SMZ yazidi kuubomoa Muungano yataka bara walipe kodi ya ardhi

Wapemba kiwanja chao ni Daraja bovu, tena kuanzia kule Kidatu, Chumbuni hadi karibu na Amani fresh, miaka 30 nyuma Wanyamwezi waliweza kuonekana mitaa hiyo, lakini kwa sasa wanatakiwa wawe mbali zaidi ya Mwera! Mpemba akiingia sehemu shughuli yake inafahamika!
 
Wewe Kibs. Pigisha kura leo pale wanapata CCM. Hiyo namaanisha kuwa Wapemba wengi tu ni Wapenzi wa CCM.
 

Shughuli gani?
 

Na haka ka muungano ni hadithi ya tembo kumeza chura, chura ameanza kukoroma tumboni sasa.
 

Wimbo wa taifa wa Zanzibar ulikuwepo tangia Mapinduzi na ulikuwa ukiimbwa kila siku Televisheni Zanzibar (TVZ) ikianza matangazo au ikimaliza matangazo, hata mashuleni wanafunzi walikuwa wakiimba hivyo haukupitishwa bali labda ulipewa umuhimu zaidi tu - jee unashangaa wazanzibari kusema wao ni nchi leo?, mioyoni mwao wao ni nchi tokea Day 1 ya muungano. Hii bendera ambayo inaonyesha tu kuwa wamekuwa koloni la Tanganyika sijui ni Wazanzibari wangapi wanaijua ilivyokaa au kujivunia kuwa nayo.
 

Na Zanzibar hiyo hiyo imechangia kifedha,vifaa na hata damu wakati mulipomchokonoa Iddi Amini na kukuvamieni, ama kweli mkono mtupu haurambwi, leo hawana kitu munawakebehi.
 

Hivi ukitoa nafasi ya makamu wa raisi na wabunge 50 ambao sababu ya idadi hii imeelezwa uzuri na Mwalimu Nyerere hebu tuelezeni jamani kuna faida gani nyengine ambayo Zanzibar inaipata ambayo isingeliweza kuipata au kujitosheleza kivyake kama ingelibaki kuwa nchi kamili?, nafasi za mawaziri/mabalozi/wakurugenzi ngapi katika SMT zimekuwa allocated kwa wazanzibari ki katiba? - duh!!.
 
Pakacha,
Hakuna lisilowezekana chini ya jua, hebu tuwe serious na haya matatizo kila yakiachiwa yanakuwa na kuongezeka, itafika pahala tutakuwa hatuaminiani tena, maana itakuwa kama ugomvi wa ndoa mwisho wake kuachana baada ya suluhu kushindikana.
 
 
mimi siku zote nasema, muungano sahihi na wa serikali moja na zanzibar iwe si zaidi ya mikoa 2 ya Tz, yaani Pemba na Unguja kama ilivyo Pwani na Dar es salaam. Haiwezekani muungano wa namna hii hata siku moja kero kwisha, kwani zikiisha upande wa Zanzibar, basi zitaanza upande wa bara, kwani wataanza kuhoji kulikoni kutokuwa na equal contribution and representation katika organs mbalimbali.

Mimi ningefurahi kuona hili la serikali moja linawezekana, au basi kila mtu apewe serikali yake na ashiriki kadri ya urefu wa mkono wake!
 

Serikali moja kwa sasa hivi sahau hilo wazo (ingawa ni zuri). tatizo ni kuwa katika hizi mbili wa-Zenj wanadidimizwa jee hiyo moja si masalale. Jitahidini ku-wa treat vizuri katika Serikali mbili na wakiridhika basi moja itakuja tu hatimaye-kila la kheri. Kinyume chake hao Wa-zenj wakiendelea kuhisi kuwa wanabanwa basi hata hizo mbili zitatakiwa ziwe tatu na hapo ndio mwanzo wa kusambaratisha na kugawana mbao.
 
Muungano arudishiwe OBAMA, kwa niaba ya CIA waliotuwekea.

Zenji wanatuona sisi tunawatalawa. Sisi tunaona Zenji wanatuibia na kutunyanyasa.

Ila kama CIA/USA wanataka uwepo Muungano, nani ana ubavu wa kupinga?

Au ndiyo UCHAGUZI unakaribia? Kila mtu anataka aonekane anafanya kazi (Zenji?)

