Michezo ni matukio au vitendo vinavyohusisha matumizi ya viungo vya mwili kwa lengo la kujenga afya na pia ni ajira. Kwa mantiki hii iwapo nchi ikiweza kwenye michezo kuanzia sasa ni dhairi naiona Tanzania ya miaka 15 yenye mafanikio makubwa.
Michezo ambayo hupendwa sana duniani ni pamoja na Soka, Mpira wa Pete, Mpira wa Kikapu, Mpira wa Wavu, Ngumi na Riadha . Michezo kwa ujumla wake ina faida zifuatazo, ajira, kujenga afya, huleta mshikamano, kuitangaza nchi kimataifa, kuongeza jiografia kwa wachezajina na inaleta fedha za kigeni.
Nchi yetu ina vijana wengi wenye vipaji vya michezo lakini vipaji hivyo vimekufa kwa sababu nchi haikutoa fursa ya kuvitambua na kuweka mpango wa muda mrefu wa kuviendeleza.
Nchi yetu kupitia Wizara ya Sanaa, Michezo na Utamaduni na vyombo vilivyopewa dhamana ya kusimamia michezo vinafanya jitihada kusimamia michezo. Pamoja na jitihada hizo bado kama nchi tunahitaji kujipanga upya kwa kubuni mikakati ya kuendeleza michezo ili baada ya miaka 15 hadi 20 Tanzania niipendayo iweze kupatika kimichezo.
Makala hii imejikita katika kuendeleza mchezo wa soka kwa wanaume na wanawake. Chama cha Mpira Tanzania kimekuwa kikiendeleza timu za vijana katika umri tofauti tofauti na kushiriki kwenye mashidndano ya ndani na kimataifa. Vijana hao daima wanakutwa tayari wamejitafutia misingi ya soka wenyewe mtaani pasipo kuandaliwa kiweledi. Makala hii inalenga kuleta mikakati ya kutengeneza vipaji ili soka iwe sehemu ya moyo wa taifa wa kuwapatia ajira vijana wetu na kuinua pato la taifa.
Mikakati ninayopendekeza ni kwamba serikali ijenge shule kuanzia shule ya msingi hadi sekondari katika kanda nchini ambapo tuanze kwa kuwekeza kwenye mpira wa miguu kwa wanaume na wanawake na michezo mingine itafuata baadae. Nimeona uwekezaji uanze kwa mchezo mmoja kwa kuwa rasilimali ni chache na itakuwa rahisi kujitathmini baada ya miaka 15.
Shule za soka zitakazo anzishwa kwenye kanda zitaanza na shule za msingi kwa kuchukua watoto wa darasa la tano na wataendelea hadi kidato cha sita. Wanafunzi wa kujiunga na shule hizo watapatikana kutoka katika shule za binafsi na serikali zilizopo kwenye kanda husika.
Napendekeza zijengwe shule sita na kanda zitakuwa sita kama ifuatavyo, Mashariki - Pwani, Dar es salaam na Morogoro, Kusini - Mtwara, Lindi na Ruvuma, Kanda za Nyanda za juu kusini - Mbeya, Njombe na Iringa,Kanda ya Ziwa - Mwanza, Kagera, Geita na Mara. Magharibi- Rukwa, Kigoma na Katavi na Kanda ya kati - Singida, Simuyu, Dodoma na Shinyanga.
Shule hizo sita za kanda zijengewe miundo mbinu yote na vifaa vya michezo kwa ajili ya kujifunzia. Pamoja na mambo mengine itapaswa kujengewa viwanja vya michezo na shule hizo ndizo zitakuwa maalumu kuendeleza vipaji na kuvuna wachezaji kwa ajili ya klabu mbalimbali ikiwemo timu ya taifa.
Serikali kwa sasa inajenga shule mpya za sekondari kwa ajili ya wasichana kwa kila mkoa. Kwa hiyo serikali pia ibebe jukumu la kujenga shule hizo 6 maalumu kwa ajili ya soka na baadae itaongeza michezo mingine kutokana na uhitaji na upatikanaji wa rasilimali. Nimependekeza shule hizo zijengwe na serikali kwa sababu sera iliyopo sasa elimu ni bure hadi kidato cha sita. Kwa kuwa shule hizo zitagharimiwa na serikali itatoa fursa sawa kwa watanzania wote wenye vipaji kujiunga na shule hizo bila ubaguzi.
