Soka la Tanzania limekua au soka la Afrika limeshuka?

Kwa miaka mingi sana vilabu kutoka Tanzania vimekua si lolote si chochote kwenye soka la Afrika mpaka pale Simba SC walipo kata utepe kwa ku Qualify Group stage, kwa umri wangu ndio mara ya kwanza niliona klabu ya Tanzania kuingia group stage licha ya kwamba miaka yote alikuwepo bingwa alie enda kushiriki

Baanda ya miaka kadhaa kwa Simba SC kuendelea kutamba huko kumataifa tumewaona Yanga Sc na wao waki anzisha utawala wao kiasi cha kutinga mpaka fainali shirikisho barani Africa

Msimu huu timu zote mbili zinawania tiketi ya kwenda clabu bingwa makundi, ila tayari Yanga kasha weka mtaji wa ushindi wa goli mbili igenini huku simba wao wakitoka sare na goli mbili za away

Kwa hesabu za kawaida ni kama Yanga amesha fuzu na simba wana zaidi ya nusu ya asilimia kufuzu makundio

Kwa mantiki hii kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika Tanzania inapeleka vilabu viwili makundi ya clabu bingwa Afrika,

Wengi wanachukulia wepesi hili jambo ila sio jambo la kuchukulia wepesi kabisa.
Hii ni zaidi ya achievement.

Swali ambalo nime jiuliza na kukosa majibu haya yanayo endelea ni kwasbabu ya kukua kwa soka la Tanzania au, soka la Afrika limeshuka so na watanzania wana serereka huko?

Kuna siku Yanga na Simba watakutana huko clabu bingwa kwenye mtoano, iwe robo au nusu, au fainali, na hapo ndio patakapo chimbika bila jembe.

Uwekezaji umeongezeka maradufu kwenye soka la TZ.

Wafadhili wakiingia mtini soka letu litarejea kule kule kwa zamani.
 
Mkuu, nafikiri wewe ndio una mtazamo wa Usimba na Uyanga. Labda ningetumia jina tofauti na Manara.

Swali unalopaswa kujiuliza ni kwanini hakujawahi kuwa na Uwekezaji mkubwa kama huu huko nyuma licha ya kuwa Ushabiki wa Yanga na Simba ulikuwepo?

Nimetaja watu kama Manara, ndani yake kuna wengi sana, nimetaja media ikiongozwa na Azam, ndani yake zipo mpaka online Tv, nimetaja wawekezaji sio wadhamini wa Timu na Ligi tu, bali pia hao wadau wengine wote wa mpira.

Why Uwekezaji Leo!? Jibu ni Kukua kwa Hamasa. Hii haikuzwi na wafadhili au Azam au Manara peke yake, ni mchango wa wengi sana.

Cha muhimu ni kujua, KUKUA KWA LIGI YETU HAKUNA FACTOR MOJA.
Hamasa ilikuwepo tangia zamani, ishu ilikuwa ni uchumi, kampuni kama ya Bakhressa na Azam Tv, ambao kwa kiasi kikubwa ndio wamechangia havikuwepo
Makampuni ya kamari kama Sportspesa na M bet, havikuwepo
Pia sera za TFF na serikali kubadilika na kuruhusu wachezaji wengi wa kigeni kusajiliwa tofauti na zamani,
 
Sio nisichoelewa, usichoelewa wewe ni kuwa watanzania wanapenda mpira tangia zamani, hawahitaji hamasa kuipenda Simba, au Yanga,
ni Simba ikifanya vizuri kutokana na uwekezaji wake, na uwekezaji wa kampuni kama Azam, na mashabiki wanahamasika zaidi, hata Taifa Stars ni hivyo hivyo, haihitaji hamasa uchwara bali uwekezaji mzuri na uwanja wa Taifa unakua unajaa,

Hao wachambuzi uchwara na wapiga domo , mpira hauhitaji domodomo, ni hela na management nzuri....Dunia nzima, mpira ni uwekezaji na management nzuri
Kuna kitu hutaki kuelewa sababu ya hisia zako dhidi ya watu fulani.

