silent lion
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 1,278
- 1,794
Kwa heshima kabisa naomba kuleta malalamiko yetu katika jukwaa hili kubwa la Jf.
Hivi sasa kisiwani Unguja kumekua na kasi kubwa ya ujenzi wa Majengo mbali mbali. Ni jambo la heri na jambo la kupongezwa na kwa hakika tunamuunga mkono Mheshimiwa Rais wetu .
Jambo lilonifanya kuleta bandiko hili ni kua ujenzi huu unafanyika katika maeneo ya wazi ambayo tangia ukoloni maeneno haya yamewekwa kwa ajili ya michezo na watoto.
Viwanja maarufu vya Malindi ambavyo vipo karibu na bandari navyo vipo hatarini na serikali imeshatangaza rasmi kuvitwaaa kwa ajili ya ujenzi wa maegesho ya magari.
Ikumbukwe sehemu kubwa ya viwanja hivi imeshanyakuliwa na vigogo na hivo vilivyobaki navyo serikali inavitolea macho licha ya pingamizi kubwa kutoka kwa wakaazi wa maeneo hayo.
Hivyo kwa heshima na taadhima tunaiomba Serikali yetu tukufu ya SMZ na mpendwa Rais wetu , isitishe ujenzi huu kwa maslahi mapana ya vizazi vya sasa na baadae.
Na kwa wanachama wote wa JF mtusaidie kupaza sauti juu ya jambo hili.
Mungu awabariki nyote.
Tuipende nchi yetu.