Nimependekeza wanafunzi watakao jiunga na shule hizo waanzie darasa la tano kwa kuwa wengi wanakuwa na miaka 9 hadi 10 na wanakuwa wanajitambua na viungo vyao vinakuwa vimenyumbulika kwa ajili ya mazoezi. Shule za msingi kupitia walimu wa michezo wataanza kuwatambua wanafunzi wenye vipaji vya soka kuanzia darasa la kwanza hadi la nne. Baada ya kuamaliza darasa la nne mchujo wa vijana wa kujiunga shule maalum za soka utanza ngazi ya shule, kata, tarafa, wilaya na mkoa.
Kanda itaanza na wanafunzi angalau 60 hadi 100 kutegemeana na uwezo wa serikali kuwahudumia vijana hao ambao watapaswa kukaa shule za bweni ili kupata ratiba nzuri ya kushiriki mazoezi. Uchujaji wa wanafunzi utashirikisha jopo la wataalamu wakiwemo walimu wa soka waliothibitishwa na mamlaka husika za michezo kwa kuratibiwa na wizara za kisekta yaani elimu,michezo na TAMISEMI.
Matokeo ya uwekezaji huo utaanza kuonekana dhairi baada ya vijana kumaliza kidato cha nne ambapo wengi watakuwa na umri wa miaka 18. Iwapo mpango huu utakubalika na kuanza mwaka wa 2026 baada ya miundombinu kukamilika wanafunzi wataingia darasani mwaka 2027 na watamaliza kidato cha nne mwaka 2034. Kwa hiyo mwaka 2035 tutakuwa na uzao wa kwanza wa vijana wenye vpaji vya soka 600 nchini iwapo serikali itakubali kuanza na vijana 100 kwa kila shule.
Kuhusu swala la walimu wa kufundisha shule hizo, si changamoto kwa kuwa tuna walimu wa kutosha mtaani ambao wamehitimu vyuoni lakini hawana ajira. Pia, kutakuwa na walimu (coach) waliofundisha klabu mbalimbali nchini watahusika kufundisha shule hizo, wachezaji wa soka waliofanikiwa na wenye uzoefu. Vijana hao wakihitimu masomo yao kupitia wizara ya kisekta, mawakala wa wachezaji na wenyewe wataanza kutafuta fursa za kucheza soka ndani ya vilabu nchini, kwenye ligi za wilaya, mikoa, taifa na nchi za nje.
Kwa kushirikiana na Wizara ya elimu hususani kitengo kinachohusika na kuandaa mitaala waandae masomo ambayo yatajikita zaidi kwenye mambo ya michezo hususani kuanzia darasa la tano hadi kidato cha nnne. Miongoni mwa masomo ya msingi ninayopendekeza ni pamoja na historia ya mpira wa soka, sheria na kanuni za soka kutambua haki na wajibu wa mchezaji, sheria za mikataba, sheria za mahusiano kazini,maadili ya mwanasoka, afya ya mwili, afya ya akili, lugha hasa misingi ya lugha kusoma, kuongea na kuandika Kiswahili, Kingereza, Kifaransa, Kispania, Kijerunani, Kireno na Kichina, Saikolojia na Philosofia ya mpira, ualimu wa soka na uamuzi.
Pia vijana wafundishwa namana na kuishi kama mtu maarufu, utunzaji na matumizi bora ya pesa. Aidha, wafundishwe somo la uajasilia mali ili hata kama watakosa fursa ya kuendelea na mpira watafanya ujasilia mali mtaani.
Nihitimishe kwa kusema iwapo andiko hili litafanyiwa kazi naamini tutaitangaza Tanzania duniani kote kupitia vipaji na uchumi utakuwa kwa maendeleo ya taifa na Tanzania niipendayo itapatikana.
Imeandaliwa na,
Email. gobagoba2001@gmail.com
Simu. 0755 650 221

Upvote
10