka kuwapata wajinga, wapenda dezo, wawape senti zao. WIZI WA MCHANA KWEUPE!

Mungu ibariki Tanzania.

-> Mwana wa Haki
 
kwa uelewa wangu huwezi ukapata sms hizo kama hujajiunga sasa je? wewe ulijiunga au ni suala la upeo wa elimu ulitumiwa sms ukajua ni lotto ya zain,tigo nk.sababu kama wewe hutaki habari za chama au kujishirikisha na bahati nasibu hiyo sio lazima kama huna chambo pumzika kaka
 
kama kuna mtu ambaye anaona ameingiliwa faragha yake nendeni mahakamani.. angalau muoneshe ujasiri kuwa hamjaridhishwa.. haitoshi kulalamika humu.
 
Back
Top Bottom