Kama umefuatilia kwa makini sasa kuna kundi la watu ambao walikuwa hawaendi viwanjani au hawafuatilii sana michezo lakini wanaenda viwanjani na kushabikia sana michezo. E.g. wanawake, watoto na wazee jinsia zote.

Hii inatokana na hamasa za hao unao kataa hawana mchango ktk ukuaji huu wa ubora wa soka letu.

NB: Nimetumia neno michezo sababu pia ngumi nao Wana Anza kupanda juu kama soka.

Media zina mchango mkubwa sana. Na media zinategemea watu kama wachambuzi, wasemaji, wahamasishaji, waongoza vipindi, waandaaji wa vipindi, n.k.

Wadhamini wanajitokeza wanapoona wanaweza kujitangaza kupitia wafuatiliaji wa hao watu kwenye media na viwanjani.
 
Uwekezaji umeongezeka maradufu kwenye soka la TZ.

Wafadhili wakiingia mtini soka letu litarejea kule kule kwa zamani.
Kuna wafadhiri na wadhamini, wafadhiri ni wachache sana ila wadhamini ni wengi na wanafaidika na udhamini wao so usitegemee kuwa wataondoka.
 
Kuna kitu hutaki kuelewa sababu ya hisia zako dhidi ya watu fulani.

Kama umefuatilia kwa makini sasa kuna kundi la watu ambao walikuwa hawaendi viwanjani au hawafuatilii sana michezo lakini wanaenda viwanjani na kushabikia sana michezo. E.g. wanawake, watoto na wazee jinsia zote.

Hii inatokana na hamasa za hao unao kataa hawana mchango ktk ukuaji huu wa ubora wa soka letu.

NB: Netumia neno michezo sababu pia ngumi nao Wana Anza kupanda juu kama soka.

Media zina mchango mkubwa sana. Na media zinategemea watu kama wachambuzi, wasemaji, wahamasishaji, waongoza vipindi, waandaaji wa vipindi, n.k.

Wadhamini wanajitokeza wanapoona wanaweza kujitangaza kupitia wafuatiliaji wa hao watu kwenye media na viwanjani.
Nyie ndio mna hisia za mahaba na hao waropokaji kiasi cha kuwapaisha kuwa eti ndio wameinua mpira wa Tanzania....kama wanaweza kuinua mpira kwa hamasa kwa nini walishindwa kufanya hamasa kwa Taifa Stars? Timu kongwe ikifanya vizuri lazima itapendwa tu sababu ina base ya mashabiki tangu zamani
 
Hamasa ilikuwepo tangia zamani, ishu ilikuwa ni uchumi, kampuni kama ya Bakhressa na Azam Tv, ambao kwa kiasi kikubwa ndio wamechangia havikuwepo
Makampuni ya kamari kama Sportspesa na M bet, havikuwepo
Pia sera za TFF na serikali kubadilika na kuruhusu wachezaji wengi wa kigeni kusajiliwa tofauti na zamani,
Ibaki hivyo Mkuu!
 
Kwa miaka mingi sana vilabu kutoka Tanzania vimekua si lolote si chochote kwenye soka la Afrika mpaka pale Simba SC walipo kata utepe kwa ku Qualify Group stage, kwa umri wangu ndio mara ya kwanza niliona klabu ya Tanzania kuingia group stage licha ya kwamba miaka yote alikuwepo bingwa alie enda kushiriki

Baanda ya miaka kadhaa kwa Simba SC kuendelea kutamba huko kumataifa tumewaona Yanga Sc na wao waki anzisha utawala wao kiasi cha kutinga mpaka fainali shirikisho barani Africa

Msimu huu timu zote mbili zinawania tiketi ya kwenda clabu bingwa makundi, ila tayari Yanga kasha weka mtaji wa ushindi wa goli mbili igenini huku simba wao wakitoka sare na goli mbili za away

Kwa hesabu za kawaida ni kama Yanga amesha fuzu na simba wana zaidi ya nusu ya asilimia kufuzu makundio

Kwa mantiki hii kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika Tanzania inapeleka vilabu viwili makundi ya clabu bingwa Afrika,

Wengi wanachukulia wepesi hili jambo ila sio jambo la kuchukulia wepesi kabisa.
Hii ni zaidi ya achievement.

