Snura aachana na muziki wa kidunia, aomba nyimbo zake zisipigwe tena, na picha zake zisipostiwe akifariki dunia

Snura aachana na muziki wa kidunia, aomba nyimbo zake zisipigwe tena, na picha zake zisipostiwe akifariki dunia

Kipenzi chetu Imam Hussein aliuwawa kikatili sana Karbala ili kulinda na kuutetea uislamu. Nasi Allah katupa Tawfiq. Lakini cha kuhuzunisha Sunni hawamuenzi Imam wetu wanamdhihaki kumtukana nakutudhihaki.

Allah mwenyez Mungu mwingi wa rehma ampe qaul thabeet kipenzi chetu Imam.
Imam Hussein ndio aliuwawa kikatili Karbala katika kulinda na kutetea uislamu , na hakuna Muislamu mwenye akili timamu ambaye atathubutu kumtukana na kumdhihaki , na sisis tunamuombea kila la kheri kwa Allaah tunampenda na tuna dhana nzuri juu yake.

Mashia wapotofu na wajinga katika dini , wanafuta batili na kuzungumza uongozo sisi hatuko pamoja nao.
 
Aah kumbe watu mna connection za snura na hamsemi
 
Mwanamuziki Snura Mushi ametangaza kuacha muziki huku akikataza nyimbo zake zisichezwe kwenye vyombo vya habari na sehemu nyingine, Hatua hiyo imekuja baada msanii huyo kudai kuwa kwa sasa ameamya kumrudia Mungu wake.

ā€œWatanzania na nje ya nchi mimi Snura leo natangaza rasmi kuwa nimeacha kazi za sanaa nilizokuwa nazifanya. Sababu kubwa ya kuacha ni kumrudia muumba wangu, nifuate dini yangu ya Kiislamu inavyosema na mwanamke wa Kiislamu anavyotakiwa kuwa,ā€ amesema Snura kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Mbali na hilo, msanii huyo amesema anajutia aliyokuwa akiyafanya kipindi akiwa kwenye sanaa.
ā€œNisiwe muongo najutia sana niliyoyafanya na maamuzi yangu ya kuacha sanaa niliyafanya miaka mingi iliyopita, mwanzoni wazo langu lilikuwa kuacha kimyakimya nisiseme kwa yeyote wala popote ijue tu familia yangu, ndugu zangu na watu wanaonizunguka lakini kwa sababu hivi vitu vinaishi miaka na miaka na vizazi vipya vinakuja sitaki kuwa sababu ya kuwaharibu,ā€ amesema.

Katika hatua hiyo ya kutangaza kuacha muziki pia ameomba nyimbo zake kuacha kuchezwa kwenye vyombo vya habari.

ā€œNisingeweza kupita kila redio na Tv kuwakataza wasicheze nyimbo zangu, natumia fursa hii ndugu zangu kwa heshima na taadhima naomba sana mnipokelee ombi langu msicheze kazi zangu kabisa naomba mfute, fanyeni kama hakuna kilichotokea,ā€ amesema Snura.

Snura pia ameomba siku atakayofariki picha zake zisichapishwe kwenye mitandao ya kijamii.

ā€œUkisikia nimekufa umehuzunishwa na msiba wangu njoo unizike kama ni mwanamke usije mtupu njoo na stara, picha ambazo hazina heshima msiposti hayo mapicha wala madude dude kwa sababu naona tukifa hayo madude ndiyo mnaposti,ā€ amesema.

Baadhi ya ngoma alizowahi kutamba nazo Snura kabla ya kutangaza kuacha muziki ni ā€˜Majanga’, ā€˜Nimevurugwa’, ā€˜Chura’, ā€˜Shoga Yake Mama’, ā€˜Ushaharibu’ na ā€˜Shindu’.
 
Mods unganisha huu Uzi na nyingine kama hizi.
 
Binafsi nampongeza sana maisha yenyewe mafupi haya ukipata muda wa kutubu kabla hujatwaliwa ni vyema sana
 
Mwenzake mzee yusuph alisemaga ivoivo ghafla baada ya maokoto kuisha akaamua kurudi tena

Snura ni Ndoa ndo imemfanya aache muziki baada ya kupewa presha na ndugu wa mume. Ngoja aachwe atakuja kuomba radhi watz time will tell.

Lucifer ana nguvu mno.
 
Imam Hussein ndio aliuwawa kikatili Karbala katika kulinda na kutetea uislamu , na hakuna Muislamu mwenye akili timamu ambaye atathubutu kumtukana na kumdhihaki , na sisis tunamuombea kila la kheri kwa Allaah tunampenda na tuna dhana nzuri juu yake.

Mashia wapotofu na wajinga katika dini , wanafuta batili na kuzungumza uongozo sisi hatuko pamoja nao.
Hao mashia ndio walimuua, wahuni tu katika dini na si waislamu
 
Eti ameamua kuwa mtu wa Allah kwani music unawazuia nini kobazi mbona Ali kiba mnapa sifa zote za "ustaadh" na bongo fleva yake au kuvaa juba la kiarabu ndio kubadilika?
 
Back
Top Bottom