May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Mimi sio Mchambuzi wa soka lakini kama Shabiki wa soka nimekuwa nikijifunza kla siku kupitia kuangalia Soka.
Baada ya Soka kuonesha mafanikio na ufuatiliwaji mkubwa kama kawaida Wenzetu(haswa Wazungu) waliona fursa na kuigeuza kuwa kati ya biashara kubwa sana Ulimwenguni.
Hivyo basi kama zilivyo biashara nyingine kadri siku zilivyokwenda Soka polepole ikahamishwa kutoka kuwa sanaa ya kuburudisha mpaka kuwa sayansi na Hisabati, na kipaumbele ikiwa ni Timu kupata ushindi.
Mabadiliko ya aina hii yamewaathiri pakubwa Watu weusi labda kuliko Wengine, kwa Weusi Sanaa na Michezo ni eneo tunalolimudu sana labda kuliko Sayansi na Hisabati.
Huwa nikifuatilia hata Mechi za hapa nyumbani pale Timu yenye Wachezaji "wakubwa" dhidi ya wale wanaoonekana wa kawaida tofauti kubwa utakayoishuhudia ni tofauti ya maamuzi ya kila Mchezaji Uwanjani na utagundua ya kuwa kuna upungufu mkubwa unaoonekana kwa timu hizi ndogo.
Na hata kama wataishia kuapata ushindi kwa siku hiyo lakini bado wao ndio watakaoongoza kwa kuwa na maamuzi mabovu kabisa kwa Mchezaji mmoja mmoja ukilinganisha na Wenzao.
Maamuzi ninayozungumzi ni namna Mchezaji anapoamua ampe nani pasi, ampe vipi imfikie, achague upande gani amshinde Mpinzani n.k. Mchezaji kujiridhisha kama kanzu au tobo atakayompiga Mpinzani (opponent) itamnufaisha ama la...na yote haya yanahitaji maamuzi ya papo kwa papo jambo ambalo linawashinda wengi.
Kwa mfano rahisi naweza kutoa kama pale jana Mugalu alipourudisha Mpira nyuma kumpa Morrison wakati yeye anafuatwa na Mabeki wawili kumzuia, si kwamba hilo ndio pekee nililoliona au kwamba Mugalu ndio mchezaji Mahiri zaidi la hasha ila nimetoa tu kama mfano wa maamuzi anayopaswa kufanya Mchezaji ili kuinufaisha timu badala ya kuupoteza Mpira kwa maamuzi mabovu.
Ila kama kufanya maamuzi sahihi itakuwa ni sehemu ya kipaji chako basi ni kheri.
Ukiangalia kwa hali ilivyo kwa sisi Watu weusi tunafanya vizuri sana kwenye michezo inayohusisha uwezo wa Mchezaji mmoja mmoja...Michezo kama Ngumi, Riadha n.k hii tutatawala milele labda tu Wazungu waje na mbinu nyingine ya kulazimisha Michezo hii nayo ifanyike kama timu....na ikishakuwa timu basi ni hisabati.
Na sababu haswa inayotushinda Weusi kuwa na mafanikio kwenye Michezo inayofanyika kwa mfumo wa timu ni kwa sababu timu inahitaji kazi ya pamoja kufikia malengo...ambapo kila anayekuwepo kwenye timu anatakiwa kuwajibika kwa timu yote kisayansi na kihisabati hivyo hapa Kipaji pekee sio kipaumbele.
Kwa mtindo huu timu za Africa itakuwa vigumu sana kuchukua Kombe la Dunia...na hata ikibahatika Mwaka mmoja itawachukua tena miaka kadhaa huko mbeleni.
Kwa hili soka la kisasa ni bora kumfundisha asiye na Kipaji ili mradi tu awe na uwezo wa kuelewa mafundisho kuliko Mchezaji mwenye Kipaji ambaye haelewi chochote anachofundishwa .
Kipaji bila kufundishika sahau kutoboa.