Swali ambalo nime jiuliza na kukosa majibu haya yanayo endelea ni kwasbabu ya kukua kwa soka la Tanzania au, soka la Afrika limeshuka so na watanzania wana serereka huko?

Kuna siku Yanga na Simba watakutana huko clabu bingwa kwenye mtoano, iwe robo au nusu, au fainali, na hapo ndio patakapo chimbika bila jembe.
Na usemi wa umekutana na timu dhaifu utaishia hapo hapo
 
Yes mkuu,kwa muda mfupi huu tumesogea sana,hofu yangu uwekezaji endelevu?au boss akinuna bakuli linatembea
Mleta Mada kachambua vizuri. Hata hivyo naomba nimsahihishe kidogo. Timu ya Kwanza kutoka Tanzania kucheza Makundi ya CAF Champions League ni Yanga, ilifanya hivyo mwaka 1998. Nakubaliana na wewe kuhusu uwekezaji ambao si endelevu kwani tumekuwa tukitegemea mtu badala ya Timu kuendeshwa kama Taasisi. Ndio maana kuana wakati kwenye mitandao huwa kunachafuka ukisikia Mo anasema bora awekeze kwenye Benki. Suala jingine nakubaliana kuwa kuna mchango wa Azam TV na makampuni mengine ya Azam kwenye promotion na uwezeshaji kwenye Ligi yetu.
 
Nyie ndio mna hisia za mahaba na hao waropokaji kiasi cha kuwapaisha kuwa eti ndio wameinua mpira wa Tanzania....kama wanaweza kuinua mpira kwa hamasa kwa nini walishindwa kufanya hamasa kwa Taifa Stars? Timu kongwe ikifanya vizuri lazima itapendwa tu sababu ina base ya mashabiki tangu zamani
Unafikiri Taifa Stars imefuzu AFCON kwa makosa au bahati pekee?
Imefika pale kutokana na uzoefu au mafanikio yatokanayo na wachezaji toka klabu mbalimbali zinazofanya vizuri ambazo zimefaidika na hizo hamasa na kadhalika.
 
Point yangu haikuwa hiyo, pointi yangu kwenye mfano wa Taifa stars nilitoa nj kuwa, hamasa huwa haisadii kama hakuna uwekezaji kwenye quality ya wachezaji, management na ufundi kiujumla

Kwa kuwa kuna kipindi hao wahamasishaji walipewa kazi na serikali ya kuhamasisha stars lakini haikuzaa matunda, stars haikufanya vizuri na mashabiki hawakuwa wanaenda uwanjani kwa sababu stars haifanyi vizuri

So uhamasishaji wenye impact ya kweli ni ule unao improve quality ya team, hapo mashabiki wa soka lazima waende tu uwanjani

Nikutolee mfano wangu binafsi, nilikuwa sitazami sana mechi za Yanga kama kukiwepo mechi ya Simba au timu kubwa ya nje inacheza, lakini juzi ilibidi nitazame mechi ya Yanga kwa sababu ya quality, beauty, inayoonyeshwa uwanjani, sio kwa sababu wakina Ali Kamwe au Manara wameniambia bali kwa sababu ya quality niliyoiona kwenye mechi zao za awali
 
Nadhani shukrani zianzie Azam media ndo imeleta mabadiliko yote tunayoyaona zile kauli sisi ndo watu wa Mpira zimepungua tangu mpira huanze kuoneshwa hivyo kuleta ushindani unaosaidia ligi yetu iache janja janja ya kusajili magalasa toka nje
 
Back
Top Bottom