Soka la Tanzania limekua au soka la Afrika limeshuka?

Mkuu, Jiulize tu kwanini Ligi ya China au Saudia sio maarufu kama ya EPL?

Na hakuna MTU ataweka hela yake kwenye Soka ambalo halina Hamasa.
Yaani watu wananunua haki za matangazo halafu wewe unasema hakuna haja ya hamasa, kiaje aisee?
 
Soka letu limekuwa kibiashara,tunaweza kusema biashara ya mpira imekubali bongo.
Soka letu kindanindani limekuwa ila sio kama ambavyo biashara hiyo ilivyokuwa I mean tutasema tumekuwa kindani kutokana na vipaji tunavyozalisha nakucheza katika ligi kubwa zaidi.
Wachezaji wetu wengi wazawa wanacheza nje.. kama hapana basi soka halijakuwa!.

Tulipofikia kibiashara si kubaya na itakuwa ni chachu yakuleta shauku kwa wazawa na vipaji vingi kuibuka zaidi.
 
Kuliko ligi ya DRC?
DRC wana vipaji kuliko Tanzania kwa ujumla wa wachezaji walikua wanalipa vizuri kwenye zile klabu zao mbili kubwa ila vita imewarudisha nyuma,Katumbi kabla hajapata matatizo ya kisiasa na kwenda uhamishoni walikua wapo vizuri kwa timu yake ya mazembe ila baada ya kurudi toka kwenye maswala ya kisiasa inaonekana hawajarudi katikabmsuli ule waliokua nao kabla na Mazembe wameanza upya wamejenga uwanja na kuanza kwenye timu za vijana wamewekeza naona nguvu zimepungua As vita ile yakina Ibenge ilikua hatari na Hela walikua nazo kuka kitu Congo kimetokea kwenye uchumi wao maana hata As vita kama wana mdororo wakiuchumi

Sent from my SM-G9650 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, Jiulize tu kwanini Ligi ya China au Saudia sio maarufu kama ya EPL?

Na hakuna MTU ataweka hela yake kwenye Soka ambalo halina Hamasa.
Yaani watu wananunua haki za matangazo halafu wewe unasema hakuna haja ya hamasa, kiaje aisee?
Hamasa ilikuwepo tangia zamani, haijaletwa na Manara, sijui umezaliwa au umeanza kufuatilia soka lini, ila ushabiki wa Simba na Yanga ni mkubwa kabla hata Manara hajazaliwa
 
Mbona DRC imetulia sasa hivi kuliko enzi za Kabila
 
Hamasa ilikuwepo tangia zamani, haijaletwa na Manara, sijui umezaliwa au umeanza kufuatilia soka lini, ila ushabiki wa Simba na Yanga ni mkubwa kabla hata Manara hajazaliwa
Mkuu, nafikiri wewe ndio una mtazamo wa Usimba na Uyanga. Labda ningetumia jina tofauti na Manara.

Swali unalopaswa kujiuliza ni kwanini hakujawahi kuwa na Uwekezaji mkubwa kama huu huko nyuma licha ya kuwa Ushabiki wa Yanga na Simba ulikuwepo?

Nimetaja watu kama Manara, ndani yake kuna wengi sana, nimetaja media ikiongozwa na Azam, ndani yake zipo mpaka online Tv, nimetaja wawekezaji sio wadhamini wa Timu na Ligi tu, bali pia hao wadau wengine wote wa mpira.

Why Uwekezaji Leo!? Jibu ni Kukua kwa Hamasa. Hii haikuzwi na wafadhili au Azam au Manara peke yake, ni mchango wa wengi sana.

Cha muhimu ni kujua, KUKUA KWA LIGI YETU HAKUNA FACTOR MOJA.
 
Wewe unaonaje?
 
Ilipaswa nikueleweshe tokea hapa
Sio nisichoelewa, usichoelewa wewe ni kuwa watanzania wanapenda mpira tangia zamani, hawahitaji hamasa kuipenda Simba, au Yanga.
Wawekezaji ndio wenye kuhitaji Hamasa ya kutoa hela pasipo hatari ya kupata hasara. Kupenda timu tu haisaidii kuita wawekezaji bila support ya wadau wengine kama media, Ushabiki tu hautoshi.
ni Simba ikifanya vizuri kutokana na uwekezaji wake, na uwekezaji wa kampuni kama Azam, na mashabiki wanahamasika zaidi
Hapo juu ulidai mashabiki hawahitaji Hamasa, hapa unakiri kuwa kuna Kuhamasika zaidi.

Zingatia, UWEKEZAJI NI HESABU, zisipolipa hakuna anayetupa hela pasipo akili.

Watu wamewekeza mpaka Ihefu, SFG, Namungo, nk... Ni lini uliona mafanikio yao? Kwanini hatujawahi ona uwekezaji huo kwa timu ndogo miaka ya nyuma? HAMASA IMEKUA, unawasahau vipi wahamasishaji?
Hao wachambuzi uchwara na wapiga domo , mpira hauhitaji domodomo, ni hela na management nzuri....Dunia nzima, mpira ni uwekezaji na management nzuri
Unatakiwa ujue hilo domo ni sehemu Uwekezaji. Propaganda ni sehemu ya Biashara. Tafakari vema.
 
Mbona DRC imetulia sasa hivi kuliko enzi za Kabila
Ni kweli lakini pia congo wachezaji wengi wazuri wanamilikiwa na watu sio timu na wameona tobo kwa sasa lipo Tanzania kwani ligi yetu baada yao kushuka sisi imepanda na ina promo kubwa Africa pia ni sehemu nzuri ya kutokea kwahiyo biashara nyingi zimekua kuja Tanzania

Sent from my SM-G9650 using JamiiForums mobile app
 
Huyo jamaa ana issue binafisi na Manara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…