SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imetangaza mkakati mpya wa kuwataka wawekezaji na watu wenye asili ya Tanzania Bara kusajiliwa na kuanza kulipa kodi ya ardhi ya dola za Marekani 5000 (Sh6.5 milioni), kila mwaka kwa kila hekta moja ya ardhi.
Hata hivyo, SMZ ilisema mwekezaji mwenye asili ya Zanzibar atapaswa kulipa dola 500 (Sh650,000).
Habari ndio hiyo, nashangaa huyo mwandishi wa habari alivyoipamba hii habari kwa kichwa cha kibaguzi na ni kama ni kitu kipya sana! Na humu wengi wameingia mkenge na kuanza kutoa maneno ya chuki!
Lakini Tz kuna tatizo la wananchi wake kulipa kodi... zile dezo za miaka ile zimelipeleka Taifa katika hali mbaya!
Hautakuwa mwisho wa muungano kama walipitisha wimbo wao wa taifa na bendera yao unafikiri hili litawasitua wabara.Unaelewa wabara tunapenda sana sifa.na wengi wao hawana uzalendo na nchi hii.Hebu fikiria baada ya kuruhusu wawekezaji kwenye kilimo kutoka nje sheria ya ardhi ilipitishwa na kuongeza umiliki wa ardhi toka miaka 33 hadi 99.Huo ndio utakua mwisho wa Muungano. Sijui kati ya Bara na Visiwani ni wepi watakaoumia.
watakufanye njaa huku wamejazana bara wanalima mashamba makubwa wanaendesha biashara kubwa za kila aina tatizo hawapeleki pesa zanzibar bari kule kwa mjomba.Nemegundua sasa kumbe dhamira yenu wazanzibar wafe njaa, mnataka wasiwe na hata kamradi hivi ka kujiingizia? wasubiri mgao wa muungano tu mgao wenyewe mpaka mafisadi wajigawie kwanza aaaa mtu kimfaacho chake bwana, kwahili semeni mpaka mdate kama hamtaki kulipa mtahama.
Hebu tulia kwanza. Haya maneno ya Nyerere hapa hayafanyi kazi maana siyo sisi tueanza kuuvunja Muungano na kutenga watu. Tumelilia sana turekebishe mambo na tubaki pamoja. Tumeitwa majina ya ajabu sana, tumenyanyaswa na sasa tunaanza kutengwa waziwazi.
Nyerere huko juu, nafikiri utakuwa na sisi wakati tukiruhusu Wazenji KULA NYAMA YA MTU. Wao ndiyo wataendelea kulana. Kwani sisi kuna kabila linataka kujitenga Tanganyika? Au kuna mtu kasema kabila fulani inabidi litengwe? So longer Wanyamwezi/Wasukuma bado hawana noma, Tanganyika itasimama pamoja.
Mzalendohalisi,
Huyo Mkuu wa kodi wa Zanzibar ametoa vipengele vya sheria yao, yuko makini sana huyo mtu. Kwa nini umkosoe kiongozi anaetekeleza sheria? Wa-bara mnaotaka Serikali itoe tamko kuwafurumusha wapemba Buguruni ni lazima mjiulize kama mnayo sheria. Katiba imewaruhusu Wanzanzibar wawe na sheria zao, za mambo yao. Sisi tulikubaliana nao kwamba chetu chao, chao chao.
Tulikuwa tunaambiwa eti ni hatari kuwa jirani na kisiwa kinaelea elea tu, tukichukue tukimiliki. Hii ndio bei ya haka ka kisiwa, ka nchi kadogo hata Masasi kubwa mara tano unawapa Vice President na Mawaziri na nafasi zaidi ya hamsini kwenye Bunge la majimbo 232. Wamejaa Bungeni, Cabinet, Uongozi wa Vyama, wamejaa Buguruni, Namanga, wamejaa Kariakoo, kila kona. Lakini kwao wao tusijae, kwa mujibu wa sheria. Tulitaka wenyewe hiki ki ndoa hiki, sio Zanzibar ndio tatizo, ni sisi ndio tulijiingiza kwenye huu mkenge.
Nlijua utakuja tu blah blah zako.Naona wadanganyika wanaanza chuki..lol