Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,379
- 41,294
Alf lela ulela za Bi. Kasinde kabla hajatafakari.
Hii ni maalum kwa kupata simulizi endelevu za Bi Kasinde akiwa chumbani kwake kila apatapo wasaa.
Atachukua kilongalonga chake na kupachika miwani kwenye macho kisha kuanza soga na aliyeko...
K: Mjuba umeshindaje leo?
M: Vibaya sana sijasikia sauti yako..
K: Kwani hujaizoea tuu? Mbona saa hizi nshabwia bangi sauti imekuwa ya zeegee teja ana afadhali.
M: Kasinde hujui tuu, hiyo koroma na kwaruza ya sauti yako mie ndo asusa yangu..
K: Aaahahahahahahahaa Mjuba hebu sema unataka nini acha kunichota kama chepeo la fundi mwashi aahahhahahaaa
M: Eeehehehehe hayo ndo maneno Kasinde, zima taa mie nashusha neti nataka nikusimulie hadithi ya akaja sembamba.....
Ikawa jioni...
Ikawa usiku...
Ikawa usiku wa manane...
Ikawa alfajiri....
Bibi hooiiiii, alma nusura azime, mbiombio mjuba kawahi dripu ya maji ndo vimacho kufumbuka.
NB: Simulizi hizi naziweka kwa namna ya mazungumzo baina ya Kasinde na Mjuba (dialogue) yaani nasimulia yale
nnayozungumza na wajuba nikiwa chumbani na si tunachokifanya.
Kasinde Matata.