SMS kwa Kusaga na Clouds FM

SMS kwa Kusaga na Clouds FM

Mi sidhani kama waandaaji ndo walaumiwe, kwani wale wabibi walitishiwa risasi kuingia kwenye hayo mashindanoo?? Na kama ni njaa, mbona wanakuja kutembelewa na ndugu zao wenye afya nzuri tu jamaniii..!
 
ndio hivyo ndugu yangu. kwanini wasiwasaidie tu, hadi wawachezeshe viduku na azonto? mwendeshaji wa kipindi mwenyewe kama mvuta bangi. hana heshima hata kidogo.

Duuh dhambi kweli,basi hapo mabibi watakua wanajionea sawa tu,inamana na hao wadhamini wao wanaona sawa tu??????ama hakika huu ni msiba
 
hata na mm hili limenigusa unajua ni kweli kua hawa team cloudz suala la ubunifu kwao ndo limelala na pia ni wepesi wakuziona fursa na kuz2mia sikatai, lakn kwa hili siyo siri bila kumung'unya maneno wala kung'ata ulimi huu ubunifu siyo wenyewe na hii fursa ina negative imapact ya udhalilishaj wa wa2 wenye umri unaoheshmika ktk jamii kama hawa mabibi ze2 hata kama ni swala la kuwasaidia kifedha lkn co kwa dizaini hii...
 
Yaani hiyo program ya bibi bomba ni udhalilishaji mtupu..

Tafadhali Clouds jaribuni kuangalia hili suala..hizi fursa zingine ni majanga matupu.
 
Wazee wa fursa sidhani kama wanasikia yasemwayo humu. Ni janga juu ya janga na majanga.
 
ninachokiona hawa
mabibi ni wale waliokua hovyo toka enzi za ujana wao ni sawa na hawa tunaowaona sasa kwenye magazeti uchi kila kukicha hivi unafikiri wakizeeka ndio watajiheshim? hivi unafikiri wangekua hawaja chezea ujana wao na kuwa na maisha yao wangejizalilisha?
 
hapo ndo huwa tcra siwaelewagi haWajui majukumu yako wanataka mpaka wabunge waongee bungeni ndo wafanye kazi yao kwani hili swala la udhalilishaji wa mabibi za watu hawalioni mbona hao clouds hawawapeleki bibi zao kwani hawana mpaka wawachukue bibi zetu au ndo kutufanya matahila
 
With all due respect,Mr.Kusaga the don..Timu yako ni wabunifu sawa hilo sipingi ila tuwe wastarabu kidogo.Ile bibi bomba naona kama ni udhalilishaji tu wa watu muhimu na tunaowaheshimu sana katika jamii zetu africa,kuwachezesha kiuduku,sijui azonto,mara ngololo,hipop,bongo fleva si ustaarabu japo ni haki yako kubuni...zile ni shida tu zinawasumbua wale mabibi ungewasaidia tu bila kuwafanya chanzo cha fedha nadhani ungebarikiwa zaidi...sidhani kama sisi bibi zetu tunawezawafanya vile runingani.‪
huwa sitaki hata kuangalia kile kipindi wanatia huruma najiuliza kama mama yangu angekuwa pale anachezeshwa hip hop? jamani hata kama ni kuwasaidia basi tafuta njia nyingine ya staha kidogo labda washindane kusimulia hadith za kale nk. haya bwana pesa ni yako fanya utakalo
 
Back
Top Bottom