Wabara siye UFISADI unatutesa, ngoja kwanza tuhangaike na MAFISADI na tukimaliza, amini amini nawaambia, kabla Jogoo halijawika mara tatu, KERO YA MUUNGANO ITAKWISHA.
 
Hiki kibao wakigeuziwa Wazenji/Wapemba, pale Buguruni vile vibanda vya mbao naona vitatoweka.
mimi naona hakuna tatizo, sio ubaguzi wala chuki. nchi zote zilizo endelea wanafanya hivyo. mimi naishi nje ya Tanzania na hiyo system inatumika hapa .sio kwa wageni tu ,bali hata raia. Na hata bara wakifanya hiyo system ni sawa tu. kwasababu wazawa wa kila sehemu wana haki ya ardhi na kitakachopatika katika ardhi hiyo. Ardhi ya Tanzania ni mali ya serikali. Ardhi ya bara ni mali ya bara, ardhi ya Zanzibar ni mali ya Wanzibar. Muungano isiwe sababu ya kuibiana ardhi. Mpemba au Mzanzibar anaeishi bara na kumiliki mali yoyote huko bara , anamiliki hivyo viyu kutokana na sheria za Bara .kwani sheria za ardhi nitofauti. Mtanganyika anaeishi na kumiliki mali ya aina yoyote zanzibar , anamiliki vitu hivyo kwa sheria ya Zanzibar. HATA HUKU NJE SHERİA YA MKOA MMOJA NA MWENGİNE ZİNATOFAUTİANA. KUMBUKENI KAMA ZANZİBAR NI NCHI ,NDIO BAADAE UKAPATIKANA HUO MUUNGANO.
 
Ardhi ya Tanzania ni mali ya serikali. Ardhi ya bara ni mali ya bara, ardhi ya Zanzibar ni mali ya Wanzibar.

Hakuna ardhi ya bara. Ardhi ya bara ni ya watanzania wote na ya Zanzibar ni ya wazenji peke yao!

Utatusaidia kama utatutolea mfano wa nchi nyingine ambapo uhuru wa kumiliki ardhi kwa baadhi ya raia unawekewa vizingiti wakati wengine hawana vizingiti!
 
ukianza kuwashambulia wapemba wanaofanya biashara na kuishi hapa Dar au bara utakuwa unakosea

Hapana, ni sahihi kabisa kwani wanatutafuta wabara bila sababu. Waende wakagombane wao kwa wao nyumbani kwao, wakishapatana warudi tuungane. Wakiridhia huko visiwani, wawelezaji wa kipemba nao walipe $5,000 kwa kila hekari ya ardhi Tanzania Bara
 
Hakuna ardhi ya bara. Ardhi ya bara ni ya watanzania wote na ya Zanzibar ni ya wazenji
Kwa maana hiyo Mathalani Mpemba wa Chokocho anapokwenda Sengerema akifika kule akitaka ardhi anaomba kupatiwa ardhi ambayo kihalali ni ya kwake. Lakini Msukuma wa Sengerema akienda Dole na kuomba ardhi pale anomba aredhi ambayo si ya kwake-Lakiniikiwa atakaa pale Dole kwa muda wa mikaka mitano mfululizo anakuwa ni Mzanzibari (kwa mujibu wa sheria ya Mzanzibari). Hivyo atakuwa na haki ya kuomba na kupewa ardhi hiyo. Sasa tatizo lipo wapi hapo. Pengine watu hawaufahamu Mfumo wa Muungano wetu wa Jamhuri moja ya Tanzania ambayo imeruhusu kuwepo kwa Nchi kamili (ndani ya Jamhuri) Zanzibar.
 

Tatizo dilo hilo. Kwa nini ardhi ya Sengerema iwe ruksa kwa mpemba lakini ya Dole iwe marufuku kwa msukuma? hata hicho kipengele cha kukaa mfululizo kina matatizo. Huyo Msukuma akiomba uzanzibari baada ya miaka mitano si atakumbushwa pale alivyoenda kuhani msiba Sengerema akakaa zaidi ya mwezi mmoja! Na kwa hiyo miaka mitano anapofukuzia huo uzanzibari awe analipa hizo dola 5000 kwa kila kihekta kimoja!

Kuujua huu mfumo wetu wa Muungano haumaanishi kuwa kila kitu kifanywacho chini yake ni cha haki.

Amandla......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…