Socialphobia, anxiety, depression, panic attack inaniua taratibu! Msaada

Njia za kutatua hilo tatizo ndio utata unapokuja. Inshort sijui ni mtu gani sahihi wa kumueleza matatizo yangu akanielewa na kutunza privacy yangu maana wengi wao siwaamini. Najihisi ni mtu wa ajabu kuwahi kutokea duniani.
Kanisani ndo sehemu sahihi,utapenda mwenyewe ,yaan ni maneno ya baraka tu utakua ukiambiwa mpaka utajipenda mpaka bas,imba kwaya,yaan kuimba kinarelease pain yaan jiulize kwa nin wasouth Africa walikua wanapenda Sana kuimba katikat ya mateso,sababu ndo hiyo ,utaambiwa ww ni wathaman Sana,km una karama yoyote lazima mtumish ataiona iwe kuimba au kuombea watu yaan kanisan kila kitu
 
umemaliza kila kitu, sema kanisa lenye neema ya kinabii ni zuri zaidi, na linaloamini katika kukuza karama na vipawa
 
Unapokua getto kuna vitu hua unaangalia/penda...mfano movie,music or mpira...km kuna kimojawapo unapenda mfano mpira toka nenda either uwanjani or sehemu wanazoonyesha mpira ...baada ya muda utatengeneza marafiki wapya hapo ndio utapata chances zakuongea what your facing and sometimes hutasema bali ilehali yakutojichangaya itaanza ondoka yenyewe.
 
Mwenzio nimezoea ikinijia hio hali nasikiliza zangu mziki kwa sauti kubwa sana baada ya muda inatulia naendelea na yangu
 
Pole napitia the same ndo maana unaona nimereply thread ya mda mrefu kwasababu natapatapa kupata solution maana yangu ipo on edge
 

ukiwa na hela hivyo vyote vitaisha.. tafuta hela
 
Hauna lolote wewe, ushoga tu unakusumbuwa.
 
Same problem, japo nimefanya kazi za kukutana na watu ila hua inanipa wakati mgumu sana
 
Same problem, japo nimefanya kazi za kukutana na watu ila hua inanipa wakati mgumu sana
Pole sana, upo mkoa gani nataka nikuelekeze solution ya tatizo lako.? Huu ni ugonjwa kama magonjwa mengine tu na dawa yake ipo.
 
Pole sana, upo mkoa gani nataka nikuelekeze solution ya tatizo lako.? Huu ni ugonjwa kama magonjwa mengine tu na dawa yake ipo.
Dar es salaam

Swala la social interaction limenishinda kabisa, hata nijitahidi vipi, mambo mengi kama si yote lazima nipambane mwenyewe hamna namna nyingine, na sipendi kujielezea hata kama kuna tatizo dogo inafikia mahala mpaka liwe critical kabisa ndio either nitafute wa kumuelezea na wapo wachache sana na wachache hao wengi wao wanakua hamna msaada wowote wanatoa zaidi ya kuwapa taharifa na ni mpaka waulize tofauti na hapo nitalitatua mwenyewe taratibu

Swala hili linasababisha kua na watu ninao fahamiana nao tu ila si marafiki na sina marafiki kabisa, na nilio nao ni wawili tu, na sina mazoea nao hata ya kuombana misaada

Na enjoy nikiwa mwenyewe zaidi kuliko nikiwa karibu na watu, sikai vijiweni labda niwe nimeenda kwa maelekezo flani au kuna kitu nafuatilia, tofauti na hapo utanikuta nyumbani au kwenye kazi tu, huwezi nikuta bar wala grocery wala kwenye banda lolote la mpira wala kubet

Mziki uliopo nina mke ambae ni tabia zake ni opposite kabisa na mimi nilivyo yaani extrovent jambo ambalo linaibua hitilafu mara kwa mara haswa akitaka kua kama mimi au nikitaka kua kama yeye, nikikagua yaliyo tukutanisha mpaka kuelewana na kuishi pamoja na mpaka kua watoto nabaki kushangaa tu

Kwa ufupi kwa mimi naona kuna faida kidogo kuliko hasara ukiwa na hali kama hii, haswa nikiwa natamani ningekua naweza ku interract na ku cooparate na wengine kama ninao waona, ila swala hilo nime gonga mwamba kabisa na si kwa matakwa yangu binafsi

Nimesha tafuta tiba ya tatizo hili, imeshindikana kabisa, hata kufanyia kazi maoni niliyoyapata, hivyo swala hili limekua kama tatoo halitoki hata niki act
 
Sikia tafuta mti wa mlonge chuma majani yake yatie kwenye chai asubuhi kunywa utakuja kuniambia. Hapa Dar milonge ipo kibao. Hii inakufanya kua mchangamfu na mwenye kujiamini huondoa hofu kabisa na haina madhara kabisa baadhi ya nchi kama ufilipino wao wanatumia majani ya mlonge kama mboga kabisa. Nakuhakikishia utaweza kujielezea hata mbele ya umati.
 
Sikia tafuta mti wa mlonge chuma majani yake yatie kwenye chai asubuhi kunywa utakuja kuniambia. Hapa Dar milonge ipo kibao.
πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ«‘ Dah!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…